kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Katika hotuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu mapitio ya serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka 2023/2024 amesema mikopo inayotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo imetoa shilingi bilioni 78.54 kwa wakulima 119,797 wanaojishughulisha na kilimo, mifugo na uvuvi.
Ongezeko la utoaji mikopo hiyo inachangiwa na kupungua kwa riba ya mikopo kati ya 17% hadi 20% hadi kufikia 9%. Wakulima wengi wanaweza kukopa na kuimarisha kilimo kwa kununua pembejeo na kuongeza eneo la kilimo. Serikali ya Rais Samia Suluhu imeadhimia kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na cha kibiashara.