Ommy Dimpoz Atoa dukuduku lake Baada ya Kutoa Ngoma Yake ya Kajiandae

Kwenye mathematics Kuna kitu kinaitwa directly proportional yaani, kama variable ya left side ikiongezeka basi na right side itaongezeka, simple diamond ana followers wengi, likes nyingi, subscriber wengi, show za kumwaga, Bila shaka views watakuwa wengi, alafu mjue mpaka YouTube wameweka awards zao wanalijua hili tatizo na ndio maana huwa wanahakiki viewers na subscribers kama wakigundua wanaiburn account yako, ndio maana ya awards hizo kabla hawajatoa lazima uhakiki ufanyike kuepuka ujanja ujanja, diamond sio viewers tu mpaka mauzo iTunes kwa wasanii wa East Africa anakimbiza, akifuatiwa na eddy kenzo. Ommy we mtoto wa kiume ilo swala ni uzushi kama ngoma imebuma usitafute visingizio, kaa Chini tafakari toa nyingine, we diamond platnumz mpaka wasanii waliomshirikisha video zao zina viewers wengi ambao hawajawahi kuwapata (Jah preyhah, akothee, harmonize, chege na mpaka audio yake ya helo imesikilizwa mara zaidi ya laki nane). Inamaana hawa nao anawanunulia, aache kulalamika afanye kazi kila kitu kinawezekana.Kwa wale kidogo ngeli inapanda waitembelee hii link ya website ya YouTube, Kuna maneno yanasema
'' Views generated by some third-party businesses and services will not be counted or reflected on YouTube, and can lead to disciplinary action against your account, including removal of the video or account suspension.''
ukishasoma na kuipitia hii page nzima,utaona anachokisema ommy dimpoz ni upuuzi, chuki na wivu waki uke wenza.
Increase YouTube views - YouTube Help
 
Mkuu hiyo hello ina laki tisa asa iv inakimbilia million
 
Nasikia ukifikisha viewers sijui laki 5 au milioni 5(sina uhakika kwenye no),YouTube unalipwa dola kadhaa na wamiliki wa YouTube.
 
Kila kitu kinataka pesa!! Unaanza kwa kununua umaarufu then unakula mikataba ya maana!!

Simbaaaàaaaaaaaaa bin laden
 
Acheni kukurupuka.
Ommy dimpoz hajamtaja diamond,
Imebainika watu wanachezasha idadi ya viewers na sio Tanzania tu na inakua ni kujidanganya kwakuwa halipwi kwa hizo namba fake alizojiongezea ila wanakua wanaamini ni sifa .....
Wewe ndio unaekurupuka kwani nani bongo hii akiweka tu video u tube kunafurika? Kwahiyo ommy amewazidi uelewa u tube ambao wanagawa tuzo ? huyo mtu ananunua kwa faida ipi? ni utoto tu, whether alisema kwa nia njema au mbaya
 
Mnadhani atasema nini,ili apate nafuu .......kila msanii sasa hivi njia ya kutoka ni kutupa dongo kwa DIAMOND,mnafikiri warushe kwa nani dongo ili wapate kiki ........ Kama hivi anazungumzwa,mnafikiri angepiga dongo kwa wengine hata hii habari ingefika hapa ........... Wameshajua mwenye muziki wake ni MOND,na hawana namna ya kupita bila kupitia njia hiyo.Nendeni mkaone Insta yake ilivyopata ugeni mkubwa,na leo atazungumzwa sana na hilo ndio lengo lake na atakuwa keshafanikisha hiko.
 
mi mwenzenu sijui siku hizi nikoje,yaaan mtoto wa kiume kulalamalalama or vijembe vya kikekike vimemtawala napatwa hasira na ghadhabu sana natamani ata nimpige ata kofi moja la maana mpaka mkono univimbe nahisi akili ndo itamkaa sawa.
wawe basi kama ney tu makavu live.......sio mtoto wa kiume unazunguka mbuyu utasema unayemsema ni Mungu tuseme atakuzimisha any second.onyesha uana ume wako mface mtu,mchane kama we mwanaume kweli otherwise huna uhakika na unachokiongea au chuki binafsi tu.hadi shishi anawashinda
 

Mziki ni biashara na biashara inaubunifu sio kuimba tu halafu una kaa sebuleni kwako unasubiri call ya promoter,kununua views ni sahihi kabisa kwa wasaka pesa lakini kama unahisi pesa unayopata inatosha na umaarufu ulio nao unatosha
endelea na utaishia kariakoo kama Dully sykes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…