OpenAI imezindua
ChatGPT Atlas, browser ya
akili mnemba itakayofanya kazi kwa ukaribu na chatbot maarufu ya ChatGPT, suala linalotarajiwa kuleta muelekeo mpya dhidi ya utawala wa
Google Chrome.
Uzinduzi huu ni hatua nyingine ya OpenAI ya kutaka kunufaika kupitia watumiaji
milioni 800 wanaotumia ChatGPT kila wiki, huku ikilenga kupanua wigo zaidi katika maisha ya kila siku ya watumiaji wa mtandao.
Open AI wananafasi nzuri ya katika hili kutokana na uzoefu walioputa pamoja utajiri wa taarifa za watu walizovuna juu ya za matumizi ya akili mnemba na namna watu hutumia browsers.
View attachment 3491883
Ujuio wa
ChatGPT Atlas unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika utafutaji wa taarifa mitandaoni unaosaidiwa na AI, hii ni kutokana na namna watumiaji watakavyogeukia
matumizi ya kujibizana (Conversation) badala ya majibu ya kawaida ambayo hayatoi nafasi ya kujadili matokeo ya ulichokuwa unakitafuta. Utafutaji kwa njia ya majibizano ni moja ya njia mpya zenye ufanisi sana ambazo kwasasa zinazotumiwa na browser ya
Google Chrome iliyounganishwa na akili mnemba ya
Gemini, Utafutaji huu husiadia kupunguza mlundikano wa matokeo ya utafutaji na kuleletea majibu yanayo karibia muktadha wa kile ulichokuwa unakitafuta. Kitu ambacho watu wengi wameona kinamsaada kwa kuwa hakuhitaji mtumiaji awe na uelewa wa ndani juu ya kile anachokitafuta..
Ujio wa Atlas unaenda kuongeza ushindani kati ya
OpenAI na
Google, hili limeaonekana wazi siku ya jana, kwani baada ya uzinduzi wa Atlas, hisa za Kampuni ya Alphabet zilishuka kwa
asilimia 1.8.
Atlas inazinduliwa kipindi ambacho kuna mfumuko wa Browser za AI kama vile,
Perplexity Comet,
Miscrosft Edge,
Brave browser na
Opera Neon.
Wasiwasi unakuja juu ya madhara ya ongezeko la Akili Mnemba kuunganishwa moja kwa moja katika mifumo ya kompyuta inayochakata taarifa binafsi.
Wakuu, matumizi ya AI kuunganishwa katika browser na mifumo ya komptuta yana mijadala hasi sana.
Makundi yanayofanya uraghbishi juu ya masuala
usalama wa taarifa binafsi wanadhani Matumizi ya AI yanaweza kabisa kuondoa lengo la Msingi la njia za ulinzi kama vile
Msimbo wa Mwisho na Mwisho End to End Encryption, Hii ni kwakuwa Akili Mnemba
zinaweza kutumia taarifa hizo kabla hazijawa encrypted kipindi inakusaidia kundika au kujadili na kwakuwa AI hazichakati taarifa hizo kwenye Kompyuta za watumiaji bali kwenye data center na kwenye makao makuu yake swali linaibuka juu ya usalama wa taarifa za watu.
Pia maoni mengine hasi juu ya matumizi ya Akili mnemba katika browsers ni suala la
kunyima mapato kwa wamiliki wa tovuti mbalimbali, kwani utafutaji unaosaidiwa na AI hauhitaji mtu kutembelea tovuti husika kwakuwa Ai inafanya jukumu hilo na hivyo kupunguza watembeleaji wa Tovuti zenye vyanzo vya taarifa ambazo watumiaji wanazitafuata hivi kupunguza uwezekano wa kupata mtangazo.
openai.com
Mabadiliko huwa yanakuja na faida lukuki ila kunawakati huwa yanatabia yakuchukua sehemu ya uhuru wetu. Wakuu, niwatakie siku njema.