dour
Member
- Aug 7, 2017
- 7
- 9
Muhtasari
kulingana na kukua kwa takwimu za vifo vitokanavyo na wivu wa mapenzi, Andiko hii imeangazia kwa undani juu ya asili ya wivu, uhusiano uliopo kati ya wivu na mapenzi, namna wivu unaleta uhalifu, na nini chakufanya kutatuta uhalifu huu wa hisia.
UTANGULIZI
Mnamo tarehe 16 ya mwezi wa saba 2020 vyombo vya habari vilirindima kwa habari ya kusikitisha ya mauaji yaliyotokea Mbezi Makabe juu ya kijana aitwae Hamis Abdallah aliye chomwa moto na mpenzi wake aitwae Grace Mushi sababu ikielezwa ni wivu wa mapenzi.
Tarehe 10 mwezi wa 8, 2021 huko Mbeya mwalimu ajulikanae kama jina la Jema aliuawa na mpenzi wake kikatili sababu ikiwa ni wivu wa mapenzi (wasafi tv). Mnamo tarehe 20/09/2021 mwanamke ajulikanae kama Zulfa aliuawa kikatili sababu ikitajwa ni wivu wa mapenzi (wasafi tv).
Mnamo tarehe 23/09/2021 mwanamke ajulikanae kama gladiness aliuawa kikatili chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi (wasafi tv). Mnamo tarehe 23/09/ 2021 kijana ajulikanae kwa jina la Isiaka aliuawa na mpenzi wake kikatili chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Tarehe 22/12/2020 Kamishna wa Polisi wa Dar es Saalam, bwana Liberatus Sabas aliambia vyombo vya habari nchini juu ya ongezeko la matokeo ya kihalifu yatokanayo na wivu wa mapenzi. Hii yote ikithibitisha kuwa uhalifu utokanao na wivu wa mapenzi kitaalam ujulikanao kama (crime of passion) uhalifu wa Hisia umekua janga linaloangamiza jamii kwa kasi kubwa.
MAPENZI NA SAYANSI
Ni wazi kuwa umoja, muungano katika jamii, ukuaji wa uchumi na maendeleo huletwa na kuwepo kwa amani. Na amani huletwa na upendo. Upendo ni hisia za ndani za uhitaji wa kitu au mtu. Upendo waweza kuwa kati ya wanafamilia, wanajamii au wanandoa.
Mwanasayansi na mwanasaikolojia aitwae Gail sulz alielezea sayansi juu ya mapenzi na upendo, alisema mapenzi huleta uraibu kama vile yaletavyo madawa ya kulevya. Ukaribu na hisia huweza kusababisha uzalishwaji wa homoni iitwayo dopamine pamoja na oxytocin hizi homoni ni mahususi kwa uraibu na huleta utegemezi kwenye mapenzi.
Tafiti huonyesha mapenzi huleta maumivu sawasawa na maumivu mengine au zaidi, na hii hutokana na kutokuheshimiwa, kutokujaliwa au kuthaminiwa na mtu unaempenda.
WIVU NA MAPENZI
Dr Sue Johnson katika kitabu chake cha "Love sense", ametafsiri wivu kama hisia za kufadhaisha sana zitokanazo na upungufu wa upendo kwa mwenza wako. Kulingana na mtafiti Lec Edward amegawa wivu katika nyanja mbili moja ikiwa ni wivu wa kingono, na wivu wa hisia.Wanaume hupata wivu wa kingono zaidi ukilinganisha na wanawake ambao hao hupata wivu wa kihisia zaidi. Wivu wa ngono huletwa na hisia kali za matamanio ya ngono kwa mwenza wake. wivu wa kihisia ni wivu unaoletwa na hisia kali juu ya uitaji wa kujaliwa, kuthaminiwa na mwenza wake.
Wivu una nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya mahusiano. Mwanafalsafa Ted fischer alisema kwenye kipindi cha Think big kuwa "wivu ni nguvu inayo unganisha upendo madhubuti". Katika watu kumi walio hojiwa na muandishi wa makala hii, watu nane waliafiki kuwa kuna umuhimu wa wivu katika kulinda mahusiano na wengine wakiafiki wivu ni ishara ya upendo wa dhati kwenye mahusiano baina ya mtu na mwenza wake.
Dr John gottman ni mtafiti wa masuala ya mahusiano anaeleza kuwa kuna sababu mbili zinazopelekea mtu kuwa na wivu katika mapenzi ambazo ni vinasaba vya urithi na mazingira ya makuzi katika jamii. Katika utafiti wake alioufanya mwaka 2013 alibaini mapacha au watu wenye vinasaba vya chimbuko moja huweza kuwa na hasira sawa au wivu sawa. Kwa upande wa pili watoto waliotoka kwenye makuzi ya manyanyaso, mateso na wivu wameonesha uwezekano wa asilimia 60 kuwa na hizo tabia ukubwani na hata kwenye maisha yao ya mahusiano.
Kuna tofauti kubwa iliyopo kati ya wivu na mashaka, wivu ni uhitaji wa kuona upeeke uliopo kwako juu ya mpenzi wako, hutaki kuona unachofanyiwa kama mpenzi kufanyiwa mtu mwingine. Mashaka ni wasiwasi juu ya kupoteza penzi lako au mabadiliko ya tabia ya mwenza wako ambayo huku yazoea.
