Ongeza damu: Tengeneza na kunywa juisi hii

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Posts
2,613
Reaction score
795
Jamani eeh,

Sina fedha wala dhahabu ya kuwapeni wenye tatizo la upungufu wa damu kama vile wagonjwa na wanawake wenye ujauzito, ila nilicho nacho leo nawapa. Niwapacho ni maarifa ya kutengeneza juisi ya matunda na mboga ya majani iliyosheheni madini ya chuma (Iron Galore). Juisi hii ina utajiri mkubwa wa madini ya chuma, folic acid, magnesium, vitamin E na C ambavyo ni muhimu sana kwa utengenezaji wa damu mwilini.

Weka pamoja kwenye mashine ya kutengeneza juisi (Blender) vitu hivi: Kiazi sukari (beetroot) kimoja, apple moja, carrot mbili, mboga iitwayo broccoli kiasi cha nusu kikombe na mjani mawili ya mboga iitwayo 'kale' au kwa kimombo 'Kale leaves'. Kama kuna kitu hapa hujaelewa just google utaona picha yake na kisha nenda sokoni au supermarket ununue.

Ukishatengeneza hiyo juisi kunywa. Ukitaka kutengeneza juisi nyingi zaidi ongeza tu idadi/ vipimo vya hivyo vitu kwa uwiano nilioeleza hapo juu.
 
Maji unamix kiasi gani?
Kiasi cha maji sio muhimu sana. Muhimu ni content iliyomo kwenye hivyo utakavyo-blend. Maana nutrients ni zilezile (fixed) no matter kiasi cha maji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…