Salamu kwa wote.........
Jamani eti hizi open marriages za wenzetu wazungu je kuna uwezekano kuwa wanatekeleza ule msemo wetu wa Mapenzi ni maua popote huchanua? hata kwa mtu ambaye ameoa au kuolewa?.
Kwa maana ya kuwa kuolewa au kuoa si mwisho wa kupenda? Je kuna ukweli katika msemo huu na kama ni ndio vipi sisi ambao hatufuati taratibu hizi za open marriages au ndoa za mikataba, tunawezasema tunaishi kinafiki kwa kupingana na hali halisi au?
Nazungumzia hizi ndoa za "Nitakuwa mwaminifu kwako Mpaka kifo kitutenganishe"
...ofcourse, kuoa na kuolewa si mwisho wa kupenda,..lakini ndoa kama (mfano) ilivyo Kufunga, iwe swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, au Kwaresma,...au funga yeyote ile, lengo nia na madhumuni yake ni kujizuilia nje ya mipaka ya Nia uliyoweka.
Kama umefunga Kwaresma, na ukaambiwa jizuilie vitu unavyovipenda, ama Nyama, Maziwa, Jibini na siagi... halafu katikati ya funga wewe ukala au kunywa hayo maana yake ushabatilisha funga yako na maana ya tendo hilo.
Sawa sawa na waislamu akiamua kwa makusudi kula au kunywa katikati ya mchana wa funga yake ya Ramadhani...atakuwa keshafungulia!
Ndoa ni hivyo hivyo,... kuoa maana yake 'kujifunga' na matamanio, hata kama utapenda, kutamani, au kushikwa na uchu kiasi gani... Jifungie tu humo humo kwenye ndoa, Open marriages zinaondoa maana kamili ya neno
'Marriage'.
sijui wengine mwalionaje hili...