Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,587
Jumamosi juzi alichukua 1.5mn za u MC akiahidi atafanya pale Danken na tena kumbe akachukua pesa zingine kuwa atahudumu kama MC kule Picolo!
Siku yenyewe alituma mtu amshike pale Danken lakini wenye harusi wakamkataa wakataka mpaka wamuone mwenyewe basi ndio akaja fasta.
Ilipofika wakati wa chakula wale wa sherehe nyingine ya kule Picolo nao wakaja kwani walikuwa wameshajua yuko Danken baada yakumtafuta kwa muda.
Bahati nzuri walipofika Danken alikuwa tipped akatoroka ila waliomfuata wakajua na kumfukuza mpaka wakamkamata nje karibu na kwa Mzee Mwinyi na wakaanza kumpiga na badae wakamrudisha Picolo na kumfungia kwenye chumba huku wakiendelea na harusi yao pamoja na kumpa kichapo kingine na mwishowe walimsimamia mpaka amewarudishia pesa yao!
Wale wa Danken nao bado wanadai sababu aliwakimbia hakumaliza harusi yao!
Kwa hiyo nimeona niwaonye ndugu kwani huyu ndiye aliyekuwepo kwenye send off ya Nicole Kundi wa Evarist Mashishi na Anna Masta pale Danken jumanne iliyopita msije mkatapeliwa kwani hii inaonyesha ni tapeli haswa!
Sent using Jamii Forums mobile app