Operation Katiba ichukue nafasi ya Operation Sangara

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
302
Nguvu zile zile na ari ile ile kwa kasi ile ile ya Operation Sangara iliyotumika kuhamasisha wananchi kujua haki na wajibu wao, sambamba na kufanya mabadiliko ya mfumo wa utawala, sasa itumike kuhamasisha wananchi hao hao umuhimu wa kuwa na katiba mpya kupitia slogan ya 'Operation Katiba'.

Suala la katiba lichukuliwe kwa mapana yake lisije likaonekana ni suala la viongozi au watu wachache tukarudia makosa ya zamani ya kutoshirikisha wananchi na kujikuta tunaanza kutia viraka baada ya kipindi kifupi, tuwapelekee wenye nyumba ambao ni wananchi.

Naamini kabisa kwa kutumia slogan hii mpya baada ya miezi sita watu watakuwa wamehamasika na kuwa na uelewa mpana wa nini umuhimu wa kuwa na katiba mpya, mbona Operation Sangara ilifanikiwa.

Napendekeza jina hilo kwa vile limebeba ujumbe ulio wazi kabisa unaotakiwa kufikishwa kwa walengwa kwa vile neno lake ni simple and easy to remember, 'OPERATION KATIBA'

Naomba kuwasilisha.
 
Operation Katiba na Operation Sangara ziende sambamba, zote ni muhimu. Sasa hivi CHADEMA ina timu kubwa ya wabunge, wapeane majukumu. Mwendo mdundo!
 

Naunga Mkono saaa ... na
 

I like your points. Nawaomba uongozi wa juu wa CHEDEMA, walichukue hili na kulifanyia kazi.
 
Operation Katiba na Operation Sangara ziende sambamba, zote ni muhimu. Sasa hivi CHADEMA ina timu kubwa ya wabunge, wapeane majukumu. Mwendo mdundo!
Huu ni ujumbe toka kwa Slaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…