Ongea na Mshua we Ridhiwan ..

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Hizi ripoti asipuuze mshua, hali ya maisha inazidi kuwa mbaya sana. Gharama za hizo semina didimizi zingeweza kununua madawa ya kutosha zahanati zote nchini.

Yale matrekta pale Suma Jkt yatakuja kufa bila kuwafikia wakulima waliolengwa. Ayapeleke kwenye halmashauri za wilaya yakawekwe kwenye vituo vya kukodishia matrekta ili wakulima waweze kuyatumia na gharama zake zitarejea.

Awa tayari kuachana na fikra za kiswahiba za kuteua washikaji, hao ndio wana mwangusha, wengi si safi na hawezi kuwawawajibisha wanapokosea. Ona wale wajakazi wake wa karibu kabisa kama waziri wa elimu, hao wanamiliki shule, wakuu wa Bodi za Zabuni na maafisa masuhuri wa Wizara ndio wanaomiliki makampuni makubwa ya kutoa huduma serikalini.


Mwambie Mshua, kule magogoni tulidhani ndo chuo cha demokrasi, sasa imekuwa ghasi hakuna kitu pale ni mazalia ya waleta udhia katika nchi hii.


Ile aliyowaambia waache uzinzi na ulevi wa kupindukia..ina halalisha ulevi wa kiasi..mwambie Mshua akiwa Dom awe anajaribu kutembelea pale club 84. aone hao jamaa zake wanavyoviumizi vitoto vya wenzao....Spidi ya kwenda Loliondo imeficha mambo mengi sana, kama taifa linaongozwa na wanaoumwa hatima yake ni nini?


Rizi, mwambie Mshua yale maghorofa pale Moro na kule Mbezi beach tumeyaona, hakuna mtazanzania wa kawaida anaweza kufanya kufuru za jinsi hii, kama ni wewe plisi, punguza hiyo kasi Rizi...Sijui lakini kama unakumbuka zile siku ulizotoa za kutaka kuombwa radhi kwa kuchafuliwa,?? tunaona kama zimekwisha na kimya kizito...au ilikuwa stahili ya magamba ...
 
Baba Rizi anajidai hausikii kabisa huo wimbo, ngoja na mimi nimtungie ngonjera, huenda ikamshtua japo kidogo.
 
huu wimbo umepigwa na jamaa anaitwa izzo bussiness..umejaa maudhui ya kutosha,jamaa sio mbana sauti..its such a nice song..
 
uyo ridhi mwenyewe atafikisha maana yemwenyewe gamba
 
Ingekuwa mipasho hapo ungemvuta mh. Ila kwa hilo hit usitegemee jipya.
 
izzo b nmemkubali mwana kaongelea suala la ukwel
 
Nice song, tusubirie wimbo kupigwa marufuku. si unajua viongozi wa kibongo.!!!:dance: but for sure its a nice and focused song.
 
hivi ni kweli kale ka chalii kana degree au mnatania?
 
aliyowaambia waache uzinzi na ulevi wa kupindukia..ina halalisha ulevi wa kiasi..mwambie Mshua akiwa Dom awe anajaribu kutembelea pale club 84. aone hao jamaa zake wanavyoviumizi vitoto vya wenzao

YAANI UKIWAKUTA HAPA MPAKA WANATIA KICHEFUCHEFU, MABABU NA VIJISICHANA VIDOOOGGGOOOO,DAH!!!!!
 
ee bana hili mistari meshiba kama kuna m2 anayo nyimbo nzima attach hapa tufaidi mwanzo mwsho
 
Wasanii wengine wajifunze kwa izzo bN sio kutuimbia mapenzi mapenzi ambayo wao wenyewe hawayajui, namshangaa dully sykes na wimbo wake mpya (bongo fleva) hata sielewi anazungumzia nini!!!!!
 
usipuuzd riz,mwambie mshua street kimenuka mbaya.kasi ya kumchukia mshua imeongezeka mara kibao,chadema wadau nyomi wanaipa gwala,pliz riziwan usipuuze,kijana wake nape anambwela tu yaani hakubaliki kitaa ovyoo,mkama mzinguaji au wanatupia kitu cha kush maana wanavyo bugi balaa.mwambie mshua pia nyodo aache.
 
Jamani ninasikiliza mziki unaitwa we riz1 ongea na mshua! Ujumbe wa mziki huu ni kumuomba riz1 apeleke ujumbe kwa mdingi wake kuhusiana na jinsi mambo yanavokua magumu hapa tz. Nadhani kama mshua akiusikiliza anaweza akanyang'anya ile studio aliowanunulia hawa bongo fleva. Kwa kweli msanii amejitahidi kuwakilisha ujumbe. Kwa namna hii tutaleta mapinduzi tz badala ya kila bongo fleva kuimba nyimbo za mapenzi wakati kuna mambo mengine wanaweza imba.
 
duh!!!nimeusikiliza leo asubuhi.....kuna ujumbe mzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…