Omog anena mazito juu ya safu yake ya ushambuliaji.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Namnukuu.. "Mimi nafikiri baada ya mechi tatu au mbili, kuanzia sasa Simba itakua ni timu yenye safu kali sana ya ushambuliaji. Yapo matatizo madogo madogo ambayo nimekua nikiyafanyia kazi."

Hebu tuzione hizo mechi tatu au mbili ni zipi.

07.09.2016(Wed) Simba SC Vs Ruvu Shooting... MAIN NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
11.09.2016(Sun) Simba SC Vs Mtibwa Sugar... MAIN NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
17.09.2016(Sat) Azam FC Vs Simba SC... MAIN NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
24.09.2016(Sat) Simba SC Vs Majimaji FC... MAIN NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM

Baada ya hizo mechi tatu au mbili, kocha bora kutoka nchini Kameruni, ameshatamka.. Namnukuu tena.. "..Simba itakua ni timu yenye safu kali sana ya ushambuliaji.". Sasa tuone Mnyama atakutana na "kitoweo" gani???

01.10.2016(Sat) Young Africans Vs Simba SC... MAIN NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM

Chonde Chonde "Wazee Wa Kimataifa" msikimbie uwanja.

Ingawa yale matatizo madogo madogo katika safu ya ushambuliaji bado yanafanyiwa kazi.. Hii haitawaepusha Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, Azam FC na Majimaji FC kupokea vipigo vizito vizito.

SIMBA SPORTS CLUB, NGUVU MOJA.
 
Mkuu Sembo wewe ulitakiwa uwe msemaji wa club, kama Masau Bwile team pinzani wanafungwa kwanza na msemaji wa club then team inaenda tu kumalizia uwanjani.
 
Sembo katika ubora wake
 
Mkuu Sembo wewe ulitakiwa uwe msemaji wa club, kama Masau Bwile team pinzani wanafungwa kwanza na msemaji wa club then team inaenda tu kumalizia uwanjani.

Shukrani sana Mkuu kwa heshima kubwa uliyonipatia.. Ila nadhani huku huku pananifaa.
 
Haha.. mkuu umeona lakini tamko kali la kocha bora toka "Kwa wanaojua" Kameruni?
Kocha bora gani aliyevurunda hapa hapa akiwa na Azam FC, huyu ana sifa kweli ya kuitwa kocha bora? Kama ndiyo hivyo, hii nchi ni ya "vipanga", niko tayari kuelekea Segerea kwa kauli yangu hii.
 
Kocha bora gani aliyevurunda hapa hapa akiwa na Azam FC, huyu ana sifa kweli ya kuitwa kocha bora? Kama ndiyo hivyo, hii nchi ni ya "vipanga", niko tayari kuelekea Segerea kwa kauli yangu hii.

Kwanini Omog ni bora?

1. Aliiwezesha AFC Leopard ya Congo Brazzaville kutwaa ubingwa wa CAF Confederation Cup katika msimu wa 2011/2012.. Ikumbukwe ni hili kombe Yanga SC wamelitia Taifa aibu kubwa sana msimu huu, na endapo Rais wa inchi hii angekua Kim Jong Un, makombora ya masafa marefu yangekua haki yenu.

2. Aliipa Azam FC ubingwa wa kwanza wa VPL Mei 2014 mbele ya "timu bora nchini' Simba SC na "wazee wa kimataifa" Yanga SC.

Sasa kwa baadhi ya hizo sifa hapo juu, Kwanini Omog asiwe bora??

Labda nikuume tu sikio.. Msimu huu Omog ataiwezesha Simba SC kubeba makombe matatu.
 
Kama kushiriki nane bora ya mashindano yaliyoanza na zaidi ya timu thelathini ni aibu kubwa sana, Je kutopata nafasi hata ya kuwemo kwenye hatua za awali za mashindano hayo ni fahari ya kiasi gani?
 
Kama kushiriki nane bora ya mashindano yaliyoanza na zaidi ya timu thelathini ni aibu kubwa sana, Je kutopata nafasi hata ya kuwemo kwenye hatua za awali za mashindano hayo ni fahari ya kiasi gani?

Ana aibu kubwa sana yule aliye thubutu kuingia kichwa kichwa kushiriki nane bora na kufeli.. kuliko yule aliyebaki nyumbani.
 
Ana aibu kubwa sana yule aliye thubutu kuingia kichwa kichwa kushiriki nane bora na kufeli.. kuliko yule aliyebaki nyumbani.
Mahaba yako kwa msimbazi huniacha hoi hiyo tarehe moja mjiandae tu kisaikolojia kipigo halali yenu ila salama lakini ndugu yangu?
 
Mahaba yako kwa msimbazi huniacha hoi hiyo tarehe moja mjiandae tu kisaikolojia kipigo halali yenu ila salama lakini ndugu yangu?

