Ongezeko la kodi ya Mafuta ni kuwalipa fadhila "Wakubwa" wanaomiliki hisa/makampuni/vituo vya Mafuta?

Ndio maana hata mimi nikasema kama mafuta yanawasili hapa nchini kwa gharama ya sh 1110, haitakiwi yauzwe zaidi ya 1,600 maana yake muuzaji unamuwekea apate faida ya sh 200 kisha hiyo sh 300 ndio iende selikalini

Kwahiyo kuna shida huko selikalini.

Huwezi kupunguza kodi za pombe na kubet kisha unaongeza kodi kwenye mafuta!

Samia asipoangalia mafuta yatafika 3000 by December.
 
Na kazi iendelee, vyuma ndiyo vimezidi kukaza, yeye ndege tu na kupaka lipstick...
 
Narudia, issue hapa sio Samia bali Serikali za CCM zinazofanya mafuta kuwa chanzo cha mapato kwa sababu zimeshindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato!!

Halafu unajua nini...

Jinsi ulivyojikita kwenye hoja ya betting nikalazimika nitafute hotuba ya Mwigulu!! Nilichogundua, ni tofauti na unachojaribu kutuaminisha hapa!!

Alichosema Mwigulu, kodi imepungua kwa pesa anayolipwa mshindi aliyecheza kwenye hiyo michezo lakini kodi imepanda kwenye mapato ya kampuni za betting kutoka 25% to 30%!!


Sasa kwanini unapotosha ndugu yangu?!

OH! Let me guess... ni katika lile lile la kuonesha "...Haya yanatokea kwavile Magu hayupo", ambapo nikisema Magu huwa mnampa asizostahili, utarudi kusema "yaani naumia sana nikiona Magu anasifiwa"!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]We jamaa bhana! Unamtengaje Samia na ccm?

Kwanini kwenye korosho unamlaumu Magufuli tu ila kwenye mafuta hutaki Samia alaumiwe!
Unahisi tunamkandia Samia sababu ya Magu?

Mafuta yanabebeshwa zigo kubwa la kodi ndio maana yanapanda bei,
Sasa wewe kwenye utetezi wako unasema soko la dunia!

Soko la dunia vipi wakati Rwanda Burundi na Zambia wanaochukua mafuta hapa bei zao zipo chini?

Mkuu, wewe kama una mahaba sana na Samia yawe kwa kiasi!
 
Ndo maana husikii progress kwenye miradi ya matumizi ya gesi asilia kwenye magari na kupikia majumbani, yaani ni thinking ya hovyo kudhani kwamba kuruhusu progress kwenye energy ambayo ni low cost na isiyo na madhara makubwa kwenye mazingira kama gesi ni kuua mapato ya kibeberu na kifisadi yatokanayo na biashara ya mafuta, bull shit!
 
Komeo wewe ni Mtanzania kama Magufuli. Ninasikitika sana kwamba sisi Watanzania hatujielewi au hatueleweki. Bajeti ilisomwa vizuri na kuainisha ongezeko la baadhi ya bidhaa ikiwemo mafuta kwa shilingi 100 na lengo likiwa limewekwa bayana. Je, tulitarajiwa huo mzigo utamwangukia nani kama sio sisi walaji Watanzania? Sasa hii hamaki inayokuja baada ya kuanza kutekelezwa kwa bajeti inatoka wapi? Tuache unafiki!
 
Duh!! Kwahiyo unataka kusema nilikuwa namshutumu Magu kwa kushuka bei ya korosho?!! Mimi sio mbumbumbu wewe, na narudia tena hapa... mambo ya kiuchumi naongea kiuchumi!!

There's no way ningeweza kumlaumu Magu kwa kushuka bei ya korosho wakati najua bei ya mazao ya biashara inategemea sana na soko la dunia!!

Kwenye korosho, nilimlaumumpinga Magu mambo yafuatayo....

1. Wafuasi wa Magu kutaka kuaminisha kwamba, bei mzuri ya korosho ilitokana na Magu!! Hapa nikawa natoa hoja hapa kwamba, kama ni yeye basi apandishe na bei ya pamba ili ndugu zake waneemeke!!

2. Nilimlaumu Magu pale alipotuma jeshi na kuingilia ununuzi wa korosho, na nikasema wazi kwamba anachofanya Magu kitaleta damage kubwa kwenye zao la korosho! Hoja hapa ilikuwa ni kumtaka aache nguvu ya soko ifanye kazi!!

Hapa ningekuwa kwenye PC, ningekutafutia posts zangu kuhusu korosho, na uone Magu nilikuwa namlaumu au kumpinga nini kuhusu suala la korosho!!
 
Sasa kwanini hukuilamu ccm kama unavyotaka sasa hivi tuilamu ccm badala ya Samia.?

Mkuu, haya mahaba yako kwa Samia hata kwa vitu vilivyowazi yanatoka wapi?

