Open University acheni kufanya watu wajinga

Open University acheni kufanya watu wajinga

Nansawa

Senior Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
190
Reaction score
30
Hii ni maalum kwa Mwl wa OAF 112: Management Mathematics and Statistics. Kwanza yeye mwenyewe au pamoja na moderator wa maswali km yupo hawako makini na wanachotunga. Hali inayoleta wasiwasi km hata usahihishaji uko sawasawa. Sio kwamba hesabu ni tatizo la kitaifa, nakataa mbona vyuo vingine haiko hivi. Mtunzi analeta swali la linear programming haleti graph paper, analeta hesabu za compounding haweki interest rate, mwisho wa siku anasahihisha anaweka zero mark. Huu ni ushenzi, tena unashangaa msimamizi unamwambia graph paper anakuambia we chora tu ataona idea yako, this is nonsense, ataona wapi idea hizo points nazikadiriaje? Mnatuchelewesha kumaliza kwa wakati. Km mtu mtihani anatunga vibaya tuna hakika gani anasahihisha sawasawa? Acheni kufanya watu hawana akili hii inakuwa km mitihani ya CPA, kuwa wanatakiwa watu kadhaa kwa mwaka fulani basi. Hesabu za set nazo ni hesabu za kumshinda mtu. Mwl jipange ili tuone usomi wako sio kucheza na maisha ya watu kwa kufelisha kwa kisingizio watu hawajui hesabu. Yawezekana hata wewe pia hujui bwana.
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Lakini mngeweza kumshitaki hata kwa dean wa faculty labda ingeweza kusaidia mnaenda kabisa na ushahidi na kama asipowasaidia basi mnasogea hata kwa Dvc(Academic) inaweza ikawa msaada....huo ni mtazamo wangu tu...
 
Back
Top Bottom