Ondoa tatizo la umeme mdogo katika makazi yako au eneo lako la kibiashara

Ondoa tatizo la umeme mdogo katika makazi yako au eneo lako la kibiashara

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,637
Kutokana na kuongezeka kwa makazi ya watu huku ukubwa wa transformer za Tanesco zikibaki zilezile,kumepelekea maeneo mengi ambayo miji yake inakuwa kukabiliwa na tatizo la umeme mdogo hasa kipindi cha high consuption.

Vifaa kama vile AC, fridge,freezer,motor na mashine za kufulia zimekuwa zikishindwa kufanya kazi katika maneo yenye tatizo la umeme mdogo.

Hali hii imefanya watu wengi kuto furahia huduma ya umeme kutokana na low voltage.

Nimekuwa nikiunda mashine mbali mbali ambazo zinatumika kuondoa tatizo hili la umeme kwa muda mrefu sasa.

Hii ni aina nyingine ya VOLTAGE BOOSTER ambayo nimeiunda kwa kutumia technolojia ya PUSH-PULL three stage

Ambayo inaongeza umeme katika stage tatu ili kuweza kukabiliana na maeneo yenye extreme low voltage.

Kitu kingine kizuri kwa mfumo huu wa PUSH-PULL ni kwamba unaweza kuunda voltage booster yenye ukubwa zaidi ya kilo watt 100

Unaweza kutumia kifaa hiki kwa ajili ya kuendesha
-motor za visima vya mafuta kwa idadi yoyote ile.

-Kuendesha vyumba vya idadi yoyote ile vyenye AC

-Kwa ajili ya matumizi ya nyumba ya kuishi yenye vitu vizito kama vile AC,Motor za visima vya maji,mashine za kufulia,heater za maji n.k

Mashine hii ni ya nne ya mfumo wa PUSH-PULL kuweza kuunda

kati ya mashine Arobaini na mbili tulizowahi kuunda za kupambana na tatizo la low voltage.

Mashine za PUSH -PULL ambazo tumewahi kuziunda ni za kilo watt 8,kilo watt 24,kilo watt 52 hii ya kwenye picha ina kilo watt 12

Switching voltage yake ni Automatic sawa na mashine za mwanzo ambayo ni hii hapa katika mchoro:-

111111111111-png.199409



Tunatumia tekinolojia nzuri ya security kwa ajili ya kuilinda mashine yenyewe na mtumiaji.

12Kilowatt hii hapa chini:-

Hapa ikiwa eneo la matengenezo

tra-jpg.199411



Hapa imefungwa katika nyumba ya mteja


tr-jpg.199412


Muundo wa booster nyingine ni huu hapa

img_20130601_030304-jpg.707825


ytt-jpg.707828


mes-jpg.707826


mes6-jpg.707827
 

Attachments

  • IMG_20130601_030304.jpg
    IMG_20130601_030304.jpg
    162.2 KB · Views: 610
  • mes.JPG
    mes.JPG
    65.7 KB · Views: 561
  • mes6.JPG
    mes6.JPG
    106.8 KB · Views: 555
  • ytt.jpg
    ytt.jpg
    71.3 KB · Views: 631
mkuu hongera! naomba cont zako hiyo tcnlogy nime ipenda sana, huwa natumia stabilizer kwenye kaz ya kuzalisha umeme wa upepo ila ufanisi wake cyo mzri kabisa. namba yngu ni 0657139511
 
nyinyi ndio mnaosababisha wengine tupate low umeme eeh? mfano ni kama vile wale wanaotumia mashine za kupampu maji wengine tunapata maji kidogo!
 
nyinyi ndio mnaosababisha wengine tupate low umeme eeh? mfano ni kama vile wale wanaotumia mashine za kupampu maji wengine tunapata maji kidogo!

Mkuu mbona kama hujaeleweka vizuri!,Mashine tajwa hapo juu ni kwa ajili ya ku boot umeme sasa na sababu unazozitoa wapi na wapi?
 
Mkuu umesema inaboost voltage
Vipi kuhsu current?
Kama mahitaji ya vifaa vya umeme ni 230 voltage
Wewe unaboost voltage ifike ngapi?
Mahitaji ya vifaa vya umeme (load) ni current sio voltage
 
Mkuu umesema inaboost voltage
Vipi kuhsu current?
Kama mahitaji ya vifaa vya umeme ni 230 voltage
Wewe unaboost voltage ifike ngapi?
Mahitaji ya vifaa vya umeme (load) ni current sio voltage

Voltage booster ina ongeza kiwango cha voltage kulingana na Current inayo hitajika,Fahamu kuwa maeneo ambayo kunakuwa na umeme kidogo,kinacho pungua pale huwa ni VOLTAGE(msukumo) na siyo CURRENT (bidhaa inayo sukumwa)

Hivyo vifaa hivi kazi yake ni kuongeza VOLTAGE(msukumo) wa CURRENT ili kupata uwiano sahihi wa VOLTAGE na CURRENT,kumbuka kwamba nyumba zenye Umeme mdogo zinatumia Current nyingi (ili ku compasate voltage iliyo pungua) Kuliko nyumba zenye umeme sahihi.


Kanuni inasema ili kifaa kifanye kazi ileile sehemu ambayo kuna umeme mdogo ni lazima kita Drain current nyingi zaidi,Hivyo sisi vifaa vyetu vinaongeza voltage ili uwiano wa current na voltage uwe sahihi.


Lakini kumbuka kuwa vifaa vyetu pia vina kiwango chake cha power,kulingana na matumizi yaliyo kusudiwa,viwango hivyo tunavipima katika wattage.

Ikiwa na maana Kuwa booster ina uwezo wake katika kusukuma mzigo flani

Kazi ya hiki kifaa ni kuongeza voltage maeneo ambayo umeme upo chini ya 220V,kwa kawaida kuna maeneo umeme unashuka kati ya 200 hadi 100V,kazi ya kifaa hiki ni kuhakikisha kuwa Voltage haishuki,hivyo kubakia kiwango kile kinacho takiwa yaani 220v
 
Mkuu hebu jibu hoja ya mkuu@puttin hapo juu,alafu ingekua vyema utupatie na bei mkuu.
Nimejibu.

Bei zinatofautiana kulingana na wattage

WATT 1000 = 170,000/=
WATT 2000= 300,000/=
WATT 3000 = 400,000/=
WATT 4000 = 600,0000/=
WATT 5000 = 800,000/=
10KV = 1,400,000/=
 
Nyumba ya ac 2,mafeni fridge,taa na pump ya kisima inahitajika watts ngapi?
 
Bei zinatofautiana kulingana na wattage

WATT 1000 = 170,000/=
WATT 2000= 300,000/=
WATT 3000 = 400,000/=
WATT 4000 = 600,0000/=
WATT 5000 = 800,000/=
10KV = 1,400,000/=
 
Back
Top Bottom