Wivu na mashaka kwenye mahusiano husababishwa na kutokujiamini, kujiona huvutii, fikra hasi na kutokumuelewa mwenza wako. Wanaume wengi hukiri kuwa na wivu zaidi pale wanapo gharamia wenza wao kisha kuoneshwa dharau kwenye uhusiano.
UHALIFU WA HISIA
Mnamo mwaka 1951 tukio lililoshangaza ulimwengu, lilitokea Urusi ambalo lilitikisa vichwa vya Habari ikisimuliwa katika kitabu "The World great crime of passion" cha kwake Tim Healy kilieleza kisa hicho kwa kina, ilikuwa ni juu ya mauaji ya aliyekuwa waziri wa inchi hio Bwana Pierre Chevallier aliyeuliwa na mkewe Yevonne sababu ikiwa ni wivu wa mapenzi.
Katika tovuti inayo chambua takwimu mbalimbali ya Hurumap imeonesha vifo vitokanavyo na wivu wa mapenzi kuanza kuongezeka kwa kasi kuanzia 2015 katika mikoa mbali mbali hapa nchini.
Ongezeko hili la mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi linashika nadharia ya kuwa janga jipya bila watu kufahamu kuwa lina sura ya kuwa janga. Elizabeth Coldwell katika kitabu chake cha "when love break the law" aliandika Uhalifu wa hisia (utokanao na wivu wa mapenzi) ni uhalifu hupasao kupewa jicho la tatu katika jamii licha ya jamii kuona wepesi juu ya jambo hili.
Ukubwa wa tatizo hili unatakiwa upewe uzito sawa kama uhalifu mwengine mfano ujambazi n.k. Uhalifu wa hisia katika mapenzi unahatarisha amani katika jamii kwa kiasi kikubwa, Wengi wa wanajamii wakitishia kuwa endapo wataachwa basi wako tayari kufanya chochote watakachokiamini ni fidia juu ya mapenzi yao.
Wivu na mauaji
Je, kuna ulazima wa kuua au kujeruhi kisa mapenzi?
Mwandishi maarufu shake spare, "wivu ni ushetani na mbegu ya uhalifu katika jamii”. Bwana mmoja ajulikanae kwa jina la Mohamed Burhan ameeleza sababu mpaka kufikia mauaji ni hali ya mtu kutaka kuwa pekee katika mahusiano lakini pia kujilinganisha kwenye mahusiano, amesema kila mtu anahitaji kupendwa na kuthaminiwa kwa namna ileile anayomthamini mwenza wake.
Kuwepo kwa michepuko na wapenzi tofauti tofauti kumetajwa kusababisha wivu wa mapenzi ni kutokana na kupungua kwa thamani ya mapenzi ikihusishwa na fulani kua chanzo. Bwana kilango ramadhani ameeleza kukasirishwa na jirani aliye kua na mazoea Na mpenzi wake na kumsadiki kua yeye ndo chanzo ya kutothaminiwa katika maisha yao ya mahusiano.
Sauti ya Muhammed Burhani na Kilango Ramadhani
Dr. Russed grieger katika kitabu chake "couple therapy companion" ameandika uwepo wa wivu husababishwa na kumjali mwenza na kumuhudumia. Wanaume wengi ambao huwahudumia wake zao kwa thamani kubwa wameonesha kuwa na wivu zaidi kwa wenza wao mpaka kupelekea kuwatendea vibaya ambao wanahisi wana mahusiano ya kimapenz na wenza wao.
Nini kifanyike kupunguza Janga hili?
kutokana na ongezeko la idadi ya wahanga, majeruhi na vifoo vitokanavyo na uhalifu wa hisia (uhalifu utokanao na wivu wa mapenzi) ipo haja ya kulipa uzito jambo hili kwa upana ili kuweza kulitatua, kulipunguza na hata kuliondoa.
Serikali na wadau wangane katika utoaji wa elimu ya mahusiano. Ni aibu katika jamii kuona wazazi wanaogopa kuelimisha watoto wao juu ya masuala ya mahusiano ikiwa hakuna mahala popote mtoto anapoweza kupata elimu hiyo sahihi. Shuleni pia huishia kufundishwa mifumo ya uzazi tu lakini sio elimu ya mahusiano. Ipo haja yakushirikisha wazazi, walezi, viongozi wa dini na viongozi wa serekali katika kutoa elimu ya mahusiano ili kutengeneza kizazi chenye elewa zaidi
Uwepo wa huduma ya wanasaikolojia. kuongeza huduma na kuelimisha, na kutoa motisha kwa watu juu ya huduma ya saikolojia. Uwepo wa wanasaikolojia unahitajika kwa ukubwa sana kama huduma ya matibabu mengine. Hivyo serekali ifanye Juhudi kuzalisha wataalamu wengi wa saikolojia, kuweko vituo vyakutolea huduma za kisaikolojia na pia kuhamasisha kwenda kupata huduma hizo zinazo husiana na mahusiano na mapenzi.
Uwepo wa mahakama ya mahusiano. Katika nchi zilizo endelea tumeona uwepo wa mahakama za mahusiano zinazotumika kusuluhisha ugomvi wa mahusiano, kwa maana hiyo ipo haja ya sisi kuanzisha mahakama hizi kwa lengo kupunguza athari zitokanazo na uhalifu wa hisia

Upvote
9