Operation Barracuda: "Mission hatari ya kijasusi nchini Kongo"

Hongera kwa mwandishi maana Ngoma ni ndefu aisee, baada ya kusoma naomba nitoe maoni yangu juu ya hii Operation iliyochukua uhai wa shujaa wa Congo na Africa kwa ujumla

Sijaelewa sehemu moja, sa sijui walitaka tu kuifanya iwe operation ya kuvutia au vipi, Yani mateka mnao nyie, mnawapeleka msituni na kuwafunga kamba kwenye miti Kisha utekelezwaji wa mauaji ufanyike na maofisa wa marekani, waliosafiri kwa Siri sana kutoka Kenya

Kisha miili ya marehemu inazikwa na badae kufukuliwa na kuwekwa kwenye Acid, mbona kama me naona Kulikuwa hakuna haja ya kusubiri wauwaji watoke Kenya, Tena ni snipers, yani waje walenge binadamu waliofungwa kwenye miti.....?

Sijaona umuhimu wa hao Snipers kwenda kufanya mauaji ya kitoto kiasi hicho Kongo, laiti kama Lumumba na marafiki zake wangeachiwa huru na hawa snipers kufanya kazi yao kwa kuwavizia wakiwa matembezini au makwao hapo ingeleta mashiko

Leo hii Mh Mbowe anashikiliwa kwa mashtaka ya ugaidi, mfano serikali iamue auawe, alafu imchukue na kumpeleka msitu wa mabwepande na isubiri wauwaji watoke watoke Cameroon ambao wamekuja kwa kujificha ficha hadi msituni wafanye kazi yao Kisha maiti ilowekwe kwenye Acid

Sasa kuna haja gani ya kuzunguka kote huko ilhali wangeweza kumuuwa wao wenyewe na kumweka kwenye Acid na story ikawa imeishia hapo, maana ata iweje itajulikana nyie ndio mmehusika kwenye mauaji yake au kupotea kwake maana mara ya mwisho inajulikana nyie ndio mlikuwa nae enzi za uhai wake

All in all hongera mwandishi kwa kushea nasi hii story juu ya shujaa wa Africa
 
Asante sana kiongozi....
 
Kuna barua Lumumba alimwandikia mkewe inabidi niitafute kwanza,niliikopi sehemu na kuiwekw kwenye mfumo wa pdf. Mleta uzi naomba utuletee na uzi wa kuundwa kwa Taifa la Saudi Arabia chini ya Chifu Al Saudi wa Riyadhi
 
This is Africa. Ambapo kumejaa kusalitiana kwa hisani za wazungu
 
Asante mkuu kwa andiko zuri. Kuna kitu kimoja nadhani inabidi ukifanyie revision. Unamtaja hapa John Foster Dulles kuwa alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani na alishiriki katika Operation Barracuda. Lakini sidhani kama hilo ni sahihi. Ni kweli kuwa John Dulles alishika wadhifa huo lakini alifariki mwaka 1959 wakati Operation Barracuda ilikuwa active mwaka 1960 hadi mwanzoni mwa 1961 wakati Patrice Lumumba alipouawa.
 
Ukisoma "HEART OF DARKNESS" kila kitu kilichoandikwa humu utakikuta. Huyu jamaa alijitahidi Sana, kutafsiri novel nzima sio mchezo.
Kitabu cha Heart of Darkness kimetoka karne ya 19 hata kabla Lumumba hajazaliwa. Mleta mada amezungumzia mambo yaliyotokea karne ya 20 hasa hasa kuhusu maisha ya Lumumba. Unawezaje kusema kuwa mleta mada ametafsiri kitabu hicho!
 
Usaliti mkubwa unatokaga ndani ya himaya yako. Laiti kama mobutu asingekua mbegu ya usaliti ndani ya kambi ya lumumba labda historia ingeandikwa tofauti leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…