Samia ndio Rais wetu na nikakwambia kwa mujibu wa wenzetu wanaoingiza mafuta, hadi yanafika hapa bongo lita moja ina gharimu sh 1110 kwa hiyo kinachopandisha bei ya mafuta ni makodi!

Wewe ukaja na utetezi kwamba Samia asilaumiwe ni soko la dunia, ukaenda mbali na kusema mbona kipindi cha Magu 2018 bei ilikuwa juu. Lengo lako hapa ulifikiri tunamkandia mama na kumpa ujiko Magu ndio ukaona usawazishe mambo.

Mim nakuuliza tena hao BURUNDI, RWANDA, ZAMBIA wanaochukua mafuta hapa kwetu na bei zao zipo chini wao wanachukua kwenye soko la dunia tofauti na hii yetu?
 
Watanzania wana mahaba na mihemko ya hovyo. Yaani kuna watu wana Mahaba na Samia hawataki akosolewe. Watakwambia sababu ni Mwanamke au ni Muislamu. Lakini kwa Magufuli kumkosoa na kumtukana ni sawa. Hapa nashindwa waelewa watanzania.

 
Ficha ujinga wako mkuu- angalia trend ya soko la mafuta duniani utapata jibu badala ya ranli zako chonganishi
 
Ficha ujinga wako mkuu- angalia trend ya soko la mafuta duniani utapata jibu badala ya ranli zako chonganishi
Ficha upumbavu wako dogo angalia bei wanayouzia mafuta Zambia wanaopitisha kwetu mafuta .acha mahaba niue
 
Ni katika harakati za kuukimbia ukweli na kutanguliza mahaba, uchama na ubinafsi zaidi ya walio wengi.

Ukiweka maslahi ya walio wengi mbele, zaidi ya 80% ya waTz wanaishi kwa $1 kwa siku, na haya ndio maisha halisi ya TZ. Wachache wanaoishi kama wako paradise, ni wale ambao ukimwambia mkae mezani, mapato yake halali hayaungani na uhalisia wa maisha yake na hawa ndo wadhulumu wakubwa wa wale 80%

Chama kimekuwa kikifadhiliwa na hao wenye kudhulumu walio wengi, na kuna wakati ni kwa lazima; anapewa mianya ili aweze kufadhili chama, angalia matajiri wa mafuta kipindi kile, wamefia wapi kama biashara ni halali kwa mujibu wa taratibu?

Na wale wengine akina TICTS, ni untouchables; mmiliki alikuwa mtunza hazina wa chama, hao kina Meremete, Bulyanhulu, Liganga, vitalu vya uwindaji n.k, wote wakilindwa na chama kwa makusudi maalumu.

Unamkumbuka mfanyabiashara fulani aliamua kujitoa chamani karibia na uchaguzi, akatangaza, kontena mbili zikazamishwa baharini, akarudi!

Tunaaminishwa bandari bagamoyo ni muhimu, hii si ni kama gesi ilivyouzwa kwa hati ya dharula bungeni, usiku kwa usiku? Nani ni mnufaika kwa sasa? Si ni huyu huyu spika alikuwepo? Anajua utamu wa usaliti na hawezi kuacha; lengo la kutaka kuleta bomba la gesi bagamoyo na bandari yake unadhanj ilikuwa kwaajili ya watanzania na wanabagamoyo? Kuna nini kitakachoathirika pale Mtwara kama tukisimamisha na kujenga libandari likubwa kabisa duniani na gesi ikauziwa kule tukaachana na gharama za kusafirisha bomba mpaka bagamoyo?

Kodi za kipumbavu kwaajili ya wenye chama ndo mwiba kwa 80% ya waTz, niliwahi kuwa mpokeaji mafuta miaka fulani, yalikuwa mpaka yakiingia depo, ni sh 590 kwa lita kwa dizeli ilhali mtaani ilikuwa sh 1600. Sukari pale kiwandani inatoka kwa sh 490 kwa kilo kipindi hicho, mtaani ikiwa sh 1,300 yaanj kutoka hapo tu kiwandani.

Tulisikia Shimbo ana 3trilioni kule SA, kwa namba moja kupewa taarifa miaka ile, nini kimefanyika mpaka leo? Ni mtanzania gani akiwa mtumishi wa serikali anayeweza kuwa kiasi hicho cha pesa kihalali?

Unataka walio kwenye hiyo cheni, baada ya kuzibiwa mianya yao, wafurahie?

Atakusumbua bure tu, ukweli ni huo; kama unavyosikia siku hizi kuna CHAWA, basi elewa hao wanaoiifanya wanaelewa uchumi na mambo yanavyopaswa kuwa kwa maslahi ya wachache ni CHAWA tu na ndio wenye ujuaji huko mitandaoni.
 
Bei ya sukari sh.kwa kilo,Bei ya mafuta kula sh.kwa lita,bado Bei ya simenti sh.kwa mfuko mmoja wa kg.50.leo tunajadiri petrol,tunakoenda Ni kubaya zaidi.
 
