Ommy Dimpoz ni msanii bora zaidi ya Alikiba

Ligaba

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
1,063
Reaction score
2,874
Hi kwa wanaburudani wote.

Nakumbuka nikiwa mdogo baba aliwahi kuniambia. Mafanikio ya binadamu yoyote yanategemea vitu vikubwa vitatu:-
1. Bahati
2. Kipaji
3. Elimu
Akaniambia kati ya vyote bahati ndio inabeba vyote. Kama huna bahati hata uwe na kipaji vipi bado hutofanikiwa ipasavyo, hata uwe na elimu gani bado hutofanikiwa kulingana na elimu yako. Leo nikifikiria naona majibu kwa ukaribu.

Tuje katika mada. Hii ni opinion yangu na wala sio fact. Nawe unaweza kuwa na yako. Nimemfuatilia msanii Ommy Dimpoz kwa muda mrefu nimegundua jamaa yuko talented enough katika Bongoflava ila naona amekosa bahati. Jamaa anajua sana na hata anajua kubadilika kwendana na wakati, nikajaribu kuangalia sifa na ukubwa anaopewa msanii Alikiba nikaona hastahili alipaswa kuwa chini ya Dimpoz. Mwisho nikapata jibu Alikiba amepata bahati ya kushindanishwa na Diamond Platnumz, hii ni bahati ya mtende vinginevyo saa hizi tungemuongelea Sawa na Marlow.

Hebu angalia kwa mfano wimbo kata wa Dimpoz, ule wimbo angeupata Alikiba Dunia ingejuta, Clouds tungewakoma. Hata angeupata Diamond huu wimbo ungefikisha views 50m, ila mwenyewe sijui kafikisha 6m, hata sijui. Kabla hujabisha kaanze kusikiliza hits songs za Dimpoz zote, sikiliza zote za Alikiba halafu rudi na comment.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
100%, soko la muziki limebadilika sana tangu miaka ya 2011. Mtoa mada uko sawa, ukiangalia trend ya Bwana Omary Nyembo tangu hit song yake ya kwanza 'nai nai' 2011- '12 japo alimshirikisha Ally Salehe Kiba na ngoma zote zilizofuata zilikasimiwa na mandhar ya kisasa.

ANGALABU kwa Kiba hit zake zote zimetanabaiswa na swaga za Cindelella 2007 muziki wa masikion.
 
Ommy dimpoz bado sana kumfikia Kiba...Nyimbo ya Alikiba ya Mshumaa Jamaa amechezea sana Kitu kinaitwa Fasihi...kwa 90% hila kuhusu kata Dimpozi kaimba sana bila creativity / Nadhani Alikiba Ataendelea kukaa Juu wala sio kwa bahati Bali uwezo wake wautungaji Mashahiri.
 
Huu Mshumaa umeuonaje sokoni? Alikiba yuko static sana. Huu wakati nyimbo zinazotoboa ni za kuchezeka zaidi ila Alikiba alitambui kubalance nyimbo zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya Ruby na nandi Nani anajua??

Sent from my I phone
 
OMy Dimpoz karibu nyimbo zake kali zote kamshirikisha Alikiba sasa huo uwezo katoa wapi ?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuunga mkono kwasasa ommy dimpoz anafanya mziki unaopendwa na wengi na ngoma zake zinafanya vizuri kuliko za alikiba ila kwa maana ya kipaji kiba ana kipaji kikubwa kushinda ommy dimpoz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…