Bishara za mtandaoni unaweza kufanya Tanzania.
#1. Ecommerce
Unauza bidhaa zinazo shikika kwenye tovuti yako, unacho takiwa nikuweka picha,bei na maelezo ya bidhaa. Shopify . Com na ecwid .com watakusaidia kutengeneza tovuti hii kwa wepesi utawalipa pesa kidogo. Wordpress .com/. Org itakusaidia kitengeneza kwa gharama ndogo.
Chakuzingatia
-kiswahili kitawale kwenye tovuti yako
-Uwe na utaratibu wa kutoa elimu kwa watanzania namna yakununua kwenye tovuti yako.
-Njia ya malipo iwe mobile money(asante kwa pesapal na direct pay)
-huduma kwa wateja
-delivery services.
Bishara hii inakuwa kwa kasi sana, watu wapo busy hawana muda wakuzunguka kufanya shopping na kadri siku zinavyozidi kwenda ndio watu wanazidi kuwa busy vibaya mno, wape fursa yakufanya shoping huku wamekaa.
Hizo sijui watanzania wengi hawa tumii mitandao, watanzania wanao tumia internet ni 23+ milioni, itazidi ongezeka kadri siku zinavyo kwenda.
Hii ni biashara ya sasahivi na pia ni biashara ya baadae.