kilwakivinje
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 6,184
- 9,407
Angalia Dimpoz ana subscribers wangapi na Mondi anao wangapi?Msanii wa muziki Ommy Dimpoz amedai kuna baadhi ya wasanii wananunua views katika mtandao wa YouTube ili video zao zionekane zimeangaliwa zaidi.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’ akiwa na Alikiba amedai yeye hawezi kufanya mchezo wa kununua views kama baadhi ya watu wanavyofanya.“Mimi nataka kutoa wito maana siku hizi watu ‘wanachiti’ sana hususan kwenye mambo ya views YouTube,” Ommy alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Mimi ningewaambia kitu kimoja fanya ngoma kali video acha watu waangalie,” “kwa sababu naongea kwa uzoefu wangu mimi na video yangu ‘Wanjera’ ilikuwa na views laki tisa, kuna mtu mmoja akaniambia siwezi kumsema ni nani ila aliniambia bwana vipi unataka views YouTube? Nikamuuliza views YouTube kivipi, akaniambia hebu nitumie link ya video yako. So mimi nilikuwa nataka kuprove nikamtumia link ya ‘Wanjera’ na ilikuwa na views laki tisa na elfu nne hivi lakini baada ya kumtumia masaa sita baadae akaniambia angalia kuangalia nakuta na milioni moja,” alifafanua zaidi.
Muimbaji huyo amedai hatua hiyo ilimfanya agundue ni kweli kuna baada ya watu wananunua views YouTube.
Video mpya na muimbaji huyo aliyoshirikiana na Alikiba ina views 607,967 ikiwa na inaelekea wiki ya pili toka iwekwe katika mtandao wa YouTube.
hAHAhaha Mziki Unaelekea Mgumu Sana Bwana Dimpoz Hapa nadhani Unawachokonoa wafuasi wa Simba
Source: Bongo5 & Times fm
Kwani Ommy dimpoz kamtaja mnunuaji[emoji3][emoji3]Wivu wa kike namna hii ndio unatufanya bongo wasanii wasiendelee!Hivi kweli hajui kama kadri unavyokuwa famous ndio inaongeza viewers u tube?
Basi diamond ana hela sana za kuhongo coz mpaka sasa Salome ina 8mil+
Sikuwahi kufikiria kama ommy nae anauelewa mdogo kiasi hiki
Na Kwa Kuongezea Siyo Kwamba Watu Wote Wanaofollow Wanakuwa Online Muda Wote Msanii AnaopostAcha kudanganya watu wewe, mtu kuwa na likes chache haina maana amenunua follows
Mfano selena gomes instagram ana follows zaidi ya 100m lakini akiweka pic au video likes hazizidi milioni 7 , maana yake ni kwamba sio wote wanaoona pic huwa wanalike, wengine ni ghost follows wao kazi yao ni kuangalia pic au kusoma ulichoandika then wanapita zao hawana muda wa ku like wala kucomment
Ni kweli wanalipa, na wanao cheat wanaweza kufungiwa account, ila unaweza kununua traffic kwa njia ambazo zinaruhusiwa, inategemea unafanyaje, mfano kwa video unaweza uka share kwenye site zenye traffic nyingi kwa kuwalipa wenye hizo site wakuwekee, ukai sponsor video facebook au insta, au mtu akauwekea video yake kwenye account yake ya Youtube yenye subscibrers wengi n.k, na sioni kama kuna ubaya kwa kuwa ni moja ya njia za kujipa promotion kufahamika zaidiHuyu Ommy
kila akiongea anaongea ujinga
na hajifunzi kudanganya
Google wanalipa pesa ukiwa na viewers wengi
unafikiri google wajinga kihivyo wasijue haya mambo?
wapoteze hela zao ovyo ovyo?
Coz kuna malalamishi kibao kwa bwana domo kuwa ananunua views ndo maana watu wanahisi kuwa jiwe limetupwa kwa bwana platinumKwani jamani Dimpoz kamtaja Diamond hapo? wengine tulikuwa hatujui hicho alichokisema,sasa suala msanii anayefanya hivyo hilo ni lenu nyie.
Hata Ali kiba alipondwa sana kuhusu zile tuzo ila mwishowe kapewa.
Hakuna cha ukweli apo ni porojo tu ununue views alafu unafaidika na nnKuna watu wameshaamua kujiajiri kwenye mziki. Kwao mziki ni biashara so ndo wanakofikiria sana jinsi ya kufanya vema zaidi. Kwa msanii aliyepo Bongo na amesha hit international platform sidhani kama anaweza kuinvest sana kwenye kununua views cause fan base yake tayari imeshasambaa vya kutosha across the globe. Anaweza kununua views yes lakini sidhani kama anaweza kuinvest hela nyingi sana kwa ajili ya hiyo.
Ommy anaweza akawa ana ukweli anaoungea lakini pia tuangalie na possibility upande wa pili.
Sasa wasiseme kuwa Dimpoz kamsema Domo.Coz kuna malalamishi kibao kwa bwana domo kuwa ananunua views ndo maana watu wanahisi kuwa jiwe limetupwa kwa bwana platinum
Labda kwa mtu aliyejitoa akili tu ndio anaweza asijue nani anazungumziwa hapo! Wewe unafikiri ata wasema wengine ambao wanafikisha mwezi hata viewers million 1 haijafika?Kwani Ommy dimpoz kamtaja mnunuaji[emoji3][emoji3]
Isipokuwa ninachoamini ni kwamba views za D ni za ukweli ndo maana kapewa tuzo ile na Google ambao ni watu lazima wajiridhishe na authenticity ya hizo views.
Diamond kawanunua mpaka google mkuu
Kawaongelea wote wanao cheatSasa wewe bwana daudi unafikir kamuongelea nani hapo kuhusu kununua viewers huko youtube davido o wizkid?
Dimpoz hajawasema washindi wa tuzo za YouTube.Wewe ndio unaekurupuka kwani nani bongo hii akiweka tu video u tube kunafurika? Kwahiyo ommy amewazidi uelewa u tube ambao wanagawa tuzo ? huyo mtu ananunua kwa faida ipi? ni utoto tu, whether alisema kwa nia njema au mbaya