BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakati deni la Serikali likifikia Sh71.55 trilioni, Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina amesema Serikali ilikopa fedha zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge na kutaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alijibu hoja hiyo akisema Bunge limeweka ukomo wa kukopa na kwamba kila mradi unaotekelezwa hupitishwa katika bajeti.
“Hakuna sehemu tunakopa bila mradi wala hakuna sehemu tunakopa bila bajeti, tumeweka kila mwaka ukomo wa kukopa ndani na nje ya nchi.
“Busara inayotumika ni kupeleka miradi itakayofungua uchumi. Nchi zinazokua ndio madeni yake yanakua. Maskini yeyote hadaiwi. Ukiona unadaiwa ujue ni nchi inayokua,” alisema Dk Mwigulu.
Juzi, wakati akichangia mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo pamoja na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2023/24, Mpina alihoji kukua kwa deni la Taifa.
Alisema takwimu zinaonyesha deni la Serikali limeongezeka kutoka Sh60.72 trilioni Aprili 2021 hadi Sh69.44 trilioni Aprili 2022, hili ni ongezeko la Sh8.72 trilioni katika kipindi hicho ambalo ni ongezeko la asilimia 14.4.
Aliendelea kuhoji kama miradi iliyoidhinishwa na Bunge kulingana na kasma ya kiasi kilichoruhusiwa kwenda kukopwa na Bunge pamoja na mapato ya ndani, fedha hizo za ziada zilizokopwa na Serikali zilienda kutekeleza miradi gani?
Alisema deni la Serikali lilikua kwa asilimia saba (2019/2020), asilimia 13.7 (2020/2021), asilimia 11 (2021/2022), ongezeko hilo ni kama mara mbili na kwamba deni hilo linaongezeka kwa kasi wakati uwezo wa ukusanyaji wa mapato ni asilimia 11.4.
Pia alisema takwimu zinaonyesha Serikali ilipokea mikopo mipya kipindi cha miezi miwili ya Mei na Juni 2021 yenye thamani ya Sh3.799 trilioni.
Mpina alitaka CAG afanye ukaguzi maalumu wa deni la Serikali katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2020/2021 na 2021/2022, ili kuweka uwazi na kuondoa mkanganyiko kwa Watanzania kuhusu hali ya deni la Serikali.