Onesho la mwisho la Franco Lwambo Makiadi, Septemba 22, 1989

Onesho la mwisho la Franco Lwambo Makiadi, Septemba 22, 1989

MT255

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Posts
3,606
Reaction score
4,914
Ijumaa , Septemba 22, 1989 Franco Luambo Luanzo Makiadi alifanya onyesho lake la mwisho maishani mwake katika ukumbi wa De Melkweg jijini Amsterdam Uholanzi. Alipoingia tu katika ukumbi siku hiyo watu wote waliona kuwa Franco alikuwa katika hali mbaya kiafya, ilikuwa wazi siku hiyo kuwa wapenzi wa Franco walianza kukata tama kuhusu afya yake.

Siku hiyo onyesho lilianza na kuendelea kwa karibu masaa mawili kabla Franco kuweza kupanda jukwaani. Siku hiyo kama ilivyokuwa kawaida MC alikuwa mpiga saxaphone wa OK Jazz Isaac Musekiwa, ambaye alikuwa na Franco toka 1957, na ndiye aliyemsaidia Franco kupanda jukwaani na kumuketisha kwenye kiti, lile jitu la miraba minne lilikuwa limepungua sana, hata kusimama ilikuwa ni mtihani. -Wimbo ambao ulikuwa upigwe ulikuwa ni Chacun Pour Soi, uliokuwa umetungwa na Josky Kiambukuta ambaye siku hiyo hakuweko.

Alipoanza tu kupiga ikajulikana wazi alikuwa mgonjwa kiasi cha kushindwa hata kupiga gitaa. Ukisikiliza kwenye video hii utasikia jinsi anavyokosea kupiga utadhani anajifunza wimbo ambao alipiga mwenyewe, inasikitisha. Alijitahidi kuimba- sehemu zake na kujaribu kusimama kilipofikia kipande chake cha kucharaza solo hali ilikuwa mbaya wanamuziki wake walijaribu kumsaidia kusimama, lakini hakuweza kuendelea kupiga tena kwani alikuwa anakosea kosea hakuwa tena Franco yule.

Ikalazimu kuacha jukwaa akiwaacha wanamuziki wake na wapenzi wake wakiwa wamechanganyikiwa kwa majonzi. Machozi yalikuwa yametanda ukumbi mzima. Siku 20 baada ya onyesho hilo tarehe 12 Oktoba 1989 LOkanga Lwa Ndjo Pene Luambo Makiadi akiwa na umri wa miaka 51 tu alifariki katika hospitali mjini Namur Ubelgiji.

Picha hii chini ilipigwa hapo ukumbini inaonyesha jinsi jitu lenye miraba minne Lokanga Lwa Ndjo Pene Luambo Makiadi alivyokuwa amepoteza.

1400925365968.jpg
 
[video=youtube_share;P5jY7KzP8Co]

On Friday, September 22nd, 1989, Franco gave his final performance in De Melkweg (The Milky Way) in Amsterdam. This will be twenty years ago next week.

As soon as he had entered the building, which was well before the audience was allowed in, it was clear that he was much sicker and weaker than the previous time he had performed there () and our hopes of his recovery were smashed to smithereens.

Later that evening, the concert had been going on for what seemed like ages, an hour, maybe an hour and a half, before Franco even entered the stage.

Master of ceremonies: Saxophone player Isaac Musekiwa (who had been with Franco since 1957 and would die only three months or so after Franco), can be seen in the first two pictures on the far left.

Franco had to be helped walking across the stage. Then, he was helped onto a chair on the stage.

The song to be performed was Chacun Pour Soi, composed by Josky Kiambukuta (who was not present).

As soon as he started touching the strings of his guitar, the hairs in my neck stood right up. He was too sick to play, really.

During the first part of the song and during his vocal solo, Franco was still on his chair. Then, when he started what was supposed to become his guitar solo, he tried to stand up, between 6:26 and 6:41into the clip. Two band members had to hold him up, keep him from collapsing. In the interview he refers to this, he had felt obliged to stand up, but he just couldn't do it anymore.

After this, he was escorted off the stage, leaving the orchestra and the audience in total disorientation. I can hardly imagine there was a dry eye in the house by then.

A short interview was done by Boune Zouboye, right after this, which can be heard at the end of the clip.

A little while later, "manager" Manzenza (on the left in the picture here: ... ) escorted Franco out of the building, to the Mercedez waiting there, to be driven back to Belgium. At this time, the orchestra was still on the stage.

20 Days after this gig, on Thursday, October 12th, 1989, L'Okanga Lwa Ndjo Pene Luambo Makiadi died, aged 51, in a hospital in Namur, Belgium.

