On a Serious Note: Waziri wa Sheria anapokuwa hajui Katiba!

mkuu... hivi ccm wanafanya makusudi au ni nini...? hivi hakuna mtu mwingine anayeweza kuwakilisha ccm katika masuala muhimu ya taifa pasipo Tambwe Hiza .... huu ni mzaha na dharau katika kuleta maendeleo ya nchi yetu

Hawajali kitu na ni dharau kubwa waliyonayo kwa watanzania ndo maana hawaoni umuhimu wa kuleta mtu makini,hatahivyo hao 'watu makini' ndio haohao walitengeneza huo muswada unapasua vichwa sasa..
 
Kuna mwelekeo wa kupanga kuhusisha ukosoaji wa mswada huu na Chadema. Serikali na ccm wanatumia mbinu hii kukwepa hoja zinazokosoa mswada huo.

Jana mkuu wa mkoa wa Dodoma alidai waliozuiwa nje ya bunge walikuwa ni wanafunzi wa udom ambao waliletwa na Chadema. Lakini siyo wote walikuwa wanafunzi na wanachama wa Chadema. Tambwe hiza alizomewa Karimjee wakadai ni Chadema. Lakini hata ccm walimzomea!

Kama nia ya serikali na ccm ni kuupitisha huo mswada ulivyo basi watatumia kisingizio hicho cha kijinga kuupitisha, wakidhani wanakomoa Chadema. Wakifanya hivyo watahatarisha Amani.

Kwanaza ni kweli kwamba huo mswada umekaa vibaya na mapungufu mengi mno. Pili, ni dharau kubwa sana kwa watz ambao siyo Chadema kuwaona kwamba hawana akili ya kuona yaliyomo kwenye huu mswada.

Tatu, basi hata kama mko sahihi kwamba ni wanachama wa Chadema pekee wenye akili na uwezo wa kuchambua uzuri na ubaya wa huu mswada, wao pia ni watz hivyo wana haki ya kusikilizwa.

Nne, kukataa hoja kwa sababu humpendi mtoa hoja ni kusokota sayansi mantiki. Shuhulikia hoja usimshuhulikie mtoa hoja!
 

Yaani CHADEMA wasiujadili huu muswada wakati wao ndio walioanzisha msisismko wa kudai katiba?
 
Kuna lawyer jana kaniboa sana STAR TV.......ati Marekani wana katiba ya miaka 250 na hawabadili katiba iweje sisi tubadili yetu yenye miaka 34 tu?

Fikra mgando, kwa mawazo hayo bado tuna safari ndefu inamaana kila tunachotakiwa kufanya lazima tuangalie Marekani wamefanya nini. huyo ni mwanasheria anayetegemewa kwa maoni na mchakato wa Katibu, watu kama hawa hawatakiwi kwenye maoni tena hawafai kwenye jamii yetu ya sasa
 

Mzee Mwanakijiji, kwa jinsi nilivyomuona Waziri Kombani, she was honest na genuine alipokuwa akitetea mamlaka ya rais, kwa vile ameona huo ndio uliokuwa mchakato wa marekebisho ya katiba. Amini usiamini, waziri anaamini wanachotaka Watanzania ni marekebisho na sio katiba mpya, ndio maana hata muswada wenyewe unasema mapitio. Ila pia ametoa room kuwa watazingatia maoni ya wengi hivyo naamini kuwa safari ya kuelekea kupata katiba mpya ndio imeanza.

Kitu kimoja ambacho Waziri Kombani hajakijua, ni tofauti ya kupata katiba mpya na kufanya mapitio ya katiba iliyopo. Kwa vile kuna notion kuwa Watanzania hawaijui hata katiba iliyopo, hivyo anaamini Watanzania hawajui wanataka nini, kama hujui unachotaka, basi ni lazima utapokea chochote unachopewa!. Tumepewa hii review na serikali ina amini tutapokea tuu kama kawaida yetu!.
 

Mkuu umenena! waziri-hana taaluma ya sheria, na katibu mkuu wake mwalimu!-piga picha!!!
 
Wakati wakitumia NGUVU zao zote kupitisha ujinga wao...wananchi walio wengi walikua wakitumia NGUVU zao zote kuhakikisha hawaelewi na wanapoteza nafasi zao next election....The harder they r pushin it,the easy we understand hw much garbage is contained in the BILL
 
yaani acha tuu...hata Robert Manumba aliulizwa kwamba katiba ya tanzania inasemaje kuhusu madaraka ya jeshi la polisi ..akajibu kuwa yeye sio mtaalam wa katiba .... najiuliza katiba hii nani anatakiwa aijue...?

khaaa!
Inabidi kuwe na somo la katiba kuanzia form one.
 
