Felixonfellix
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 1,672
- 183
1Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima
yangu,
sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
2ili uweze kutunza busara
na midomo yako ihifadhi maarifa.
3Kwa maana midomo ya mwanamke mzinzi
hudondosha asali,
na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko
mafuta,
4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,
mkali kama upanga ukatao kuwili.
5Miguu yake inakwenda kwenye kifo,
hatua zake zinaelekea moja kwa moja
kaburinia.
6Hafikiri juu ya njia ya uzima,
njia zake zimepotoka, lakini hana habari.
7Sasa basi wanangu, nisikilizeni,
msiache ninalowaambia.
8Njia zenu ziwe mbali naye,
msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine
na miaka yako kwa aliye mkatili,
10wageni wasije wakasherehekea utajiri wako
na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya
mwanaume mwingine.
11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa
uchungu,
wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12Utasema, Jinsi gani nilichukia marudi!
Jinsi gani moyo wangu ulivyodharau
maonyo!
13Sikuwatii walimu wangu
wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
a5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimuni.
14Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa
katikati ya kusanyiko lote.
15Kunywa maji kutoka kisima chako mwenyewe,
maji yanayotiririka kutoka kisima chako
mwenyewe.
16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara
za mji
na vijito vyako vya maji viwanjani?
17Na viwe vyako mwenyewe,
kamwe visishirikishwe wageni.
18Chemchemi yako na ibarikiwe
na ufurahie mke wa ujana wako.
19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri,
matiti yake na yakutosheleze siku zote,
nawe utekwe daima na upendo wake.
20Kwa nini mwanangu,utekwe na mwanamke
mzinzi?
Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa
mwanaume mwingine?
21Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele
za BWANA,
naye huyapima mapito yake yote.
22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa
yeye,
kamba za dhambi yake humkamata kwa
nguvu.
23Atakufa kwa kukosa maonyo,
akipotoshwa kwa upumbavu wake
mwenyewe.
yangu,
sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
2ili uweze kutunza busara
na midomo yako ihifadhi maarifa.
3Kwa maana midomo ya mwanamke mzinzi
hudondosha asali,
na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko
mafuta,
4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,
mkali kama upanga ukatao kuwili.
5Miguu yake inakwenda kwenye kifo,
hatua zake zinaelekea moja kwa moja
kaburinia.
6Hafikiri juu ya njia ya uzima,
njia zake zimepotoka, lakini hana habari.
7Sasa basi wanangu, nisikilizeni,
msiache ninalowaambia.
8Njia zenu ziwe mbali naye,
msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine
na miaka yako kwa aliye mkatili,
10wageni wasije wakasherehekea utajiri wako
na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya
mwanaume mwingine.
11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa
uchungu,
wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12Utasema, Jinsi gani nilichukia marudi!
Jinsi gani moyo wangu ulivyodharau
maonyo!
13Sikuwatii walimu wangu
wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
a5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimuni.
14Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa
katikati ya kusanyiko lote.
15Kunywa maji kutoka kisima chako mwenyewe,
maji yanayotiririka kutoka kisima chako
mwenyewe.
16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara
za mji
na vijito vyako vya maji viwanjani?
17Na viwe vyako mwenyewe,
kamwe visishirikishwe wageni.
18Chemchemi yako na ibarikiwe
na ufurahie mke wa ujana wako.
19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri,
matiti yake na yakutosheleze siku zote,
nawe utekwe daima na upendo wake.
20Kwa nini mwanangu,utekwe na mwanamke
mzinzi?
Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa
mwanaume mwingine?
21Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele
za BWANA,
naye huyapima mapito yake yote.
22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa
yeye,
kamba za dhambi yake humkamata kwa
nguvu.
23Atakufa kwa kukosa maonyo,
akipotoshwa kwa upumbavu wake
mwenyewe.