Ona hapa Tabia zinazokera na Uchafu wa watu wanaokaa au kupanga Nyumba Chumba Single Self

Ona hapa Tabia zinazokera na Uchafu wa watu wanaokaa au kupanga Nyumba Chumba Single Self

Manfyantona

Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
13
Reaction score
20
Chumba single Self ni chumba kimoja chenye choo ndani yake. Kwa mpangaji wa nyumba au mtu alowahi kupanga vyumba atakuwa wanamielewa sawa sawa.

Wapangaji wengi hapa mjini wanatafuta vyumba self. Nikimanisha either Single self (Chumba kimoja na choo ndani) ama double Self ( Chumba na sebule vyenye choo ndani)

Baada ya kuonekana wateja wengi hasa vijana kuhitaji vyumba vya self, hata na maboss yaani wa miliki wa nyumba nao wamekuwa wakijenga nyumba za kupanga zenye vyoo ndani na wengine kabisa kujaribu kubadilisha vyumba kuwa vya self ili tu kukidhi haja ya wateja.

Inaelezwa kuwa , watu hupenda vyumba self kwa kuepuka maradhi ya kuambukiza kama UTI etc, kuepuka uchafu ukichukulia kuwa choo cha public kinavyokuwa hovyo kutokana na kuwa wapangaji wote hawawezi kuwa na nidhamu ya usafi chooni .

Pia watu huepuka makelele ya kupangiana zamu za kudeki ( kufanya usafi chooni) na hii huwa inaleta makelele na sintofahamu na huleta kero kwani apangaji wengine hawana time na usafi hasa mabachelor wanaume huwa pasua kichwa.

Kwa maana hiyo basi, watu wengi hupenda kupanga chumba au vyumba self kuepuka usumbufu huo. Na ukweli ni kwamba hata ambao wanakaa vyumba visivyo na vyoo ndani hawapendi. Ni kwamba tu hali ya maisha haiwaruhusu ndio ile kusema 'mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake'. Hivo basi nao wanatamani kuishi vyumba self. Kama kuna raha kuishi chumba self!!!

Baada ya utangulizi huo, acha sasa nijikite kwenye maada yenyewe isemayo: " Ona hapa Tabia zinazokera na Uchafu wa watu wanaokaa au kupanga Nyumba Chumba Single Self".Na bila kupoteza muda, hizi hapa tabia hizo :

A) Kuchota maji ya matumizi ya ndani chooni.

Tabia inayokera sana hasa kwa ambao hatujazoea na pengine pale unapomtembelea rafiki au shosti wako, ni pale utakapomuona anaingia chuooni ( wao wanaotaka eti SHOW ROOM) kuteka maji ya kutumia kwa mapishi huko chooni.

Utashangaa kumuona anaingia na bakuli na kuteka maji kule na kuyaleta kwa matumizi. Wao hawana shida kwani wanajiamini na usafi wao na jinsi huko chooni kulivo nadhifu.

Wengine hata maji ya kunywa wanatumia hayo hayo ya chooni. Wanaona uvivu wa kutoka nje uani na kuteka maji na kushortcut kuingia chooni kuchukuwa maji ya kunywa.

Inakera pale mgeni ambaye hajazoea kutumia maji ya bafuni atakapopewa maji hayo. Wengine huwa wanakataa kuyanywa huku wakisema hawana kiu ila kwa ukweli wanaona ni uchafu tuu kwani hawaamini mazingira ya huko chooni hata kama ni pasafi kiaje!

B) Kuoshea vyombo chooni

Tabia hii nayo imeota mizizi sana kwa wanaokaa self rooms. Hasa kwa nyakati za usiku na hasa hasa kama mvua ina nyesha au imeonyesha nje kuna matope wao huchukua fursa ya kwenda na vyombo Kuoshea huko wanakopaita show room.

Ndio maana utakuta mtu anaekaa chumba au vyumba na choo ndani si mtumiaji wa mara kwa mara wa bomba lililoko uani! Wao ni mara chache tu wao kila kitu ni ndani kwa ndani!

C) Kumwaga maji yalotumika (yenye ukoko) chooni

Hapo sasa, wengi wanaokaa nyumba zenye vyoo ndani humwaga maji yenye ukoko au makombo madogo madogo chooni.

Kwa ujumla maji yalotumiwa kwa mfano Kuoshea vitu; kunawia nk hutupwa chooni! Hawa satu ni wa wavivu vya hataree! Yaani ni wavivu e mbaya! Wanaona taabu sana kutoka nje na kumwaga hayo maji! Ila wengine tuonavyo huo nao ni uchafu maana tunaamini kwamba unapomwaga maji chooni kuna maji machafu ya chooni yatarukia kwenye hicho chombo kwani lazima uelekezee maji mdomoni chini kwa sink.

