Pole kwa waathirika wote.
Kwa upande wa Kenya, ikiwa ni al-Shabaab, hawa wanapaswa washughulikiwe ipaswavyao. Na nimeshaonya mara kadhaa hapa kuwa hilo si jukumu la Kenya pekee bali hasa nchi zote za Pembe ya Afrika na Mwambao wa bahari ya Hindi na Afrika kwa jumla.
Ikiwa ni vurugu ziinazosababishwa na Wakenya wenyewe, yaliyowafika baada ya uchaguzi wa 2007 yangetosha kuwa ni somo kwao - maelfu ya watu waliouwawa na malaki waliokimbia makazi yao mpaka hadi leo wameshindwa kuwarejesha/ kuwarejeshea makazi.
Kwa upande wa Tanzania, mvua huaza na manyunyu. Tunapaswa kujifunza na hili la vurugu za Kenya kwani mauaji yanayotokea siku hizi ya viongozi wa vyama hayaashirii hatma nzuri. Vyombo vya usalama vinaweza kupuuza, lakini waliopoteza watu wao hawatapuza - watu wataishia kulipizana visasi na cheche ndogo baadae huko mbele inaweza kuwasha moto usiozimika kirahisi.