Ongezeko la watu kunuka mdomo

Kingsharon92

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
7,843
Reaction score
10,321
Enzi zetu wakati tunasoma usafi ulizingatiwa mashuleni na walimu wetu mwanzo mwisho tulikaguliwa kuanzia meno kola ya shati kucha nywele yote hii kuhakikisha tunakuwa simart.

Ila siku hizi kuna ongezeko la vijana kutoa harufu mbaya kinywani unakuta mtu kavaa nadhifu kabisa ngoja akuongeleshe hii utafikiri mwaloni kirumba soko la dagaa halafu hata hawajishitukii sasa tuwaulize walimu na wazazi wa siku hizi hamkagui usafi kama enzi zetu?
 
Siku moja niko Tanesco igogo mwanza pale ofisini akaja mwana mama rika la kati kapendeza vizuri akaja nilipokaa akakaa akanisalimia akatoa makaratasi samahani mzee wangu nisaidie kusoma hii form sijui hata walivyonijazia aisee nilitamani kupiga chafya kwa kilugha ila nikaogopa uhamiaji si kwa harufu ile
 
Elimu ya kupiga mswaki ni muhimu sana hapo. mtu anapiga asubuhi mpaka kesho asubuhi na hamalizi hata dakika? kwanin mdomo usinuke?
 
Hili sio jukwaa husika kwa mada hii.
 
ubovu wa meno ni sababu kubwa sana ya hili tatizo.........ni vyema kumfanyia ziara ya kushtukiza daktari wa meno........wengi wana meno mabovu lakini hawajui........
 
Kuna visababishi vya kunuka mdomo vingi ambayo hata upigeje mswaki kwa baadhi ya watu haipunguzi arufu.
Cha muhimu kama una tatizo kama hili ni
Jiaidi mdomo wako usiwe mkavu
Kunywa maji mengi mara nyingi
Tafuna kistarabu bablish zenye harufu nzuri
Piga mswaki mara nyingi zaid na hasa wakat umemaliza kula
Toa maneno mazur kinywan mwako(iman yaeza ingia apa)
 
aina ya vyakula pia na vinywaji huchangia sana mdomo kunuka, pengine wengi harufu siyo ya mdomoni tu bali huanzia tumboni, hata akipiga mswaki harufu huondoka baada ya mda hurudi tena, wengine ni wangonjwa wa infections fulani kwenye kinywa na koo, ambazo bila kuzitibu harufu haiwezi kuisha, mswaki hautasaidia chochote
 
Mimi ni muislamu, kupiga mswaki ni sunna imesuniwa kupiga mswaki kila unapotaka kuchukua udhu, kusoma quraan, unapotoka kuamka n.k kuna hadithi nilisoma mtume anasema km ingekuwa amri yake angetufaradhishia umma wake kupiga mswaki kila muda wa kuchukua udhu.

Hadithi nyingine inasema “Lau si ugumu ambao Ummah wangu ungepata ningeweka ulazima wa kupiga mswaki kabla ya kila wudhuu”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…