Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Mcheza Soka na mshindi wa Kombe la Dunia 1986 wa Argentina, Diego Maradona yupo chini ya uangalizi wa Madaktari kufuatia Oparesheni aliyofanyiwa ili kutibu tatizo la kuganda kwa Damu kwenye Ubongo wake.
Nguli huyo wa Mchezo wa Soka atatumia takribani wiki moja kwenye Zahanati binafsi baada ya matibabu yaliyofanyika ili kutibu Bonge la Damu iliyoganda kwenye Tishu (Hematoma) ambayo inaelezwa kusababishwa na Majeraha kichwani.
“Niliweza kuondoa Bonge la Damu iliyoganda kwenye tishu kwa mafanikio na Diego aliweza kuvumilia Oparesheni” Alisema Leopoldo Luque, Daktari wa Upasuaji ambaye pia ni Daktari binafsi wa Maradona.
Dkt. Luque ameongeza kuwa Maradona ambaye amekuwa akipambana na Uraibu wa Pombe na Madawa pamoja na matatizo mengine ya afya, pia anasumbuliwa na Msongo wa mawazo.
Binti wa Maradona, Dalma ambaye alimtembelea hospital siku ya Jumanne ya tarehe 3 Novemba 2020 baada ya kipimo cha CT Scan kuthibitisha uwepo wa mgando wa Damu kwenye ubongo wake, aliwashukuru wafuasi wake waliokusanyika nje ya Zahanati wakishangilia huku wakitaja jina ‘Diego’.