Ongezeko la bei za bima za magari kuanzia July

delusions

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
5,002
Reaction score
1,287
Gari ilykw inalpw elf 60 kupanda hadi 250000 itv inaongelewa ss hv
 
yaani sasa hivi gari, simu vyote anasa!
 
Biashara ya bima ni huduma.....na makampuni ya bima yamekua yakipata hasara kubwa kutokana na bima za magari.bei ndogo za bima ya magari kumeyafanya makampuni hayo kutokuwa na uwezo wa kulipa madeni kwa wakati hivyo kusababisha usumbufu kwa wateja........hivyo ili kuleta ufanisi na huduma bora ni lazima kwa makampuni haya kupandisha bei ili uwezo wa kulipa madai uwe wa haraka na uhakika.......ijulikane kuwa bima sio anasa au sio kama watu wanafikiria ni kama aina ya kodi..bali bima ni huduma ya kujikinga na majanga...na ni promise ya kampuni hizo kukulipa unapo pata na majaribio ya ajali.......hebu tuchukulie mfano wa hio bei ya mtoa mada ya zamani ya third party ya shilingi 60,000/= chukulia mfano hii gari X ifanye ajali ..na kusababisha uharibifu wa gari Z ..Tuseme gari Z imeharibika yote haitengenezeki....na mfano hii gari ni Noah...thamani yake ni Shs 14,000,000........na mtu mmoja awe amefariki....bima iwe imeamua kumlipa na hiyi fatal accident kwa shs 6,000,000 .....total ya ajali moja tu inakua ni shs 20,000,000...!!!!! sasa wewe jumlisha ...shs 60,000 unazolipa kwa gari yako...na kusababisha hasara ya shs 20,000,000...jee ni gari ngapi zinatakiwa kulipa hio shs 60,000 hadi kufika shs 20,000,000....? bila ya shaka kampuni ya bima watahitaji kufanya bima za magari kama ifuatavo...20,000,000/60,000 =333.....hapa utaona malipo ya gari 333...ndio yatalipa ajali moja tu ya shs 20,000,000......gari ngapi ? 333 !!! jeee kwa ajali ya scania bus inayo uwa kama watu 30 kwa mpigo ? na thamani ya bus moja ni shs 200,000,000 ? fikiria inahataji pooling ya magati mangapi yawe insured ili kulipa dai moja la shs 200,000,000? .....ajali ngapi zinatokea leo...boda boda ngapi zinagongwa......wangapi wanakufa hawa madereva wa boda boda?.......tutambue bila ya huduma ya bima basi shughuli za uchumi zitakufa na kupata msuko suko mkubwa sana.....hivyo ....upandaji huu ni wa lazima......
 
acha porojo ni magari mangapi yanalipia hiyo bima?na magari mangapi yanapata ajali kwa mwaka?
 
sasa gari anasa hiyo ni third part au comprehensive?

Wanatulazimisha tuendeshe Bajaj na Boda boda !! Hii serikali iko madarakani kwa maslahi ya nani? bora iondoke tukae bila serikali.
 
acha porojo ni magari mangapi yanalipia hiyo bima?na magari mangapi yanapata ajali kwa mwaka?
ahsante...mwaka 2012 ajali 24,000 zilitokea.vifo vya ajali 3,900 na majeruhi wa ajali 21,000...
ajali 24,000 x 6,000,000 =144,000,000,000 ...vifo 2900 x 5,000,000 =14,000,000,000.......majeruhi..21,000 x 3,000,000 =63,000,000,000.....weka na magari 1000 yaliobiwa ambayo chukulia 500 ndio yalikua na comprehensive....malipo yote yatakua x 10,000,000 =5,000,000,000 hapa nimechukulia average tu lakini inazidi.....na jumla ya malipo yatakua shsoa 226,000,000,000. na hapa hujatoa gharama za brokers ma assessor.....mishahara sasa tuangalie bima za magari kwa mwaka 2011 ziliingiza kiasi gani ? kwa mwaka wa 2011 bima za magari ziliingiza only 96,000,000,000 sasa kama porojo.......ndio mmezoea....na internet za bure za tigo
 
