Wastaafu kote nchini tumeshtushwa sana na tangazo la ongezeko ya pensheni kwa asilimia 2% kuanzia 2025 lililotangazwa na Waziri Kikwete (jnr).
Itakumbukwa kwamba ongezeko hili kiduchu kwa rekodi linafanyika baada ya kupita karibu miaka 10 i.e. enzi za Rais Kikwete na Waziri Mkuya walipoongeza pensheni kwa wastani wa asilimia 26% mwaka 2015!
Pengine Waziri Kikwete na Katambi kutokana na umri wao mdogo hawajui changamoto za wastaafu ambao kwa sasa kima cha chini ni laki 1 au hawajishughulishi hata kusoma historical trends za maboresho ya pensheni.
Mathalani miaka ya 2003 na 2009 serikali za wakati huo ziliboresha pensheni (kima cha chini) kwa asilimia 50% na 77% respectively!
Sasa huu uamuzi wa nyongeza ya asilimia 2% katika kipindi cha Rais wetu mpendwa Mama Samia unaingia akilini kweli?
Hakika huu ni uamuzi wa kuhujumu sifa nzuri ya serikali ya sasa. Ina maana mstaafu anayelipwa laki 1 sasa ataambulia tshs. 102,000/=!. Mungu ibariki Tanzania.