Ongezeko la watu wanaoinyooshea kidole elimu ya Tanzania

Ongezeko la watu wanaoinyooshea kidole elimu ya Tanzania

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
245
Reaction score
457
Habarini.

Rejea kichwa cha habari hapo juu.

Kumekuwa na ongezeko la watu wanaopinga elimu yetu, wengi hoja yao kubwa ikiwa ni pesa. Madai ya baadhi ya hao watu ni ni kwamba ni heri mtoto amalize form form halafu akatafute maisha Kama kufanya biashara.

Mbaya zaidi baadhi ya hao watu ni wasomi wenyewe, utasikia wakikejeli "kikubwa pesa". Baadhi ya wasomi wameenda mbali zaidi kwa kuanza kuyapuuza masomo kwa kuendekeza starehe na mambo mengine bila kujitoa katika kujisomea.

Binafsi nakubaliana na suala la kutafuta pesa, lakini naamini swala la kujiongezea maarifa kupitia elimu yetu sio la kubeza. Mimi nilimaliza chuo miaka kama minne iliyopita na nilikuwa na bidii sana kwenye kusoma na kujiongezea maarifa kupitia vyanzo mbalimbali.

Matokeo yake ni kwamba nilipata uwezo kiakili wa kutafsiri mazingira yangu yanayonizunguka, kuwa uwezo mkubwa wa kutoa maoni na kujiamini kuchukua maamuzi ya haraka kwani niliifahamu michakato mingi ya kiuchumi, kijamii, kibiashara na kisiasa.

CASE STUDY.
Kuna kijana hapa Morogoro amemaliza form six, kijana huyu anaishi kwa mjomba ambaye amejaaliwa ukwasi. Mjomba wake amemwambia kuwa hatoenda chuo bali atampa mtaji akafanye biashara.

Ewe msomaji wa hii mada, unadhani pesa au ajira inapaswa kuonekana Kama kigezo tosha cha watu kupata elimu?? Unawashauri nini watu wenye mawazo haya??

Je, unadhani elimu ya form four au six inamtosha mtu kudevelop full intelligence potential??

Je, unamshauri nini kijana wa hapa Morogoro ambayo ameambiwa kutoenda chuo ili afanye biashara??

NAWASILISHA👍
 
Mbona jibu tayari unalo mwenyewe


"Binafsi nakubaliana na swala la kutafuta pesa, lakini naamini swala la kujiongezea maarifa kupitia elimu yetu sio la kubeza. Mimi nilimaliza chuo miaka"
 
Mbona jibu tayari unalo mwenyewe


"Binafsi nakubaliana na swala la kutafuta pesa, lakini naamini swala la kujiongezea maarifa kupitia elimu yetu sio la kubeza. Mimi nilimaliza chuo miaka"
Maoni yangu hayo, yakwako ni yapi??
 
Back
Top Bottom