Naona ulitaka kuwapaisha na si kutafuta hicho unachokitafuta!! kama ni nani is who's in town corporate talk basi dhahiri umeshawataja!!!Kama wadau wengine walivuokwisha sema kuna vigezo. Japo waweza kuwaweka kwenye mizania moja lakini ukizingatia soko la bidhaa husika.
Mpaka sasa wataalamu wa masoko Tanzania ni taaluma ambayo bado inaonekana kama ipo ipo tu, lakini kwa ujumla wake ndiyo taaluma inayosababisha walaji waamue kununua ama kutokunua bidhaa ama huduma husika kwa mujibu wa mapokeo yaliyotengenezwa na wanataaluma hiyo.
Mimi binafsi zamani nilijua Afisa masoko ni mfanyakazi wa umma, kama vile mashirika ya umma kama BIMA, RTC, Vyama vya ushirika na ofsi za biashara za wilaya.Na utendaji wao wa zama zile hakika ulikuwa ni ule tusiona leo!!Zaidi kama ulikuwa unafahamiana na mmoja wapo basi utasikia ameenda ulaya, lakini utendaji wa hapa ndani zaidi ya kumuona afisa bishara na masoko akijaza form za biashara hakuna jingine.
Ujio wa Private companiesa na Corporate companies kama mobile phone network provide, Beer Industries, Soda umeleta aina mpya ya kizazi kilichosoma biashara na hasa kwa Tanzania zao kubwa la marketing ukiacha elimu ya Nje ni chuo cha biashara cha CBE.Japo vyuo kama Mzumbe na UDSM nao kupitia mifumo yao wana wanataaluma wa fani hiyo lakini wengi kwa mfano UDSM wanatokana na Bcom na Mzumbe wao ndio wameanzisha kwa sasa Degree ya Marketing.
Kwa watanzania walio wengi hawajui umuhimu wa fani hii ya masoko na hivyo hata mwenendo mzima wa taaluma hii kwa Tanzania bado haujapata kizazi cha kuifanya watanzania waifahamu Taaluma hii kwa mapana yake.Watanzania hawajui kuwa haya mabango, wanayoyaona mabarabarani, matangazo wanayosikia kwenye radio au television , ni kazi iliyobuniwa na kutengenezwa na taaluma hiyo.Watanzania walio wengi hawana ufahamu japo kuwa mpaka anavutika kununua kitu ni kazi ya mtu wa masoko