Ongezeko la atheists( watu wasioamini uwepo wa Mungu)

Ongezeko la atheists( watu wasioamini uwepo wa Mungu)

Utajua wewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2024
Posts
928
Reaction score
1,836
Habari wana-JF,

Kumekuwa na uwepo mkumbwa wa atheist duniani, sasa unahisi nini kifanyike kuokoa ndugu zetu?

Na wapi tunapofeli? Na kama tukishindwa kukemea basi tuwachukie kwa moyo wote.

Tujitahidi kusaidia atheist wanapotea vibaya mno.
 
Suala la imani ni ni kubwa sana na ni la mtu binafsi huwezi kumlazimisha mtu aamini unachokiamini wewe na asilimia kubwa ya hawa Atheists ni wasomi wa PHD yani wamesoma filosofia paka imewapoteza kabisa , namaanisha kwamba huwez kuwasaidia kwa chochote kile bali kuwaombea kwa Mungu awafungue mioyo na akili zao ili wapate kumpokea yeye na kumuamini.
 
Kwani Mungu si ametoa uhuru wa kufuata kile unachokipenda na kukiamini

Sasa kwanini tuwachukie wakati wamefata wanachokiamini.....
Leta njia zinazoweza kuwafanya waamini unachokiamini wewe zisipowasaidia waache watumie uhuru wao
Wanatuharibia watoto hawa
 
Pasta mmoja alisema kuwa utoto utumwa,ujana maswali na uzee ugonjwa. Alisema tatizo viongozi wengi wa dini hawapendi kujibu maswali ya vijana kuhusu mambo ya imani
 
Pasta mmoja alisema kuwa utoto utumwa,ujana maswali na uzee ugonjwa. Alisema tatizo viongozi wengi wa dini hawapendi kujibu maswali ya vijana kuhusu mambo ya imani
Kwasababu hawana hayo majibu
 
Habari wana-JF,

Kumekuwa na uwepo mkumbwa wa atheist duniani, sasa unahisi nini kifanyike kuokoa ndugu zetu?

Na wapi tunapofeli? Na kama tukishindwa kukemea basi tuwachukie kwa moyo wote.

Tujitahidi kusaidia atheist wanapotea vibaya mno.
Kwa nini uwachukue wakati hawamtapeli mtu kama wakina Mwamposa au Nabii kiboko ya wachawi?
 
Habari wana-JF,

Kumekuwa na uwepo mkumbwa wa atheist duniani, sasa unahisi nini kifanyike kuokoa ndugu zetu?

Na wapi tunapofeli? Na kama tukishindwa kukemea basi tuwachukie kwa moyo wote.

Tujitahidi kusaidia atheist wanapotea vibaya mno.
Typical mindset ya watu wa dini.
  • Kujihisi mko sawa.
  • Chuki kwa wasioamini ujinga wenu.
  • Hofu kuu ndani yenu.
  • Limited thinking kuhusu kila kinachohusu dini.

Ungekuwa basi unaamini dini iliyochioukia kwenu, hapo utakuwa ni aidha katumwa ka waarabu au watasha.

Jikomboe toka kwenye utumwa wa dini.
 
Habari wana-JF,

Kumekuwa na uwepo mkumbwa wa atheist duniani, sasa unahisi nini kifanyike kuokoa ndugu zetu?

Na wapi tunapofeli? Na kama tukishindwa kukemea basi tuwachukie kwa moyo wote.

Tujitahidi kusaidia atheist wanapotea vibaya mno.
Hizo ni mbinu za Ibilisi,Wanaamini Mungu yupo ila wanajisahaulisha tuu!
 
Kwani Mungu si ametoa uhuru wa kufuata kile unachokipenda na kukiamini.

Sasa kwanini tuwachukie wakati wamefata wanachokiamini.

Leta njia zinazoweza kuwafanya waamini unachokiamini wewe zisipowasaidia waache watumie uhuru wao.
Hata Paulo wa kwenye Biblia alikuwa anaitwa Sauli,Alitokewa na Bwana na kuambiwa unaniudhi na kupofushwa macho!Baadae akaamini ndio huyo Paulo wa kwenye matendo ya mitume.
 
1722856824671.jpg
 
Back
Top Bottom