Nenda shule kasome bwana mdogo, kufanya uchmbuzi wa Bima wee bado. Aliyekwambia 60,000 inayolipwa inaenda kuwekwa uvunguni mwa kitanda nani? Na je unajua kwamba kuna mashirika ya Bima hapa duniani yanatoa gawio la faida kwa wateja wake? Je unajua kwamba kuna mashirika ya bima huwa yanarudisha hizo "60,000" za wateja? Sidhani kama mnacheza vizuri na ile 'kanuni ya uwingi'. Kwa kukusaidia tu uchambuzi mzuri ni ule unaoangalia nyanja zote na 'sequntial effects' kwa kila hatua itakayochukuliwa. Kwa kuwa watumiaji wa magari nchini wanaonggezeka, ili mpate faida ambayo ni 'abnormal', ihimizeni serikali kufanya yafuatayo:-
1. Kuboresha ubora wa Barabara ili kupunguza uwezekano wa ajali;
2. Jeshi la usalama wa barabarani lisimamie sheria ipasavyo na sio kuwa watu wa deal tu ili kupunguza ajali;
3. Idara zinazosimamia leseni zitoe leseni kwa kuzingatia sifa siyo kama chanzo cha mapato ya serikali;
4. Iondoe gereje bubu za mitaani ambazo huwa zinawaaminisha wenye magari kuwa gari zao ziko vizuri haliyakuwa ni mbovu;
5. Nguvu kubwa ya polisi itumike kwenye kulinda usalama wa raia na mali zao sio kuzuia mikutano ya siasa ili kupunguza wizi
6. Ihimizeni serikali izuie uingizwaji wa spare fake za vyombo vya moto na over-used spares ili kupunguza uwezekano wa ajali
7. Serikali isimamie uzalishaji wa viwandani na kuongeza ajira zenye kipato cha kati ili kuongeza idadi ya watumiaji na magari
8. Serikali iimarishe na kuboresha usafiri wa umma ili kupunguza matumizi ya kila siku ya magari binafsi hivyo kufanya magari yatumike kwa shughuli binafsi ndogondogo kama kwenda sokoni na crucial events tu huku yakiwa yamelipiwa hiyo bima

Uchambuzi unaolenga kupandisha gharama katika huduma siku zote hauleti faida kwa jamii(social welfare) ambao matokeo yake ni kuathiri mfumo wa siasa na hatimaye kutetemesha Serikali ikibidi hata maandamano na kuangushwa kwa serikali. Hili limethibitishwa kwenye nyanja nyingi ikiwa pamoja na katika ushuru wa forodha. Kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma ndio chanzo kikubwa cha maandamano na kuangushwa kwa Serikali nyingi duniani. Haiwezekani katika sekta ya gari tu mkapandisha gharama ya kila kitu halafu mkajiona mko salama. Nyie watu msikariri kwamba price=profits tu siku zote.
 
....ndio mmezoea....na internet za bure za tigo

Na hapa umeona unavyodhihirish upeo wako mdogo, hizi huduma za free internet, cheaper calling rates ni vitu ambavyo havikwepeki sasahivi duniani kadri teknolojia inavyokua duniani hasa uwezo mkubwa wa simu za mkononi. Hata hayo makampuni mengine yajiandae tu na free internet services si miaka mingi inayokuja.
 

Wewe ni kipeperushi cha serikali ya Magamba. Mtaona basi kama tutalipa hizo bima. Sanasana tutatenga tu ela ndogo ya trafik police maisha yataendelea. Mburula bin Magamba, hovyo sana nyie mashetani.
 

CRABAT kama atakusoma positively naamini ataelekeza nguvu zake kutafuta shule ajiendeleze kwenye hiyo secta! Hata uchambuzi huo mdogo sana aliofanya amepotoka sanaa!

Serikali hapa wameharibu sana. Huwezi kupandisha kodi ya Mafuta, Bima na Road licence, wakati hapo hapo juzi juzi umebadli mfumo wa kutoza kodi ya kuingiza magari na kuweka formular nyonyaji ukadhani umefanya jambo jema kwa uchumi na usalama wa taifa!
 
Wewe ni kipeperushi cha serikali ya Magamba. Mtaona basi kama tutalipa hizo bima. Sanasana tutatenga tu ela ndogo ya trafik police maisha yataendelea. Mburula bin Magamba, hovyo sana nyie mashetani.
wacha ujinga...bima ni biashara hina siasa...haya wewe utahonga trafic ngoja ugonge mtu afe then huyo awe mtoto wa mwanasheria ndio utajua kumbe nilikua mjinga..na utafilisika...kwa madai utayodaiwa
 
Wakuu kwanza niseme mimi niko Alaska sasa mambo ya bima hususan kwenye dunia ya kwanza ni ghali sana ndio sababu ajali zimepungua kwa sababu huwezi endesha gari bila bima na unaposababisha ajali ndio bima yako inapaa kila mwaka. kwa hiyo basi unapata changamoto kuwa dereva mzuri ili bima ya gari iwe poa.

