Ommy Dimpoz akiri kununua views Youtube kwenye wimbo wa Wanjera

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Kama tunavyo fahamu kwamba Youtube ni Mtandao ambao karibia wasanii na wasio wasanii wote Duniani hu utumia kwa ajili ya kuweka kazi zao ili kuji ingizia kipato kutokana na idadi ya watazamaji. Msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz amekiri kununua watazamaji wa video yake kwenye mtandao huo wa YouTube.

Juzi Ommy Dimpoz alikuwa kwenye kipindi cha Papo kwa papo kinachoruka kila siku ya Jumatano kikiwa live kwenye mtandao wa Twitter. Dimpoz aliulizwa swali na mmoja ya wafuatiliaji wa kipindi hicho kuwa athibitishe ni ki vipi unaweza ukanunua Viewers kwenye mtandao wa Youtube? na majibu ya Ommy Dimpoz yalikuwa ni haya.

“Suala la Views, watu wanavyojua kwenye internet unaweza kucheat kwa mambo mengi sana, watu wana nunua likes Instagram yaani ni vitu vipo wazi na amini kwa watu wengi wa twitter wana elewa zaidi na watu wengi wana elewa mambo hizo za vitu vya ujanja kudanganya.

Tukizungumzia sasa views wa Youtube mimi kuna mtu alinicheki siwezi kusema ni nani? Lakini mtu alinicheki na kuniambia unataka Views? nikamwambia Views how? akaniambia tunaweza kupiga Views mwanangu Youtube, Nikamwambia kweli? unafanyaje yaani nilikuwa nashauku ya kutaka kujua unafanyaje? Kwahiyo nikagundua. Jamaa akaniambia hebu nitumie link basi nikamtumia link, na link yenyewe ilikuwa ni link ya wimbo wa wanjera ilikuwa na Views kama 940,000 na uki angalia Muda ilikuwa kama na mwaka mmoja tayari yaani views wana ongezeka kwa mwendo wa kobe umenielewa?

Basi baada ya masaa kama matano aka niambia cheki? kucheki mzigo tayari una milioni 1 ndiyo mimi nikastuka, aka niambia Are you in? yaani aki maanisha tuanze kupiga kazi, basi na mimi nikaji fikiria, nika muuliza kuna wasanii wanafanya hivyo? akasema ndiyo” Dimpoz alimalizia.
 
Hivi YouTube wapumbavu kiasi gani na washindwe kujua? Kuna watu wanalipwa kwa ajili ya views tu na sio sifa kama za wasanii wa kibongo, huyu kadanganya hapa
 
Sijui kama Omari anajua anachoongea.

Ila kwa kufupisha habari ni kuwa kwanza kushawishiwa na mtu kuwa anaweza kukuongezea views you tube ni kushiriki uhalifu na ipo kinyume na masharti ya uendeshaji wa you tube.

Hivyo basi kwa Omari kukiri hadharani kwamba amewahi kushiriki uhalifu huu anaweza kupelekea akaunti yake kufungwa.

Na ambacho hufanyika haswa ni sawa sawa na wafanyavyo wanao hack account za facebook. instagram n.k...kwa tafsiri nyingine ni uhalifu wa kimtandao.

Na wahalifu hawa mara nyingi huwa na website ambazo tayari zina wafuasi, hutumia kati ya mbinu zifuatazo kufikia malengo yao...moja, kuifanya video kuwa 'automatic' yaani kucheza yenyewe pindi mtu anapoingia you tube (mimi binafsi nimewahi kukumbwa na kadhia hii, kama miaka mitatu iliyopita)mbili, 'kubandika' picha inayomdanganya mtazamaji ili a click Video, ndipo hukutana na kitu tofauti na alichotarajia. tatu, kumlazimisha mtazamaji katikati ya video anayoiangalia kwenda kwenye Video hiyo...kwa kifupi haya yote ni maudhi kwa mtazamaji husika kwani hujikuta hakuitaka hiyo Video.

Hivyo sidhani kama Omari anamaanisha hivi anaposema views zinaweza kununuliwa....nadhani yeye anachomaanisha ni kuwa unaweza tu kutoa pesa na kubandikiwa views unazotaka, la hasha.

Kuna uwezekano kuwa Omari anaongea uongo ili tu kuwafanya watu wawapuuze wale wanaopata views nyingi kwenye Video zao...zoezi sio rahsi kihivyo na unapofanyika huu uhalifu basi ni matokeo ya kuudhi/kudhulumu haki za Watazamaji wengine wa You tube ndio wewe upate hizo views....na kamwe views haziwezi kuwa nyingi kihivyo coz sio Watu wengi watavumilia usumbufu huo bila kuripoti You tube.
 
Kwahiyo na kina Chris Brown,Adelle na wao wananunua viewers? Wale wana views zaidi ya milioni 200 kwenye video zao YouTube
Ommy hajui anachoongea, hakuna Mtu mwenye heshima zake anaweza kushiriki huo uhalifu wa kimtandao wa kudhalilisha...ambao bado hata ni wa kubahatisha na hauna uhakika wowote wa kufanikiwa kwa asilimia mia moja.
 
Anatia kichefuchefu, maneno ya hasiyejua kutafuta kwa bidii yake.
 
"Kuna wasanii wanafanya hvyo?" Swali la kinafki..akwendreee mzk wake hauna radha tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…