Ommy Dimpoz Atoa dukuduku lake Baada ya Kutoa Ngoma Yake ya Kajiandae

The Ideologist

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2012
Posts
486
Reaction score
256
Msanii wa muziki Ommy Dimpoz amedai kuna baadhi ya wasanii wananunua views katika mtandao wa YouTube ili video zao zionekane zimeangaliwa zaidi.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’ akiwa na Alikiba amedai yeye hawezi kufanya mchezo wa kununua views kama baadhi ya watu wanavyofanya.“Mimi nataka kutoa wito maana siku hizi watu ‘wanachiti’ sana hususan kwenye mambo ya views YouTube,” Ommy alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Mimi ningewaambia kitu kimoja fanya ngoma kali video acha watu waangalie,” “kwa sababu naongea kwa uzoefu wangu mimi na video yangu ‘Wanjera’ ilikuwa na views laki tisa, kuna mtu mmoja akaniambia siwezi kumsema ni nani ila aliniambia bwana vipi unataka views YouTube? Nikamuuliza views YouTube kivipi, akaniambia hebu nitumie link ya video yako. So mimi nilikuwa nataka kuprove nikamtumia link ya ‘Wanjera’ na ilikuwa na views laki tisa na elfu nne hivi lakini baada ya kumtumia masaa sita baadae akaniambia angalia kuangalia nakuta na milioni moja,” alifafanua zaidi.

Muimbaji huyo amedai hatua hiyo ilimfanya agundue ni kweli kuna baada ya watu wananunua views YouTube.

Video mpya na muimbaji huyo aliyoshirikiana na Alikiba ina views 607,967 ikiwa na inaelekea wiki ya pili toka iwekwe katika mtandao wa YouTube.

hAHAhaha Mziki Unaelekea Mgumu Sana Bwana Dimpoz Hapa nadhani Unawachokonoa wafuasi wa Simba

Source: Bongo5 & Times fm
 
hiyo ni kweli views huwa zinanunuluwa hata followers wa insta ukitaka wafike million ni sekunde tu we angaliaa siku hizi kila msanii ana followers million ila like hazifiki 100000 hamjiulizi hao mafollowers million huwa wana like wap ??bongo kila kitu ujanja ujanjaaa hata ukitaka bando la mwaka unapata ni ww tu na kujiongeza kwako juana na wtu ujue vitu
 
Kwahiyo wananunua Followers, Subscribers, Viewers, na Tuzo daaah basi wana hela sana. Anyway, wewe Ommy Dimpoz ulitoa sh. ngapi kununua viewers wa wanjera na mimi ninunue? Maana nna kavideo kangu U-Tube kana viewers 263 mwaka wa pili sasa
 
Naona jiwe limetupwa gizani litakayempata ndo huyo huyo, kumbe view zinanunuliwa....kweli bongo nyoso
 
Kumbe dimpoz kwa pozi nae ana wivu wa kitoto kiac hicho, kwel nae hana akili
 

Huyu nae wimbo mwenyewe ni mbaya tena ashukuru kupata hao views
 
Wivu wa kike namna hii ndio unatufanya bongo wasanii wasiendelee!Hivi kweli hajui kama kadri unavyokuwa famous ndio inaongeza viewers u tube?
Basi diamond ana hela sana za kuhongo coz mpaka sasa Salome ina 8mil+
Sikuwahi kufikiria kama ommy nae anauelewa mdogo kiasi hiki
 
Sasahivi mtu msanii akifeli au akitoa kitu nyimbo ikawa tofauti na alivyotarajia anasingizia mwenzake wanaofanikiwa wananunua.
Kwa akili ya kawaida mtu ananunua youtube views alafu yeye anapata faida gani?, wakati kinachofanya youtube wakulipe pesa ni matangazo kutokana na idadi ya views, haiwezekani youtube wawe wajinga wakuachie wewe ununue views alafu wao waje kukulipa mamilioni
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Me nafikiri ni chuki binafsi tu za uyo bwana PKP...sasa kama huna fan base kubwa, unatoa nyimbo ambazo hazieleweki n video zenye low quality hao viewers wengi utawapataje?

Cha msingi afanye mziki mzuri tu aache wivu wa kike kike..OVER
 
sio wote wanaoview video lazima wa like mkuu
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] nyimbo ya kajiandae haina vibes hata ikipigwa clabs beat yake producer alimuibia pesa
Ommy dimpoz alitarajia ngoma itateka lakini imekuwa tofauti
 
Mwenzao anazidi kuchanja mbuga wao wamekalia majungu tu!Haya sasa juz ile mashup ya coke studio sa imetoka ......hata official song hawajaachia ngoma imeenea kinoma mpaka huku Nangwanda bado hawajifunzi kama huyu mwenzao ana kitu cha pekee!
 
Safi Dimpoz.

Hii kajiandae ina trend sana kwenye you tube simply kwakuwa huyu kijana anajiamini.
 
Acha kudanganya watu wewe, mtu kuwa na likes chache haina maana amenunua follows
Mfano selena gomes instagram ana follows zaidi ya 100m lakini akiweka pic au video likes hazizidi milioni 7 , maana yake ni kwamba sio wote wanaoona pic huwa wanalike, wengine ni ghost follows wao kazi yao ni kuangalia pic au kusoma ulichoandika then wanapita zao hawana muda wa ku like wala kucomment
 
Hivi dimpoz anafahamu kuwa huyo anayemsema juzi katoka kupewa tuzo ya heshima na YouTube kwa kuwa moja ya "youtuber" bora afrika.. Ina maana dimpoz anaijua YouTube kuliko wenyewe wenye YouTube???

Dimpoz kwa nyimbo ile mbovu alitegemea nini? Mtoto wa kiume ukifeli kwenye jambo unainuka unapangusa vumbi na kusonga mbele sio kutaka kulaumu watu kwa maisha yako wewe binafsi kufeli.. Wivu wa kijinga kabisa

Unasikia mtu na akili zake anakwambia, wananunua views YouTube, wananunua followers instagram na twitter, wananunua mashabiki wajae kwenye shoo zake, wananunua tuzo, wananunua wananunua wananunua...
Hivi huyo msanini anayenunua kila kitu anapataje hela, maana yeye kila kitu ananunua, so ananufaikaje sasa na mziki wake..

Nasubiria siku si nyingi wataanza kulalamika kuwa tunanunua akili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…