Moja ya vitu vibaya tulivyoachiwa ni serikali iliyopita kulalamika lalamika tu sasa watu iwe twiter,Instagram,mtaani,facebook,tik tok ni kulalamika lalamika tu utadhani miaka mitano iliyopita tuliishi kwa neema.Wakati ukweli ni kua watu wengi waliishi maisha magumu yenye kukata tamaa.Waliokua wanafurahi san ni wale wanaopenda kuona matajiri au wenye uwezo wanafilisiwa au kunyang'anywa walichotafuta.Tuache kulalamika lalamika tujikite kwenye biashara,ubunifu na kupigania maendeleo binafsi na ya taifa na pia kuzingatia maslahi ya taifa inapobidi.
 
Duh!

We jamaa wewe...

Hivi JPM alipofanya mambo yake kwenye korosho kuna mtu alimshirikisha?!

Hivi yale yalikuwa ni maamuzi ya taasisi yoyote?

Au unataka kujisahaulisha ile siku Majaaliwa alikuwa anajaribu kuelezea mikakati ya serikali ili kunusuru bei ya korosho lakini Magu akamkatiza na hapo hapo akaagiza JKT waende Kusini?!

Nimekupa mfano wa bei ya mafuta July 2018 kwa sababu wewe ulitaka kudanganya watu kwamba:
Magu alikuata mafuta yanauzwa kati ya 1900 hadi 2100 na alimaintain bei isivuke 2200 kwa muda wake wa miaka yote 5
Na kwahiyo nilileta hoja ya kipindi cha Magu sio kwa ajili eti ya kutaka kuweka mambo sawa kama unavyotaka kupotosha tena hapa, bali kukuonesha it doesn't matter madarakani yupo nani, na ndipo nikasema:-
Na kukuthibitishia, nikakupa takwimu za bei ya mafuta July 2018 ambapo ilikuwa Sh. 2,409!! Sasa kuna mahali nilipomlaumu Magu hapo?!

Na post yangu ya kwanza kabisa kwenye ule uzi unaosema eti nilikuwa nasawazisha, ni hii hapa:-
Na post yangu ya pili, ndo hiyo ambayo nilikupa takwimu za bei ya mafuta July 2018!

Sasa hoja yako kwamba:-

Wewe ukaja na utetezi kwamba Samia asilaumiwe ni soko la dunia, ukaenda mbali na kusema mbona kipindi cha Magu 2018 bei ilikuwa juu. Lengo lako hapa ulifikiri tunamkandia mama na kumpa ujiko Magu ndio ukaona usawazishe mambo
Sasa nilikuwa nasawazisha nini hapo?! Kwenye hiyo post ya kwanza kuna popote nilipomtaja Samia, zaidi ya kuhoji takwimu za The Boss?!

Mim nakuuliza tena hao BURUNDI, RWANDA, ZAMBIA wanaochukua mafuta hapa kwetu na bei zao zipo chini wao wanachukua kwenye soko la dunia tofauti na hii yetu?
Hivi huwa unasoma, au huwa unakurupuka tu kujibu kabla hujasoma? Nimekuuliza chini kulinganisha na wapi, na hiyo chini ni ipi?! Unasemaje tu "bei ipo chini" bila kutaja bei husika? Au unabahatisha?!

Lakini kwakuwa nilijua hutaweza kujibu hilo swali, nikakutajia kwamba, mwezi ulioshia June 30, bei ya petrol Rwanda ilikuwa Rfw 1,088 na Burundi ni $1.28!!!

Na nimekuambia hiyo ni bei kabla mafuta hayajapanda kwenye soko la dunia!!

Sasa hivi kweli kama unaelewa ulitakiwa kurudia hilo swali?! Na kama unamaanisha bei ni chini kulinganisha na Tanzania, umeshindwa hata kutumia Google Currency Converter ambayo ingekupa:-


Mbaya zaidi, nikakuwekea hadi melezo ya GlobalPetrolPrice.Com yanayosema ni kwanini bei ya mafuta inatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine ingawaje bei wanayonunulia soko la dunia ni moja!!!

Nikaenda mbali zaidi kukuambia maeleo hayo ya GlobalPetrolPrice.Com yanaendana na kile kilichofanywa na Zambia, kwamba:-
LUSAKA, Feb. 3 (Xinhua) -- The Zambian government has granted Oil Marketing Companies a waiver to enable them to import finished petroleum products at a cheaper price.

Minister of Energy Matthew Nkhuwa said the waiver will run for six months.

Sasa unapoendelea kurudia kitu kile kile kwamba "...mbona wao bei ipo chini", hiyo Sh. 2558 ipo chini ya nani?! Sasa kama Rwanda ambao bei ilikuwa $1.10, ambayo ni zaidi ya Sh 2550, what about Burundi ambayo bei yake ilikuwa $1.28?!

Ndo maana naendelea kukuuliza... CHINI YA NANI? AU CHINI KULINGANISHA NA WAPI?

Tusichoshane bhana....
 
Mkuu endelea kumtetea mama
 
Shukrani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…