D) Kufulia nguo chooni

Watu hawa hupenda na kufurahia kufulia nguo zao chooni hasa hasa Mida ya usiku. Utakuta hasubuhi mtu kaanika nguo nyingi tu na kamba karibia tatu zimejaa ambazo jioni yake hazikuwepo na mtu huyo hayupo kasepa zake kazini kwake au kwa lishe mishe zake😀😀. Na hata hapo usiku hamkusikia purukushani zozote za ufuaji na umwagaji maji.

Hii nayo imekuwa ndogo ugomvi mkubwa baina yao na wapangaji wengine na Mmiliki wa nyumba kwa ujumla. Maana kitendo cha kufulia nguo ndani ( chooni) linapelekea Shimo la choo kujaa haraka mra katika mara hivo kuingiza hasara wengine kuvuta maji taka hayo mara kwa mara.

Ni kweli kuwa ni ngumu kwao kufulia nguo chooni na wasimwage maji hayo huko! Na kwa kufanya hivo wanajaza shimo la choo bure bila sababu babu kwa kutoamua kufuria nguo zao nje publically!

My Takes

Kuchezea chezea sana chooni, sehemu tunayoamini kuwa si mahala salama kwa afya ya binadamu ikichukuliwa kuwa ni sehemu kunakowekwa taka chafu zinazotoka mwilini mwetu si jambo zuri.

Hata kama unakuwa na usafi wa aina gani bado chooni hubakia kuitwa chooni. Mahali hapa, si sehemu pa kuteka maji ya kunywa maana ile koko ya bomba la pale nalo si salama hata kama liko salama ila kutokana na kwamba liko sehemu si salama nalo hukosa uhalali huo.

Kuoshea vyombo hasa vikombe na glass chooni nalo si jambo zuri kwa afya. Ni kujitakia magonjwa tu.

Ndoo maana utakuta mtu anakaa nyumba nzuri tu ila anakwambia anaumwa tumbo, anaharisha, nk. Hii yote ni kutokana na kutumia sana maji ya chooni au kuwa na tabia ya namna hii.

Kufulia nguo chooni nalo pia ni kujiingizia cost au kusababishia cost wengine pasipoti na sababu. Kufanya hivi ni kujighalimu mara mbili kwa maana ya gaharama ya bili ya maji na gharama a ya kuvuta maji choo🤣🤣🤣 . Si poa jamani

Mtu ni Afya.
 

Attachments

  • IMG_20200115_202359_1.jpg
    IMG_20200115_202359_1.jpg
    95.3 KB · Views: 43
MAISHA HAYANA KANUNI MAALUMU KILA MMOJA NA YAKE
 
Vyoo vyao vikiziba wasimsumbue mwenye nyumba, wakazibue wenyewe.
 
Mkuu unaona kinyaa kuchota maji chooni wakati unaingia humo na mdomo wako na pua zako..laiti ingekuwa huingii huko au ingekuwa unaingia na PPEningeona umeandikwa point
 
Naishi nao mademu hapa wanaleta mtu wa kufua nguo wakati mimi najifulia. Life is good
 
Nafikiri kinyaa cha chooni kilitokana na vile vyoo vyetu uswahilini hasa ivyo vya jumuiya. Nadharia hii imekuja hadi kwenye vyoo vya kisasa yaan taswira ya neno CHOO bado ni mahali pasipo salama kiafya.

Lakini vyoo vya kisasa vipo nadhifu hata waweza kula hukohuko na tv ukaangalia hukohukobpia.Jambo hili lafaa ujifanyie mwenyewe uliyerizika na mazingira yako hayo. Kitendo cha kumfanyia mgeni kisha akajua kwamba choo kimeambatana na bomba basi hujawa na kinyaa hivyo sio vyema kumfanyia mgeni wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika ukweli (kwa baadhi ya watu wako hivyo).
Ila ukweli huo hauna lolote la maana.
Ni sawa na serikali kununua ndege, ni jambo jema na la heri kabisa, ila kwa upande wangu halina maana.
Naomba nieleweke vizuri!
 
Mtoa mada nakubaliana na ww ..na hii tabia wanawake ndio wanayo Sana Yaan Wana vitabia vya uvivu uvivu Sana halafu .. ukawaona nje huwezi amini ushenzi wanaoufanya wakiwa peke yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati nilikua naishi kwenye nyumba ya kupanga na vyoo ni vya nje tena mbali kidogo, mbaya zaidi nyumba haina hata uzio. Ukiwa unaelekea chooni na ndoo yako mtaa mzima unajua. Balaa uwe umeleta manzi siku hiyo mtachoreka mpaka basi, hasa ukute mida hiyo akina mama wamekaa kaa huko nje.... mtageuka mada.
 
Ndiyo maana nyumba zina tengwa choo, jiko wengine na bafu tofauti.
Kiafya ukitoka chooni nawa mikono hata kiwe choo cha 5* Bado ni choo.
 
Back
Top Bottom