Open spaces and their cost to our lives

Open spaces and their cost to our lives

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
28,186
Reaction score
15,549
Wajameni!!!

Nimehamia sehemu moja hapa wilaya ya kinondoni ni pazuri sana!!! Kinachonisikitisha ni namna ambavyo mbele ya nyumba yangu kuna open space lakini kuna jamaa (wala haishi hapa) amefungua karakana ya cerpentry na watu wa welding, pia ameweka mgahawa na vitu kadha wa kadha

Hakuna choo wala vyoo, muziki ni mpaka basi lakini kila ninapofuatilia serikalini, tena hasa baana ya mkuu wa wilaya kuahidi kuondoa biashara sehemu zisizo rasmi, naambiwa tena na wakuu wa pale kwamba waondoke waende wapi? subiri uchaguzi nk.

Ombi langu kwenu ni ushauri wa kitalaam hasa kwennye rights zangu, financial implication kama naruhusiwa kushitaki au kudai fidia, haki ya wale wanaofanya biashara na uingizaji wa siasa kwenye mambo yaliyo serious

Nimeileta huku kwani naona it had to be dealth professionally kuliko kisiasa

I need you help
 
bongo hiyo bwana mkubwa!😀😀
itabidi uzoee
 
Huu ni ushahidi tosha juu ya maisha yetu na namna tunavyovuruga utaratibu halafu tunakuwa wa kwanza kulalamika mambo ysipoenda sawa. watanzania tumekuwa wa kwanza kulaumu kila mtu but ourselves... ukiuliza sasa hivi ni wangapi wanafuata taratibu za makazi, utaambiwa ni less than 20%. hii haiishii hapa, ni muendelezo kila sehemu, lakini cha kusikitisha the very same pipo tumemlaumu rais kwa kwenda kufungua hoteli iliyojengwa barabarani lakini haya yote yanaanzia mitaani kwetu

Eniwei, its another cost of corruption
 
Inaonekana huyo jamaa kavamia eneo hilo, aidha kuna mkono wa serikali ya mtaa ama halmashauri ya jiji, kwani maeneo wazi yanalindwa vizuri na sheria za mipango mji.

Cha msingi ni kuendelea kuwabana hao jamaa wa Halmashauri, kwani Mkuu wa Wilaya atabase zaidi kisiasa. Zaidi jaribu kuangalia ramani ya eneo hilo ili kuweza kujenga hoja ya nguvu ya kubadilishwa kwa matumizi ya eneo.
 
Thanks Kibs, kwakweli ni vigumu kuamini unayosema kwasababu ramani na kila kitu kipo wazi... sanasana ukizidi kuwauliza utaambiwa barua imepotea, au unataka vita nk.

The moral of my post ni kwamba tunahitaji ku-create awareness ya matumizi bora ya ardhi kabla hatujafunguka zaidi kiupeo kwani watakaoumia siku ya mwisho ni maskini na wale abusers wa sheria wanaendelea ahat kubadili mipaka ya miji na mipango miji kwa ujumla kwa sababu zao
 
ulaji wa madiwani mara zote huwa kwenye maeneo kama hayo, huo ni ulaji tu, mamlaka zinaona anafanya nini lakini hawana muda, ni swala la kutafuna mpaka kieleweke. pole kijana
 
Cha msingi ni kuendelea kuwabana hao jamaa wa Halmashauri, kwani Mkuu wa Wilaya atabase zaidi kisiasa. Zaidi jaribu kuangalia ramani ya eneo hilo ili kuweza kujenga hoja ya nguvu ya kubadilishwa kwa matumizi ya eneo.
wakuu wa wilaya wenyewe hawa makada waliofeli maisha na genge la wanajeshi wastaafu, sioni muwajibikaji zaidi ya walaji na genge la mafisadi.
 
Huu utaratibu wa kuvamia open spaces uliasisiwa na CCM! Sehemu nyingi zilizokuwa zimetengwa kama open spaces zilivamiwa na CCM na kuanza kufanywa vitega uchumi vya hao mafisadi kama vile maegesho, kumbi za starehe, maduka, bar n.k.
Utamaduni wa bustani Nhi hii haupo! Angalia pale Mnazi mmoja ni kinyaa tupu!
Tunakaribia Miaka 50 ya uhuru lakini ni porojo tu zinazotawala! Tumeshindwa hata kupanda maua. angalia pale Forodhani Zanzibar mpaka Aga Khan kaja kutupandia maua!(shame!)
Huyu anayaeitwa meya Wa jiji Bw Kimbisa anachojua ni kutembea na gari inayapeperusha bendera ya meya lakini haoni hata aibu mandhari ya Dar inavyotia kinyaa! Yaani tuseme na eposure yake yote kashindwa kuiga ha suala moja la kuboresha mji pamoja na vyanzo vyote vya mapato alivyonavyo?
Tunahitaji mabadiliko sasa ili tuweze kusonga mbele
 
Is there any way hizi open spaces zitaweza kufunguliwa tena? au ndio bye bye?
 
ukweli ni kwamba mameya ni viongozi ceremonial tu... ninaamini kabisa solution iko kwa watendaji kwani wana nguvu sana ila wamekua sidelined kwenye maamuzi ya ulaji
 
Back
Top Bottom