Kulingana na takwimu za mwaka 2021, Zaidi ya 60% ya biashara mpya hufa ndani ya mwaka wa kwanza kwasababu tofauti tofauti. Ili biashara yako isiwe miongonni mwa biashara hizo ndio maana unahitahi hii elimu kwa ajiri ya kuandaa hesabu zako za mwaka 2024 kwa umakini. Ili kuepuka tatizo hili SOMA MPAKA mwisho wa Makala hii.
Acha kuweka mtaji wako hatarini kufirisika kwa kuandaa hesabu hatarishi kwa biashara yako.
Kila mwaka unapoandaa hesabu zako na kuziwasirisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vile vile na wao wanapata wasaha wa kuzikagua kama zimezingatia matakwa ya sheria za kodi. Kuna wakati majibu yanaporudi yanakuwa tofauti na matarajio ya mwenye biashara.
Ni kama bahati kwako, leo nakuletea Makala muhimu itakayo kupa mwongozo namna ya kuandaa hesabu zako za mwaka wa fedha 2024 ili kuepukana na madeni yatokanayo na ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika Makala hii ntakupitisha kwenye maeneo ambayo yamekuwa mwiba kwa wafanya biashara walio wengi. Wafanya biashara hao wamejikuta wakiwatuhumu TRA sababu ya madeni hayo, wakati wao ndo wamejisababishia matatizo hayo kwa kuandaa hesabu zisizo na uharisia wa biashara zao.
Kwa leo nakupitisha kwenye maeneo muhimu ili uandaapo hesabu zako uone kama upo kwenye njia sahihi au la!..
1. Mauzo kwenye EFD mashine dhidi ya mauzo kwenye hesabu (Financial statements)Hakikisha unapoandaa hesabu zako, mauzo ya kwenye mashine ya EFD yawe sawia na mauzo ambayo yataonekana kwenye hesabu zako. Pindi TRA watakapo fanya ukaguzi wa hesabu zako na kubaini tofauti kati hayo maeneo, hiyo tofauti itapigwa kodi 30% pamoja na riba juu yake. Vile vile kwa mjibu wa kifungu namba 86 (1) sheria ya usimamizi wa kodi, 2015 (Finance Bill 2024) utatozwa riba ya 20% ya thamani ya mzigo au huduma uliyotoa au Tshs 2,000,000 lakini isiyo zidi 20,000,000 na itachukuliwa ambayo ni kubwa kwa kosa la kutotumia EFD machine.
2. Mauzo ya marejesho ya VAT dhidi ya mauzo kwenye EFD machine
Kabla ya kuandaa hesabu zako za 2024, hakikisha unafanya ulinganifu (reconciliation) kati ya marejesho ya VAT pamoja na mauzo kwenye EFD. Mara nyingi tofauti inaweza kuchagizwa na risiti ambayo ulifuta kwenye marejesho ya VAT lakini haikufutwa kwenye mfumo ya EFD. Kumbuka ukishindwa bainisha tofauti hiyo TRA wataipiga 18% pamoja riba juu yake.
3. Mauzo ya hesabu (Financial statements) dhidi ya marejesho ya VAT
Hakikisha hesabu zako za mwaka 2024 utakazo ziandaa, mauzo ya hesabu yawe sawia na mauzo uliyo wasirisha kwenye marejesho ya VAT. Kama marejesho ya VAT ni ndogo itatafisiriwa kuwa kuna mauzo hukiingiza kwenye marejesho ya VAT hivyo tofauti itatozwa kodi ya 18% na faini juu yake.
4. Mauzo yasiyotolewa risiti lakini yanakatwa kodi ya zuio na wateja wako
Kuna wale wafanya biashara ambao wanahudumia taasisi za serikali au taasisi binafsi kwa kuuza bidhaa au kutoa huduma. Kwasababu zao wanazozijua huwa hawatoi risiti za kielekitoniki (EFD receipts) lakini pale wanapolipwa huwa wanakatwa kodi ya zuio (withholding tax). Kumbuka kuwa TRA watatumia taarifa za hiyo kodi ya zuio iliyokatwa kutambua kiasi cha mauzo yako ilikuwa kiasi gani. Ikibainika hujatoa risiti za mauzo kodi zifuatazo zitatozwa kwenye hayo mauzo ambayo hujatolea risiti, utatozwa VAT 18% kama umesajiliwa na VAT, 30% kama ushuru wa shirika (corporate tax), adhabu na riba pia.