Ton Verhees was the one who had the strength to take these historic pictures. However, Ton took more pictures before the actual (very short performance), than during it. So some of the pictures you see after the song, were actually taken before it, including the one during the interview.

The recording was made by WorldSrv
( WorldSrv - YouTube )

 
Nimeona interview yake youtube ,aliulizwa kama ana ukimwi akachenga mno then akasema "siku nikifa watu waje waufanyie postmortem mwili wangu wajue kama nilikua na ukimwi" na anadai kukonda kwake (kuugua) kunaeza kusababishwa na nguvu za giza alizojihusisha nazo kabla ya kuokoka

NB: Franco aliwahi mpka kuslimu na kua muislamu then akaja kuokoka
 
Nimeona interv yake YouTube aliulizwa kuhusu kuumwa ukimwi akadai watu wanamsema mno ila yeye ni binadamu hawezi fanya lolote, kila mtu hataki kuamini kua yeye franco hana ukimwi, na akasema akifa afanyiwe postmorterm ili ijulikane kama hana ukimwi, na akadai kukonda kwake ni sababu ya ngvu za giza alizojihusisha nazo, saivi ameokoka kwahiyo ndio zinazomtesa. Franco aliwahi mpka kua muislamu
 
yaa kuna habar hyu bwana alikufa kwa ukimwi tafadhali mwenye taarifa sahihi atupe pamoja na galacha Marijani Rajabu
Yeye mwenyewe alikataa hana ukimwi, bali ni magonjwa mengine, watu walidai ana ukimwi,akawajibu kama wanataka kujua basi akifa wamfanyie uchunguzi, na mmoja wa watu wake wa karibu alimuuliza anaumwa nina, akajibu ni kama tumboni mwake kuna kiwanda kinafanya kazi usiku kucha halali, that is it
 
Kwani alikuwa mchawi huyo mzairwaa! nyumba, mashamaba watoto wake mke wake, aliyeanza naye Maisha wako wapiiiii!! siku hizi?
 
Kwani alikuwa mchawi huyo mzairwaa! nyumba, mashamaba watoto wake mke wake, aliyeanza naye Maisha wako wapiiiii!! siku hizi??
Alikuwa na wanawake wengi, mmoja alikufa na mwingine wa Kwanza yupo, wanae wapo Ulaya, mtoto wake pekee wa kiume anaitwa Emongo ndio maarufu,

Franco alikuwa na Mali nyingi, wakati ule aliishi Ulaya pia,na alifia huko,Mali zake Bado zipo nadhani
 
Alikuwa na wanawake wengi, mmoja alikufa na mwingine wa Kwanza yupo, wanae wapo Ulaya, mtoto wake pekee wa kiume anaitwa Emongo ndio maarufu,

Franco alikuwa na Mali nyingi, wakati ule aliishi Ulaya pia,na alifia huko,Mali zake Bado zipo nadhani
Mali za wenzake km koffi olomide tunaona majumba migari ya kufa mtu kina Bozi huyyuuuremmy mke watoto tunawaona hata aliookoteza huko mitaani majumba nk!! sasa huy icon figure walikuwa wanakula tyuuu na kuhonga kweli??
 
Mali za wenzake km koffi olomide tunaona majumba migari ya kufa mtu kina Bozi huyyuuuremmy mke watoto tunawaona hata aliookoteza huko mitaani majumba nk!! sasa huy icon figure walikuwa wanakula tyuuu na kuhonga kweli??
Huyo wanae Bado Wana maisha lakini naona Wana maintain low key, lakini Mali zake hazifiki za kina koffi japo alikuwa na pesa Miaka hiyo, juzi nimeisikiliza interview moja ya madilu system anadai aliwahi kutumwa akachukue gari ya Franco kwa ajili ya mke wa Franco,madilu akaficha ile gari,Franco akasamehe
 
Aendelee kupumzika kwa amani umeondoka ila bado unaishi tunafurahia kazi zako ulikuja kufanya ulichopaswa kufanya nacho ni burudani.

Sielewi kilingala,sisikii kifaransa zaidi ya salamu ila naufeel mziki.
 
Aendelee kupumzika kwa amani umeondoka ila bado unaishi tunafurahia kazi zako ulikuja kufanya ulichopaswa kufanya nacho ni burudani.

Sielewi kilingala,sisikii kifaransa zaidi ya salamu ila naufeel mziki.
Lwambo bado ataendelea kuishi mioyoni mwa wapenzi wa muziki wake. Binafsi record zake sidhani Kama kuna siku nitachoka kuzisikiliza.
 
Back
Top Bottom