Kwangu ni Salama Mkuu.. ila hofu yangu kuu ni hiyo 01.10.2016 mda kama huu, wewe na wenzako sijui mtakua na hali gani, baada ya Mavugo na Abracadabra kuwavuruga kabisa masaa machache yaliyopita.
Eeeh Mola nijalie uzima, niwe shuhuda wa historia tunayoenda kuweka 01.10.2016.. pia mjalie Guasa Amboni na wenzake pumzi ya kutosha, ili wapate kuwasimulia watoto na wajukuu zao ukali Wa Simba SC ya msimu Wa 2016/2017.
 
Tuseme insha Allah panapo uzima sio mbali ila tatizo lako unajua kujificha kuna jamaa zangu kabila flan husema "unajua kujipoteza "yaani kuadimika msimu ulopita tumepiga nje ndani kwa idadi ile ile sasa msimu huu dose inaongezeka.
 
!
!
Yaani hawa wa kimataifa nina hasira nao sana. Tuwapige za fastafasta kama tano hivi ili watulie
 
!
!
Yaani hawa wa kimataifa nina hasira nao sana. Tuwapige za fastafasta kama tano hivi ili watulie

Mkuu hawa Msimu huu ni wetu.. Tunawapiga nje ndani, wachambuzi wa soka tunasema.. tunawapiga nyumbani.. tunawapiga ugenini.
 
Tuseme insha Allah panapo uzima sio mbali ila tatizo lako unajua kujificha kuna jamaa zangu kabila flan husema "unajua kujipoteza "yaani kuadimika msimu ulopita tumepiga nje ndani kwa idadi ile ile sasa msimu huu dose inaongezeka.

Usijali Mkuu.. Ila mnatakiwa mtambue kua Simba ya sasa ni SIMBA MABADILIKO.
 
Ana aibu kubwa sana yule aliye thubutu kuingia kichwa kichwa kushiriki nane bora na kufeli.. kuliko yule aliyebaki nyumbani.
Aliyeingia kichwakichwa ama aliyefuzu? Aliyebaki nyumbani au aliyeshindwa?
 
Kocha bora gani aliyevurunda hapa hapa akiwa na Azam FC, huyu ana sifa kweli ya kuitwa kocha bora? Kama ndiyo hivyo, hii nchi ni ya "vipanga", niko tayari kuelekea Segerea kwa kauli yangu hii.

Mkuu, Omog alivurunda alipokuwa Azam? Hebu kuwa serious kidogo, acha ushabiki

REKODI YA JOSEPH MARIUS OMOG ALIPOKUWA AZAM FC
Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Kirafiki, Azam Complex)
Azam FC 2-0 Spice Stars (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Tusker FC (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Ashanti United (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 2-0 Cloves Stars (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 2-3 KCC (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 4-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 1-0 Ferroviario de Beira (Kombe la Shirikisho)
Azam FC 0-2 Ferroviario de Beira (Kombe la Shirikisho)
Azam FC 2-2 Prisons (Ligi Kuu)
Azam FC 4-0 Ashanti United (Ligi Kuu)
Azam FC 4-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
Azam FC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu)
Azam FC 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
Azam FC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
Azam FC 2-1 Simba SC (Ligi Kuu)
Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Azam FC 2-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
Azam FC 1-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
Azam 0-0 Rayon (Kagame)
Azam 4-0 KMKM (Kagame)
Azam FC 2-2 Atlabara (Kagame)
Azam FC 4-1 Adama City (Kagame)
Azam FC 0-0 El Merreikh (3-4 pen, Kagame)
Azam FC 0-3 Yanga SC (Ngao ya Jamii)
Azam FC 3-1 Polisi (Ligi Kuu)
Azam FC 2-0 Ruvu Shoot (Ligi Kuu)
Azam FC 0-0 Prisons (Ligi Kuu)
Azam FC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu)
Azam FC 0-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
Azam FC 0-1 Ndanda FC (Ligi Kuu)
Azam FC 2-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
Azam FC 3-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki Chamazi usiku)
Azam FC 2-3 Sc Villa (Kirafiki, Nakivubo, Kampala)
Azam FC 0-1 URA (Kirafiki Kampala, Uganda)
Azam FC 3-0 Vipers (Kirafiki Kampala, Uganda)
Azam FC 0-2 KCCA (Kirafiki, Kampala, Uganda)
Azam FC 2-2 Yanga SC (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 2-2 KCCA (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
Azam FC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Mtende (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-1 Mtibwa Sugar (Azam ilitolewa kwa penalti 7-6 Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Stand United (Ligi Kuu)
Azam FC 3-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Azam FC 1-1 SImba SC (Ligi Kuu)
Azam FC 0-1 TP Mazembe (Kirafiki Lubumbashi)
Azam FC 2-2 ZESCO United (kirafiki Lubumbashi)
Azam FC 0-1 Don Bosco (kirafiki Lubumbashi)
Azam FC 2-2 Polisi Moro (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 2-0 El Merreikh (Ligi ya Mabingwa)
Azam FC 0-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Mlandizi)
Azam FC 0-0 Prisons (Ligi Kuu)
Azam FC 0-3 El Merreikh (Ligi ya Mabingwa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…