5. Nyaraka zitokanazo na manunuzi ya mali za biashara
Kifungu namba 11 (2) sheria ya kodi ya mapato, 2004 inamtaka mfanya biashara kudai na kutoa risiti ya manunuzi au mauzo atakayo fanya. Mabadiriko ya kodi ya 2024 ya kifungu hicho hicho, inasisitiza kuwa ili manunuzi (expenses) yako yakubaliwe kupunguzwa kwenye mauzo lazima yaambatanishwe na risiti za EFD tofauti na hapo manunuzi yatakataliwa na TRA na kupigwa kodi ya 30% (corporate tax) pamoja na riba juu yake.
6. Kodi itokanayo na ajira (Employment tax)
Ikiwa kwenye hesabu zako umeonesha kuwa kuna hela ulilipa kama mishahara hakikisha kiasi husika umelipia PAYE na SDL (kwa SDL idadi ya wafanyakazi wawe 10 na zaidi). Vile vile hakikisha unafanya ulinganifu (reconciliation) kati ya namba utakazo onesha kwenye hesabu zako pamoja na zile ambazo zipo kwenye mfumo wa TRA (Taxpayer’s portal). Kwa mjibu wa kifungu namba 7 (2) sheria ya kodi ya mapato, 2004 kile apatacho mfanyakazi toka kwenye ajira yake inatakiwa kulipia kodi ikiwa mshahara wake unaanzia Tshs 270,000 tofauti na hapo hatalipia kodi.
7. Kodi ya zuio (Withholding tax)
Endapo kwenye hesabu zako umeonesha kuwa kuna watoa huduma uliwalipa kwa mwaka wa fedha 2024, mfano wa huduma ni kama ukaguzi (audit), ushauri wa kodi, ushauri wa kisheria, ulinzi, na huduma nyingine hakikisha kwenye malipo hayo unakata 5% bila VAT. Vile vile kama kwenye hesabu umeonesha gharama ya kupanga ofisi hakikisha umelipia kodi ya zuio ambayo ni 10% ya gharama ya pango. Hii ni kwa mjibu wa kifungu namba 83 sheria ya kodi ya mapato sambamba na paragraph ya 4 ya kipengele kikuu (First schedule). Bila kusahau kulipia 1% kama stamp duty ya mkataba.
8. Gharama ya usimamizi (Management fees)
Katika shughuli za kibiashara kuna wale wakurugenzi (Non-executive directors) ambao hawashiriki kwenye shughuli za kila siku za kampuni, ambapo kampuni inaamua kuwalipa gharama za usimamizi. Endapo kwenye hesabu zako kuna gharama za namna hii hakikisha umelipia kodi ya zuio ambayo ni 15% ya gharama zote.
9. Taarifa ya fedha (Statement of Cash flow)
Wakati wa uandaaji wa hesabu zako za mwaka 2024 hakikisha uandaapo taarifa ya fedha tumia ile report ifahamikayo kama direct method. Nachelea kushauri hivyo kwasababu wakati wa ukaguzi wa hesabu zako utakaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, kuna njia moja ya ukaguzi wanafanya kitaalamu inaitwa cash control analysis. Njia hii imeacha kilio kikubwa kwa wafanya biashara walio wengi. Sasa ili kuepuka au kupunguza changamoto hii ni vyema ukatumia njia ya direct method katika kuandaa taarifa ya fedha.
10. Amana ya malipo (Commission was paid to…)
Kuna biashara ambazo mwenye biashara anapata wateja kutoka kwa watu wengine, watu hao hao wanaompa kazi anawalipa amana (commission) kulingana na kazi wanazoleta. Katika biashara zako kama umefanya malipo ya aina hii, baada ya kuandaa hesabu zako hakikisha unalipia 10% kama kodi ya zuio. Usipofanya hivyo utalipishwa kiasi kikuu na riba juu yake kipindi Mamlaka ya Mapato Tanzania itakapo fanya ukaguzi wa hesabu zako.
Haya ni baadhi ya maeneo ambayo huwasumbua wafanya biashara pindi wanapoandaa hesabu za biashara zao. Hivyo basi wakati wa kuandaa hesabu zako za 2024 hakikisha haya maeneo yaliyoanishwa hapa juu unayapa kipaumbele. Kumbuka yapo maeneo mengi sana hayajaongelewa hapo juu ambayo kama mfanya biashara unatakiwa kuzingatia matakwa ya sheria ya kodi.
Oooohh!… kabla sijasahau….
Unaweza kutuchagua kuwa wakaguzi (auditors) wako wa hesabu zako za 2024
Ili kupata huduma hii tuma ujumbe sasa hivi kwenda 0752187434 au info@halaconsultants.co.tz.
Tuma ujumbe huo ndani ya saa 24 ili uwekwe kwenye mpango kazi wa wateja wetu, nje ya muda huo tutakuwa tumefunga dirisha la kupokea wateja wapya.
HALA Consultants, Certified Public Accountant
info@halaconsultants.co.tz
0752 187 434