Sijui Tanzania kampuni za bima ziko ngapi? Je kuna ushindani wa kiasi gani au ndio mafioso wanataka kujitajirisha kwa namna flani kama vile ilivyo kwenye simu za mikononi? Ikumbukwe kwamba kazi ya kwanza ya JK ilikuwa kuliuwa shirika la posta na simu ili makuwadi wake wa Voda waweze kuwakamua Watanzania inavyostahili, sasa sijui kama huko kuvimbiwa kwao kwenye simu hakutoshi na sasa wanaingilia kwenye Bima au ni kweli jitihada za serikali kutumia nyenzo hii kupunguza ajali.
 
nyote mmejitahidi kuchambua...lakini lazima mujue...secta ya bima ni huria
pili ongezeko la bei lolote sio kwa ajili ya faida tu
mujue bei za bima hazipandishwi tu kama bei za embe sokoni
bei za bima zinapangwa kwa kuweka vitu vinaitwa Risk premium,administration cost na profit margin ambayo mashirika yote ya bima wanafata international standard ya 5% kama faida....na hii faida huwa haijulikani ina tegemea claims zinazolipwa
hapa mnachamganya siasa na biashara na huduma....someni taarifa ya mwaka kuhusu bima...makampuni 11 yapo ICU yaani yamefilisika mojarra limenunuliwa tayari na kampung ya KEnya
yaliobaki yamepata has aura lakini yaani service kwa vile shareholders wameengeza capital. !!! Sasa hali hii ni maya kwa uchumi huwezi kuruhusu makampuni zaidi ya 15 ku fungi virago utasababisha mtikiso mkubwa wa ssecta ya fedha na uchumi
hivyo lazima haya makampuni yajiendeshe ku huduma uuchumi wewe usifiiiri gari Lakota tu Kiwanda cha madawa kilipoungua waliweza ku retain wafanya kazi wao na wamelipwa na kutengeneza Kiwanda chao
shughuli za uchumi zinaendelea msichanganye uchumi biashara na mambo ya mwagwanda na magamba tunaahitaji soko la bima lenye nguvu...kama huoni umuhumi wa bima basi wachia..lakini wapo wataoona umuhimu wa secka hii kuwa imara


 
Ongezeko la gharama za Bima kwa Third party halikwepeki. Nafikiri sasa wengi wataenda kwenye Comprehensive.
Ni kubadili mfumo tu watu watabadilika, unatembelea gari ya milioni 40 lakini bima ya laki moja...kisa? unakwepa Comprehensive wakati kuna risk kubwa za ajali, moto na wizi (hasa wa vifaa vya magari).
 
Kampuni zenyewe za kibongo zimekaa kiwiziwizi tu ukipata ajali hadi ulipwe lazima utoe hongo la sivyo imekula kwako
 

Mkuu hapo kwa red unajua maana yake?
kwa TZ bima hai-qualify kuwa kwenye category hiyo kwa sababu ni product inayolazimishwa na sheria kwamba kila kwenye gari akate bima! hakuna option nyingine kwa mtumiaji
 
Kama ingekuwa hivyo, kusingekuwa na kampuni ya bima ambayo ingekubali kufanya hii huduma.
By the way acha kupotosha au go back to school.
 

Umetusoma positively? Shauri yako kama utaendelea kutusoma negatively na kudhani tumekudharau! Hata hapo juu unazidi kujichanganya tu, na kujiaminisha uko sahihi! Unasema sekta ya bima ni huria... halafu eti huwezi kuacha kampuni zife!, nini maana ya huria sasa! Halafu tumeongelea bima ya magari hasa ile third party ambayo ni lazima kulipa na ambayo hupangwa na serikali kisheria. Tatizo ninaloliona ni kwamba mashirika ya bima yanataka kujiendesha kwa kutumia rungu la serikali katika bima hii ya magari badala ya kuwa wabunifu katika biashara yao. Hii sio njia sahihi ya kuimarisha mashirika ya bima. Huo u-huria wa kupanga bei za bima nyingine hakuna aliewazuia, wanashindwa tu kwasababu equillibrium ya demand na supply imefikiwa na huwezi kuongeza bei bila kushusha demand kwa kiwango cha hatari.
 

well said Sir! Am sure guys in such offices have forgotten that what they propose into law now will chew on their pension sooner or later, they even forget that Government fringe benefits are attached to their office not their person!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…