Wadau najiuliza swali naomba mwenye jibu aniambie hivi nani anaelipa kodi kwa Serikali ya Tanzania mtumiaji wa hii mitandao au mmiliki wa hii mitandao.
Kwa mtazamo wangu nadhani kwa nchi kama Tanzania na nchi nyingi za Africa mtumiaji wa mitandao ndiye anayelipa kodi. Yaani mtu mmoja mmoja na makampuni ambayo yanatangaza kupitia hiyo mitandao kutokana na vifurushi vya data wanavyonunua pamoja na makato ya card za benki wanazotumia kulipia hayo matangazo katika hiyo mitandao.
Unajua kutokana na Revenue Model za haya makampuni ya Digital kunakuwa na challenge kubwa sana katika kuyatoza kodi kwakuwa wana njia nyingi za kugenerate mapato ambazo zinawawezesha kutoa huduma zao katika masoko ya nchi za kigeni bila ya kuwa na physical presence katika nchi husika.
Lakini pia kutokana na makubaliano ya kimataifa juu ya utozwaji kodi kwa hizi Multinational Companies, ni kwamba kampuni inatozwa kodi kule ambapo inaoperate shughuli zake na kuzalisha bidhaa au huduma zake na siyo kule ambapo huduma zake zinatumiwa.
Nadhani ungetafuta ripoti waliyotoa
Organization for Economic Cooperation and Development (OECD) mwaka 2015 kuhusiana na Challenges of Taxation of Digital Economy. Kwenye hiyo ripoti imeanisha maeneo matatu ambayo yanaifanya Digital Economy kuwa ngumu kutozwa kodi
Eneo la kwanza wanasema Ni rahisi kwa hizi digital companies kuuza huduma zake katika masoko ya nchi za kigeni bila ya kuwa na physical presence katika nchi husika.
Eneo la pili wanasema thamani ya hizi digital companies zimeegamia kwenye kumiliki mali zisizoshikika hususani Intellectual Property kama vile Brand Names, Patented Inventions, Trade secrets, Algorithms and Designs.
Eneo la tatu wanasema ni kutumika kwa watumiaji wa hayo makampuni kama sehemu ya kutengeneza thamani ya kampuni.
Dooo mimi siyo mchumi, nadhani wachumi watakuja kudadavua kwa kina.