Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Urusi pamoja na mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani (OPEC) yamekubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta kwa takribani mapipa milioni 10 kwa siku ili kuidhibiti bei iliyoporomka kutokana na janga la kirusi cha corona na vita.
Punguzo hilo, ambalo liliafikiwa kwenye mkutano wa jana wa mataifa hayo ni sawa na asilimia 10 ya kiwango cha kawaida, ingawa katika uhalisia linaweza kufikia hadi asilimia 20.
Saudi Arabia inasema huenda punguzo hilo likakata uzalishaji wa mapipa milioni 12.5 kwa siku, kwa sababu ya kiwango kikubwa cha uzalishaji kutoka nchi hiyo, Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu. Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya siku nne za mazungumzo.
Mazungumzo ya awali juu ya uzalishaji wa mafuta duniani yalikuwa yamekwama kutokana na mzozo na Mexico, lakini ufumbuzi ulipatikana baada ya mataifa wanachama wa OPEC kuliruhusu taifa hilo la Amerika Kusini kupunguza mapipa 100,000 tu kwa mwezi.