Myahudi Jr II
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 6,816
- 8,809
Nakupa Big up sana Mkuu kwa huu uzi. Upo smart Upstairs. Japo najua kwa vile wabongo hatupendi kitu kinaitwa Regulations, Basi watauchukulia huu ushauri wako negative.Kwanza nianze kusema kwamba sina neno baya na mtu yeyote anayejihusisha au kufundisha biashara hii. Ni biashara inayoweza kuwa mkombozi mkubwa kama itafanywa kwa ubunifu, umakini na uangalizi mzuri. Nitaelezea wasiwasi wangu na mawazo yangu ya nini kifanyike HARAKA.
Tumeona biashara nyingi tu mpya ambazo kwa nia nzuri tu, serikali iliziacha zikue bila kuziingilia halafu sheria na miongozo mbalimbali ikatungwa baadae kulingana na changamoto na hali halisi ya hiyo biashara ilivyokuwa. Biashara kama ya bodaboda ni mfano halisi. Na hata drone operation ni biashara nyingine ambayo kwa nia nzuri tu, imeachwa ingawa najua huko mbele mambo yatabadilika. Tofauti na biashara zingine ambazo mara nyingi serikali imekuwa inaziacha zinaanza, na kuzipa muda wa kuji-establish, Forex ina tatizo moja kubwa. Yoyote anayeshiriki anaweka hisia zake kubwa sana kwa hiyo mtu anaposhindwa maumivu yanakuwa makubwa kisaikolojia na hata kimwili. Tusiache kama tulivyoacha biashara ya bodaboda, mpaka watu wapate vilema vya maisha na vifo vinavyoweza kuepukika kwa kuweka tu miongozo na kuisimamia.
Kuna baadhi ya watu bila kutajana majina wamekuwa vinara wa kupromote hii biashara. Binafsi nawapongeza siyo tu kwa jitihada za kusaidia wengine kuinuka kiuchumi lakini hata na wao wenyewe kwa kuona fursa na kuitumia. Nina uhakika kuna watu tayari wamefaidika na mafanikio yao.
WASIWASI WANGU
Tatizo zangu kubwa linakuja kwenye issue nzima ya usajili na regulation ya forex brokers. Sina uhakika brokers wanaofanya online Forex trading wamefika wangapi mpasa sasa hapa Tanzania, ila utapeli wa kwanza kwenye Forex kawaida unaanzia kwenye brokers.
Ni standard practice kwa trainer au training material yoyote inayohusiana na forex trading kuonya kuwa biashara ya Forex trading ina risk kubwa na unaweza kupoteza hela yako yote. Wenyewe wana msemo mmoja, 'only invest money that you can afford to lose'. Ni msemo ambao ningependa tupate tafsiri ya kiswahili kwa sababu unakuambia kila unachohitaji kujua kuhusu risk iliyopo kwenye biashara hii. Kuna na msemo mwingine wanautumia unasema 'past performance is no guarantee of future resuts'. Huu wanauambatanisha kwenye kila 'evidence' au ushuhuda wa matokeo mazuri kwenye trading. Nadhani hii misemo ni sehemu ya kutimiza masharti ya sheria zinazowaongoza?. Kwa kuwa sisi Tanzania hatuna muongozo wowote mpaka sasa, hata hii misemo hamna anayeona umuhimu au mwenye ufahamu wa kuhakikisha anaiambatanisha kwenye hizo screenshots au kabla ya kutoa mafunzo au marketing yoyote inayohusiana na forex trading.
Kuna broker mmoja ambaye tayari anafanya shughuli zake Tanzania nimejisajili kwake na nimeshafanya trade kadhaa, naendelea kukusanya ushahidi wa utapeli anaoufanya na nitauleta hapa wiki ijayo.
MAPENDEKEZO
Wazungu wanasema, 'the genie is already out of the bottle'. Badala ya kuanza kufikiria kuipiga marufuku hii biashara ambayo kama nilivyotangulia kusema, ikifanywa kwa umakini, inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa hili, ni vyema tukaangalia nini kinaweza kufanywa kuepuka utapeli na pia kuhakikisha inawafikia ipasavyo wale wanaoweza kufaidika nayo.
Pendekezo la kwanza. Chombo cha mpito kianzishwe mara moja kitakachoratibu shughuli nzima ya Forex trading Tanzania. Maeneo muhimu yanayohitaji uangalizi wa haraka:
Pendekezo la pili. Taasisi mbalimbali za elimu kama IFM, CBE na hata Open University waanzishe short Certificate programs, kama ya 'Investment and Portfolio Management', ambapo humo humo kutakuwa na mafunzo ya Forex Trading.
