Ona sasa De Agosto wameiponza Simba

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kama kuna timu imewaingiza mkenge Simba basi ni wale wa Angola. Baada ya kuwatoa De Agosto na kutinga makundi, Simba wameongea saana mtaani na kujiamini kupitiliza.

Msemaji wao akawavimbisha vichwa + Chama na Phiri wakajiona mi kama Real Madrid. Walitupuuza tulipowaambia kwenye CAF Champions Seague walipangiwa vibonde walipinga wakatukana sana.

Sasa basi hayo mambo yote na ukiongezea kubahatisha draw na Yanga na sifa za wachambuzi wetu ,vikawapa imani kuwa wao kweli ni wa level nyingine na kwamba wao hapa Tanzania ni bora kuliko yeyote, lakini ukweli unakuja kuupata kwenye takwimu.

Simba sasa wanaenda kaa nafasi ya tatu kwenye msimamo, na ukiangalia takwimu Azam kamwacha Simba mbali na Yanga ki takwimu na kiutendaji yupo imara zaidi ya Azam. Hivyo kwa mwendelezo huu sioni msimamo ukibadilika hivi karibuni, zaidi Simba ataendelea kuporomoka katika ligi na makundi hivyo watafukuzana humo na wasipokua makini hiyo namba tatu wataigombea na Singida na KMC!

Poleni sana ndugu zetu. Mtibwa huyo anakuja na mnamjua. Nimalizie kwa kusisitiza aliyemponza mnyama ni De Agosto.
 
Kinachowapoza simba ni upumbavu wa mashabiki wao hii mijamaa inaongea utadhani wao walishawahi kuchukua kikombe chochote cha CAF,sasa mabosi wakiona mashabiki walivyo na vibe basi nao wanavimba vichwa na kuona simba ni timu kubwa sana Africa hii,,,na ngoja utaona kuna maajabu yanakuja kwenye makundi
 
Kama kuna timu imewaingiza mkenge Simba basi ni wale wa Angola. Baada ya kuwatoa De Agosto na kutinga makundi, Simba wameongea saana mtaani na kujiamini kupitiliza.
Tulipokuwa tunawaambia kuwa wamekutana na Ihefu ya angola walimwaga mapovu kama yote, Hamasa ni jambo moja na kuwa na timu bora ni jambo jingine Kocha mgunda ni mhamasishaji mzuri ndio maana timu inaonekana inaperform mda mwingine lakini simba wanayo timu ya kawaida sana ukitoa wachezaji 11 wanaoanza pale benchi akuna mchezaji ambae ni tishio utawakuta wachezaji dizaini ya kina nyoni na boko ni tofauti na yanga
 
Yanga ni kubwa kuliko al hilal. HAHAHAHAHAHAHAAAAAAHAHAHAHA.
 
Kweli na simba angecheza na zalan fc kwenye Caf champions league simba angekufa nyingi sana maana wale zalan lile kabumbu wanalotandaza ni kama Barcelona ya ile ya Guardiola
 
Na ile zalan tuiteje maji maji fc au friends rangers ila huu ushabiki nataka nifanye nistaafu kushabikia mpira maana kwenye ushabiki hata mtu mwenye phd anaongea utumbo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…