Onyo la kutokunywa pombe latolewa, watu kulikaribisha kwa "party"

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038


Watu wenye tabia ya kubeba makopo ya pombe ndani ya garimoshi za chini ya ardhi katika jiji la London, watasheherekea onyo lililotolewa na Meya wa London la kukataza tabia hiyo.

Wameamua kunywa usiku wa Jumamosi kukaribisha onyo hilo ambalo linaanza kutumika Jumapili,tarehe 7.

Watu zaidi ya 4,000 wamejiorodhesha katika orodha hio ya walevi ambao watakwenda na pombe zao katika treni inayopita njia iitwayo "circle line" ambayo kwa kawaida ni ya mzunguko katikati ya jiji la London au "Central London".

Meya mpya wa jiji la London bwana Boris Johnson ambe ni wa chama cha conservative ametimiza ahadi ya kutoa onyo hilo ili kuzuia tabia ya ajabu ya baadhi ya abiria kubeba pombe zao za makopo na kuwa wanakunywa kidogokodogo huku wakitoa maneno ya kejeli na matusi kwa abiria wengine.

Hii sijawahi kuona kabisa na kwa maana hio watu hawatatumia circle line siku ya Jumamosi jioni.

Je kuna yeyote ambae amepata kuona mambo haya ya ajabu mahali alipo ughaibuni?

Source: Evening Standard
 

Bwahahahaaaa....unajua sana mambo ya pombe wewe.....kwikwikwiiiiii
 
...

Je kuna yeyote ambae amepata kuona mambo haya ya ajabu mahali alipo ughaibuni?

Boris Johnson kaja na moto, lakini sidhani kama 'atayetaka' kuvunja sheria atashindwa!

...acha ughaibuni, bongo bwana... nilikuwanashangaa shangaa 'vijana' wengi wao wamekamata chupa za maji ya 'kilimanjaro' zile za 300ml, nikawa najisemea moyoni mnh, hawa jamaa wamegundua nini kunywa maji kwa wingi hivi, Kumbeee...!

si wamemimina Konyagi bwana ndani ya hizo chupa!

damn!...

sitashangaa 'wajanja' wachache wakaamua 'kumimina' hayo maji yao ya shaba kwenye chupa za juice, na bia inavyofanana na apple juice ndio kabisaa...


haitawezekana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…