One stop business center ya Ubungo ikijengwa itaua Kariakoo na kubadilisha mfumo mzima wa biashara Kwa Tanzania na nchi jirani

Ndio ndio !! huu mchezo unafnywa sana mpaka kesho . Wapo vijana wanapiga kelele mitandaoni ila wanatumika na watu wakubwa kupitisha mizigo kwa majina yao .
 
Kariakoo sasa hivi hao unaowasifia hapa hawaagizi tena mizigo kwa container zao wenyewe kama zamani,wanaagiza kupitia kwa makuli wao kama wafanyabiashara ndogo ndogo (hapa sijui kama nitaeleweka)

Yaani wanapeleka hela silent ocean (watu wanasema ni ya GSM)
Sio suala la watu kusema, Silent Ocean ni ya GSM wala hawafichi hilo. Na si lazima wapeleke hela kwa Silent Ocean, mfanyabiashara anayepeleka hela Silent sio mkongwe na hana uhakika na supplier wake. Kwanza unaingia gharama kubwa kuwatumia wao wakulipie badala ulipe wewe mwenyewe.
then mzigo unaandikwa ni wa Mtanzania mfanyabiashara mdogo mdogo kwa title lets say ya Ally (huyu ni mfanyakazi wa mchina mwenye viambatanisho vyote vya biashara but hana frame ni kuli tu) mzigo ukija unapelekwa godown kwa mchina maisha yanaenda.
Hii sawa Kariakoo kuna Wachina wanapita kwenye maduka kukagua mauzo ya mizigo yao huku wakiwa hawana maduka wenyewe.
 
Wakati mnajadili, mlihitimisha ni nini kitachosababisha wateja wa Kariakoo wasiende Ubungo kwa bidhaa ambazo zinapatikana Ubungo na Kariakoo?
Ubungo wako busy kushawishi wafanyabiashara wa Kariakoo kuhamia na most of them wanakataa. Wanaolipia kukodisha maduka hapo Ubungo wengi ni new entrants au wanatokea mikoani. Wafanyabiashara wengi Kariakoo wenye hela zao bado hawashawishiki kupanga Ubungo au kufungua matawi. Na kati ya watu wenye akili sawasawa ni wafanyabishara.
 
Unachosema ni majengo yamejemgwa ila hayana wapangaji?
 
Bora wange risk kwa kufungua tawi huku wakiskilizia upepo lakin hayo maamuzi waliyoyachukua wanaweza kuja kujuta kariakoo pakibuma.
 
Unachosema ni majengo yamejemgwa ila hayana wapangaji?
Hakuna niliposema hayana wapangaji. Nenda hata sasa nafasi zipo hata leoleo ukitaka unalipia kodi ya mwaka unapewa ila haimaanishi hawajapata wapangaji kabisakabisa.
 
Bora wange risk kwa kufungua tawi huku wakiskilizia upepo lakin hayo maamuzi waliyoyachukua wanaweza kuja kujuta kariakoo pakibuma.
Ni wachache wana-risk. Wafanyabiashara wakubwa wa electronics Kariakoo kina Mashariki Power, Zabb, wale suppliers wa brands za hadhi ya wabongo kina iAccess, Aldeppo, Oraimo, Rising, Boss, Aborder, etc wengi wao wakiwa Wachina, Wahindi na Waarabu na mixer ya Wachaga na Wakinga wanaitegemea ecosystem ya Kariakoo.

Kariakoo imeishajijenga kiasi kwamba ukibeba milioni 200 yako ukapata flemu mtaa na jengo sahihi, unaanza kuuza on spot bila kuwa na wateja wa kudumu. Unauzia mawinga na wanunuaji wa jumla. Sasa Ubungo haina hiyo ecosystem, anayeenda ajue anaenda kupambana kutafuta wateja uko.

Ikiwa Wachina watapanga pale sawa, which i believe itatokea baada ya majengo kukosa wapangaji wabongo Mchina aliyejenga atafanya lobbying Wachina wapange pale badala ya Kariakoo. Sitegemei wabongo tu ndio waiinue Ubungo nq kuiua Kariakoo.

Na suala la wateja wa rejareja halipo pale. Wakienda Wachina ujue wanalenga jumla, wakienda wabongo rejareja itasumbua. Hakuna route za daladala kama ilivyo Kariakoo. Raia wakilazimisha kwenda pale wataleta foleni kubwa kuliko iliyo Kariakoo. Na Kkoo ina barabara nyingi njia mbili, chocho za kutosha, mwendokasi inazidi kujengwa nyingine na masoko ya bidhaa zote. Pale Ubungo soko la vyakula sidhani kama litakuwepo. Kariakoo ni dude kubwa
 
Tunaviongozi vichaaa hasa wa awamu hii.hapo wameruhusu wachina Kuja kuchuma Mali za Tanzania na kupeleka kwao china.yaani bidhaa zinazalishwa china Kwa maana ajira ni za wachina halafu wanazileta hapa kutuzuia takataka.Ilitakiwa wajenge kiwanda hapa ili ajira ziwe za wtz na siyo kuwa dumping place for china products.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…