- kuratibu mafunzo yote ya Forex trading yanayotolewa na watu, taasisi na makampuni mbalimbali. Hii ijumuishe utoaji wa gharama elekezi, muda stahiki wa mafunzo na hata certification kwa wale wanaofuzu.
- kuratibu uendeshaji wa brokers wote waliosajiliwa Tanzania. Hii ijumuishe kufuatilia utendaji wa kazi wa brokers kuhakikisha hawafanyi utapeli wowote wakati wa kuexecute orders na pia malipo kati ya brokers na traders yanafanyika bila matatizo.
- jukumu la kupokea malalamiko yoyote ya kutoka kwa traders kuhusu broker yoyote na kuyafanyia kazi (sasa hivi ukitapeliwa na broker hivi unaanzia kwenda wapi?).
Pendekezo la tatu. Tusukume tuwe na home-grown Forex brokers. Tayari kuna stock brokers, ni suala la kuwapa incentives mbalimbali hao hao ili watoe huduma ya online forex trading (ambayo by extension pia mtu utaweza kutrade online hata stock zilizopo kwenye Dar es Salaam Stock Exchange). Sasa hivi kijana wa kitanzania aliye Tandale ni rahisi kununua share za facebook na McDonalds kuliko za CRDB au TBL. Hili ni la kuangalia haraka.
Pendekezo la nne. Wadau mbalimbali wapewe motisha ya kuandika na kutafsiri makala na vitabu vya kuhusu Forex trading kwa lugha ya Kiswahili. Mimi nina uhakika itafika wakati hata muendesha bodaboda anaweza kuifanya hii biashara akipewa mafunzo katika lugha na mazingira rafiki.
Post yangu pekee niliyowahi kuchangia humu kuhusu Forex Trading:
Madini yangu kuhusu FOREX Trading!
Atakuoa mkuu shauri yako...Mtapigana hamtashinda. ONTARIO pambana bila kuchoka
nilitaka nikujibu upuuzi wako ulio andika lakini nilipo gundua unatumia Tecno F5 nikaamua niache nimekupunguzia marks zoteBOT wenyewe wanaTrade na hasara wanapata pia na wanajua kabisa kuwa hasara ni njia ya kujifunza
Sent from my TECNO F5 using JamiiForums mobile app
Thanks mkuu kwa maelezo na ushauri bombaKwanza nianze kusema kwamba sina neno baya na mtu yeyote anayejihusisha au kufundisha biashara hii. Ni biashara inayoweza kuwa mkombozi mkubwa kama itafanywa kwa ubunifu, umakini na uangalizi mzuri. Nitaelezea wasiwasi wangu na mawazo yangu ya nini kifanyike HARAKA.
Tumeona biashara nyingi tu mpya ambazo kwa nia nzuri tu, serikali iliziacha zikue bila kuziingilia halafu sheria na miongozo mbalimbali ikatungwa baadae kulingana na changamoto na hali halisi ya hiyo biashara ilivyokuwa. Biashara kama ya bodaboda ni mfano halisi. Na hata drone operation ni biashara nyingine ambayo kwa nia nzuri tu, imeachwa ingawa najua huko mbele mambo yatabadilika. Tofauti na biashara zingine ambazo mara nyingi serikali imekuwa inaziacha zinaanza, na kuzipa muda wa kuji-establish, Forex ina tatizo moja kubwa. Yoyote anayeshiriki anaweka hisia zake kubwa sana kwa hiyo mtu anaposhindwa maumivu yanakuwa makubwa kisaikolojia na hata kimwili. Tusiache kama tulivyoacha biashara ya bodaboda, mpaka watu wapate vilema vya maisha na vifo vinavyoweza kuepukika kwa kuweka tu miongozo na kuisimamia.
Kuna baadhi ya watu bila kutajana majina wamekuwa vinara wa kupromote hii biashara. Binafsi nawapongeza siyo tu kwa jitihada za kusaidia wengine kuinuka kiuchumi lakini hata na wao wenyewe kwa kuona fursa na kuitumia. Nina uhakika kuna watu tayari wamefaidika na mafanikio yao.
