Ona katiba mpya ya Kenya inavyowatesa Wakenya

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569

Kamwe fahari wawili hawawezi kaa zizi moja. Katiba yao mpya iliweka fahari zaidi ya watatu katika zizi moja. Ona sasa mambo ya utawala wa nchi unavyokuwa mgumu.
 
Inawatesa kwa vipi? Kwani hapa hatuteseki? Kwani hapa tuna bunge? kwani hapa tuna mahakama?
 
Migongano ya kiutawala. Nchi ina mafahari zaidi ya moja.

Kwanini kwenye chama chenu mna fahari mmoja tu anayeitwa Mbowe? Akisema kushoto geuka wote mnageuka kushoto. Akisema lockdown wote mna lockdown?

Kwa nini kwenye familia yako ni wewe tu ndiye fahari pekee? Mke wako na watoto wako inabidi watii maamuzi yako? Mke wako na watoto wako ni washauri wako tu na hulazimiki kukubali ushauri wao. Mwenye uamuzi wa mwisho ni wewe.

Au wewe na chama chako ni kambale ambao kila mmoja ana sharubu?
 
Katiba ni miongoni mwa vitu vinapata shida sana kwa nchi za kiafrika.
 
Kamwe fahari wawili hawawezi kaa zizi moja. Katiba yao mpya iliweka fahari zaidi ya watatu katika zizi moja. Ona sasa mambo ya utawala wa nchi unavyokuwa mgumu.

Hivi ndivyo Mihimili ya Bunge, Dola na Mahakama inatakiwa iwe huru kuhoji uhalali wa mhimili mwingine kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Siyo kama Tanzania ambapo mhimili wa Dola umeimeza mhimili wa Bunge na Mahakama matokeo yake hawawezi kuikosoa dola yaani serikali ijirekebishe.

Utawala bora kuna kitu kinaitwa check & balance yaani Mihimili yote inachunguzana kama inatekeleza wajibu wake kwa kufuata katiba nia njema ni uwajibikaji kwa kufuata utawala wa sheria uliokubaliwa na kutamkwa ndani ya katiba.
 
Kulinganisha Katiba ya Kenya na hii taka taka ya Tz y kikoloni ni uwendawazimu . thats was the last thing I wanted to hear.
Wewe ndio mwendawazimu, lengo la katiba ni kuboresha maisha ya wananchi kiuchumi, kisiasa na Kijamii, na kupunguza migogoro na dhuluma miongoni mwa wananchi, katika hayo yote, lipi lililoboreshwa kwa kupatikana kwa katiba mpya Kenya?, hali ndio imezidi kuwa mbaya kiasi wanataka tena kuibadilisha.
 
Hivi ndivyo Mihimili ya Bunge, Dola na Mahakama inatakiwa iwe huru kuhoji uhalali wa mhimili mwingine kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Siyo kama Tanzania ambapo mhimili wa Dola umeimeza mhimili wa Bunge na Mahakama matokeo yake hawawezi kuikosoa dola yaani serikali ijirekebishe.

Utawala bora kuna kitu kinaitwa check & balance yaani Mihimili yote inachunguzana kama inatekeleza wajibu wake kwa kufuata katiba nia njema ni uwajibikaji kwa kufuata utawala wa sheria uliokubaliwa na kutamkwa ndani ya katiba.
Tanzania pamoja na kuwa na hiyo mihimili mitatu, kuna mkuu wa nchi mmoja. Mkuu wa nchi huyu huchaguliwa na wananchi wote kila baada ya miaka 5. Hivyo yuko pale kwa niaba ya wananchi wote kuendesha nchi yao. Hakuna mtu mwingine ye yote kwenye utumishi wa umma anayechaguliwa na wananchi wote. Yeye ndiye kwa niaba ya wananchi wote anaowawakilisha ndiye huchagua na kuteua kiongozi wa mhimili wa mahakama. Yeye kwa niaba ya wananchi ndiye amiri mkuu wa majeshi yote ya nchi.
 
Hivi ndivyo Mihimili ya Bunge, Dola na Mahakama inatakiwa iwe huru kuhoji uhalali wa mhimili mwingine kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Siyo kama Tanzania ambapo mhimili wa Dola umeimeza mhimili wa Bunge na Mahakama matokeo yake hawawezi kuikosoa dola yaani serikali ijirekebishe.

Utawala bora kuna kitu kinaitwa check & balance yaani Mihimili yote inachunguzana kama inatekeleza wajibu wake kwa kufuata katiba nia njema ni uwajibikaji kwa kufuata utawala wa sheria uliokubaliwa na kutamkwa ndani ya katiba.
Sikiliza kwa makini hii video, bila shaka utajua kinachoendelea huko Kenya
 
Migongano ya kiutawala. Nchi ina mafahari zaidi ya moja.

Kwanini kwenye chama chenu mna fahari mmoja tu anayeitwa Mbowe? Akisema kushoto geuka wote mnageuka kushoto. Akisema lockdown wote mna lockdown?

Kwa nini kwenye familia yako ni wewe tu ndiye fahari pekee? Mke wako na watoto wako inabidi watii maamuzi yako? Mke wako na watoto wako ni washauri wako tu na hulazimiki kukubali ushauri wao. Mwenye uamuzi wa mwisho ni wewe.

Au wewe na chama chako ni kambale ambao kila mmoja ana sharubu?
Akilala akiamka anatangaza tu kwa mihemko yake furani sio mbunge bc woote wanamuunga mkono ,inawezekana Jana usiku wamegombea demu tu asubuihi anaamuua kumfuta ubunge halafu ndio ashike ncho itakua nchi au wendawazimu
 
Back
Top Bottom