I am of the same opinion as you. These people are not seeing and putting things in perspective. I dare say that their perspective is very myopic and self-destructive. This is what I had posted earlier:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/124760-katiba-mpya-chini-ya-saa-100-a.html
 
angekuwa ni mama yangu, ningemsihi ajiuzulu, na ningeweza hata kugoma kula mpaka ajiuzulu, si kwa sababu namchukuia ila kwa sababu nawapenda watanzania.
 
Mhe Kombani, amekiri ni kweli rais amepewa madaraka makubwa sana kwenye muswada huo, lakini akasema madaraka hayo, yametokana na katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977.

Nashindwa kuamini macho yangu yanayosoma haya; anakiri alafu anafanya the opposite kwenye jambo analotakiwa kulifanya sasa tumsaidieje? Tumsaidie kulia kwasababu yuko helpless ama?
 

Kila siku ya dunia ni mpya haijawahi kutokea moja ikafanana na nyingine na hata sura ya mwanadamu hubadilika kila saa japo slowly to be seen with visible eyes kinacho ni shangaza ni upofu wa serikali ya CCM kwenye vitu so obvious kama hivi. What I can read is si kwamba hawafahamu no ila mslahi yao ni mazito kuliko ukweli wanaouona ndiyo maana wana fight to the last drop. Na sisi tunasema this time no way out kama mbaya na acha iwe!
 
Huyu mama aombe kubadilishwa wizara........hii haiwezi.......I wish Sitta was in place

Hatuna huo uungwana ndugu sisi huwa ni all knowing omnipresent and omniscience kama Miungu vile na kukosolewa kwetu ni dharau na si uungwana. Lakini hata kama mtu hajui sheria si anaowataalamu wakutosha tu hapo wizarani? Amefanya home work yake kweli kabla ya kuja public au aliona hahitaji ushauri wa kitaalamu? Ndiyo kawaida yetu sisi na wanasiasa wetu wanataka kuwa wanasiasa, watawala, wataalamu na vilevile walaji wa kila jema katika nchi ya watu milioni 40 na ushehe. Vyakula vingine sumu hilo hawajui; ulafi pia unamadhara yake.
 
Kuna lawyer jana kaniboa sana STAR TV.......ati Marekani wana katiba ya miaka 250 na hawabadili katiba iweje sisi tubadili yetu yenye miaka 34 tu?

Unaongelea hawa ma-lawyer wanaouza rasilimali zetu kwa kutengeneza mikataba ya kizushi? Give a break pls!
 


Ni dhahir kwamba hii post anayotumikia huyu mama ni kubwa kuliko uwezo wake. Wanawake tunaweza, lakini kwa hili tukubali kwamba huyu mama kachemsha!
 
Kuna lawyer jana kaniboa sana STAR TV.......ati Marekani wana katiba ya miaka 250 na hawabadili katiba iweje sisi tubadili yetu yenye miaka 34 tu?

Pole ndugu,

Huyu mwanasheria pengine ni mgonjwa, mwache. Yaani anajaribu kufananisha katiba ya USA na ya Tz, basi si haba hajui mavi hunuka!
 
Huyo Kombani, kapwaya sana katika hiyo Wizara. Unashindwa kubaini ni vigezo gani huyo Kikwete alitumia kuwaweka watu kama hao katika wizara nyeti hivyo. Ndio maana wenye akili wanaposema Kikwete ni zero hawakosei
 

Mkuu;
Japo simtetei huyo mama , nafikiri hamkuelewana kwa sababu wewe ulitaka aongelee katiba mpya wakati wao wana mswaada wa mapitio ya katiba kukuu. Nafikiri hicho wengi ndo kinawachanganya.

Inabidi wachangiaji wachangie kwa mwelekeo wa marekebisho ya katiba.Ama wakatae kuchangia wakihitaji mswaada wa katiba mpya.Saizi unapochangia ktk mswaada uliopo inabidi ujikite na kuelekeza akili yako unachangia mswaada wa marekbisho ya katiba.
 
Kuna lawyer jana kaniboa sana STAR TV.......ati Marekani wana katiba ya miaka 250 na hawabadili katiba iweje sisi tubadili yetu yenye miaka 34 tu?

ebana dah! Hebu mpige konzi..ameboa vbaya.
 

Mkuu Pasco, umemvua huyo waziri nguo mchana kweupe! That is what at least I can say....you have undone her naked! Period

Hatuwezi kuendelea kuwa na vilaza wa namna hii kila kukicha alafu tuvumilie....go go Pascal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…