SoC02 Ona Mtazamo Hasi Unavyotafuna Siasa na Maendeleo ya Mwafrika

SoC02 Ona Mtazamo Hasi Unavyotafuna Siasa na Maendeleo ya Mwafrika

Stories of Change - 2022 Competition

Ventas Malack

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
5
Reaction score
1
Mtazamo ndiyo kitu ambacho humjenga mtu na kumpa tafsiri ya kitu chochote kile anachofanya, alichonacho, namna ya maisha na hata ufikiri juu ya maswala mengine yanayomzunguka. Afrika na watu wake huonekana duni mno kuliko watu wengine duniani ambapo kutokana na hili inafanya kusimama kwa uchumi na kukosa maendeleo katika bara hili.

Huu ni mtazamo ambao unaitafuna Afrika na watu wake ambapo hii inawafanya waafrika kujiona kuwa ni watu wasio na thamani na siyo binadamu wa kawaida kama watu wengine.

Kabla ya karne ya 15 historia inaonesha kulikuwa na usawa maendeleo duniani kote na huenda watu wa Afrika walikuwa mbele Zaidi kuliko watu wengine wa duniani kutokana na histori zinazozuka wakati huu juu ya Afrika na ugunduzi wake juu ya mambo mengi.

Waafrika walianza kuvifanya vitu mbalimbali kabla ya watu wengine wa duniani ikiwemo chuo cha kwanza duniani kilikuwa Timbuktu, pia kulikuwa na mahesabu mapema Zaidi ya wengine na hata teknolojia ya ujenzi ya Afrika ilikuwa juu sana Ushahidi moja wapo ni mapiramidi yaliyopo Misri na Sudani, licha ya hivyo pia Tajiri zaidi duniani anayeshikilia rekodi ni aliyekuwa mfalme wa Mansa Musa wa Mali aliyekadiliwa kua na Zaidi ya dola bilioni 400.

Si hayo tu yanayoonesha kuwa mwafrika alikuwa na maendeleo lakini je ni nini kilichomfanya Mwafrika kurudi nyuma kimaendeleo na kuwa chini ya mataifa na watu wa sehemu zingine?

Moja ya wanahistoria maarufu duniani Walter Rodney aliandika kitabu kiitwacho “How European underdeveloped Africa ” ambapo humu yeye anakiri kuwa unyonyaji na ukoloni ndivyo vilivyo mtafuna mwafrika na kumdidimiza kimaendeleo.

Walter Rodney anaeleza kuwa kuanzia karne ya 15 ulaya ilianza kupungukiwa malighafi hali iliyopelekea kuanza kuzitafut katika maeneo mengine ikiwemo Afrika na hii Ikapelekea utumwa na ukoloni vitu vilivyomdidimiza muafrika na kumpotezea kasi yake ya maendeleo.

Watu wa Ulaya walitumia mitazamo na siasa kuwatawa waafrika na kupelekea kushuka kwa uchumi na maendeleo kwa kiasi kikubwa walitumia njia mbalimbali ikiwemo dini na elimu ili kubadili mtazamo wa Afrika juu ya utamaduni na utawala hali iliyopelekea waafrika kuwaona wazungu ni bora Zaidi kuna wengine huwaona ni kama malaika wana uwezo wa juu Zaidi wa kufikiri jambo ambalo si la kweli.

Wazungu walitumia njia hiyo ili kuweza kumtawala mwafrika hali ambayo hadi sasa ina mgharimu mwafrika na kumfanya asiendelee na kubaki kuburutwa na kutawaliwa na wazungu pi kunyonywa ambapo kwa sasa wameleta mbinu mbadala ya kwa kutawala kupitia ukoloni mamboleo.

Ili kutoka hapa tulipo inatakiwa kuondosha mtazamo hu una kuuheshimu uafrika kuzidi kuamini kuwa wazungu ni bora kutafanya kuwa tegemezi juu yao na kushindwa kuwa na maamuzi yetu kuhusu mambo mbalimbali yanayotuhusu ikiwemo uchumi na siasa hali itayofanya Afrika kuwa palepale miaka nenda rudi kwakuwa ujasiri wa kuendele na kujitegema unatutoka kwa kuamini bila mzungu hatuwezi fanikiwa.

Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mifumo yetu mingi ambayo hutuharibu kimtazamo juu ya thamani ya uafrika na kuwatukuza wazungu ikiwemo mfumo wa elimu, lugha, teknolojia, utamaduni na siasa ambapo mengi katika mifumo hii hutufanya kuona kuwa waafrika tumeendelea baada ya kutawaliwa na hatuwezi simama bila ya wazungu kitu ambacho si kweli kwa kuwa wazungu wanatumia mbinu hiyo kutuharibu kimtazamo kwa kuwa wanahofia mwafrika akipata mwanga atakuwa hatari kwao.

Ukiwa una ufikiri ulio sawa lazima ujiulize kuwa kwanini kila historia inawatukuza wazungu na vyombo vya habari vya kimataifa vinaonesha matukio mabya tu yanayotokea Afrika je ni kweli Afrika ni maeneo yote yana matatizo hakuna vitu vizuri?

Jukumu ni letu kujikwamua kutoka kwenye kifungo hicho cha fikra maana hatma ya maendeleo ya waafrika ipo mikononi mwa waafrika kujitegemea ni siri ya mabadiliko kuna mifumo ikibadilishwa tu ndani ya muda mfupi kitatokea kizazi ambacho kitaiinua Afrika na kuipa hadhi yake iliyoipoteza kwa kuwa mifumo hiyo iliandaliwa Madhubuti kuharibu fikra za mwafrika ili atawaliwe na kunyonywa Zaidi.

by Ventas Malack

Great-Pyramid-of-Giza-in-Egypt%20(1).jpg
View attachment 2349892View attachment 2349891View attachment 2349890
 
Upvote 2
Back
Top Bottom