Watanzania nawasalimu,
Nimejaribu kuwaza ni wapi tunakoelekea nimekosa majibu. Viongozi wetu na watanzania wote ni mashuhuda kuwa tumeambiwa kuwa kuhusu nyongeza ya mishahara tusubiri uchumi uimarike kidogo.
Lakini Leo hii huyu huyu mtu anaeomba kuongezewa mshahara kutokana na kuongezeka kwa garama za maisha Leo hii anatakiwa tena achangie uchumi kupitia miamala anayofanya.
Binafsi nilifikiri mtu anapaswa kuongezewe kipato ili aweze kuchangia uchumi na si kuchangia uchumi akiwa na hali ngumu ya maisha ili aje aongezewe kipato.
Watanzania tunapaswa kujitafakari sana juu ya uongozi tunaoutaka. Nafkiri wawakilishi wetu hawajali chochote kuhusu maisha yetu. Hivi mtu anaekulilia umuongezee mshahara, unamuongezeaje gharama tena na hata hujamuongezea huo mshahara? Huoni kua unamuongezea ugumu wa maisha zaidi?