WASIWASI WANGU
Tatizo zangu kubwa linakuja kwenye issue nzima ya usajili na regulation ya forex brokers. Sina uhakika brokers wanaofanya online Forex trading wamefika wangapi mpasa sasa hapa Tanzania, ila utapeli wa kwanza kwenye Forex kawaida unaanzia kwenye brokers.
Ni standard practice kwa trainer au training material yoyote inayohusiana na forex trading kuonya kuwa biashara ya Forex trading ina risk kubwa na unaweza kupoteza hela yako yote. Wenyewe wana msemo mmoja, 'only invest money that you can afford to lose'. Ni msemo ambao ningependa tupate tafsiri ya kiswahili kwa sababu unakuambia kila unachohitaji kujua kuhusu risk iliyopo kwenye biashara hii. Kuna na msemo mwingine wanautumia unasema 'past performance is no guarantee of future results'. Huu wanauambatanisha kwenye kila 'evidence' au ushuhuda wa matokeo mazuri kwenye trading. Nadhani hii misemo ni sehemu ya kutimiza masharti ya sheria zinazowaongoza?. Kwa kuwa sisi Tanzania hatuna muongozo wowote mpaka sasa, hata hii misemo hamna anayeona umuhimu au mwenye ufahamu wa kuhakikisha anaiambatanisha kwenye hizo screenshots au kabla ya kutoa mafunzo au marketing yoyote inayohusiana na forex trading.
Kuna broker mmoja ambaye tayari anafanya shughuli zake Tanzania nimejisajili kwake na nimeshafanya trade kadhaa, naendelea kukusanya ushahidi wa utapeli anaoufanya na nitauleta hapa wiki ijayo.
MAPENDEKEZO
Wazungu wanasema, 'the genie is already out of the bottle'. Badala ya kuanza kufikiria kuipiga marufuku hii biashara ambayo kama nilivyotangulia kusema, ikifanywa kwa umakini, inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa hili, ni vyema tukaangalia nini kinaweza kufanywa kuepuka utapeli na pia kuhakikisha inawafikia ipasavyo wale wanaoweza kufaidika nayo.
Pendekezo la kwanza. Chombo cha mpito kianzishwe mara moja kitakachoratibu shughuli nzima ya Forex trading Tanzania. Maeneo muhimu yanayohitaji uangalizi wa haraka:
Pendekezo la pili. Taasisi mbalimbali za elimu kama IFM, CBE na hata Open University waanzishe short Certificate programs, kama ya 'Investment and Portfolio Management', ambapo humo humo kutakuwa na mafunzo ya Forex Trading.
- kuratibu mafunzo yote ya Forex trading yanayotolewa na watu, taasisi na makampuni mbalimbali. Hii ijumuishe utoaji wa gharama elekezi, muda stahiki wa mafunzo na hata certification kwa wale wanaofuzu.
- kuratibu uendeshaji wa brokers wote waliosajiliwa Tanzania. Hii ijumuishe kufuatilia utendaji wa kazi wa brokers kuhakikisha hawafanyi utapeli wowote wakati wa kuexecute orders na pia malipo kati ya brokers na traders yanafanyika bila matatizo.
- jukumu la kupokea malalamiko yoyote ya kutoka kwa traders kuhusu broker yoyote na kuyafanyia kazi (sasa hivi ukitapeliwa na broker hivi unaanzia kwenda wapi?).
Pendekezo la tatu. Tusukume tuwe na home-grown Forex brokers. Tayari kuna stock brokers, ni suala la kuwapa incentives mbalimbali hao hao ili watoe huduma ya online forex trading (ambayo by extension pia mtu utaweza kutrade online hata hisa zilizopo kwenye Dar es Salaam Stock Exchange). Sasa hivi kijana wa kitanzania aliye Tandale ni rahisi kununua hisa za facebook na McDonalds kuliko za CRDB au TBL. Hili ni la kuangalia haraka.
Pendekezo la nne. Wadau mbalimbali wapewe motisha ya kuandika na kutafsiri makala na vitabu vya kuhusu Forex trading kwa lugha ya Kiswahili. Mimi nina uhakika itafika wakati hata muendesha bodaboda anaweza kuifanya hii biashara akipewa mafunzo katika lugha na mazingira rafiki.
Post yangu pekee niliyowahi kuchangia humu kuhusu Forex Trading:
Madini yangu kuhusu FOREX Trading!
Ndo mke wa pili uyo mkuuAtakuoa mkuu shauri yako...
Atakuoa mkuu shauri yako...