Operation OKOA YANGA Sehemu ya kwanza 1

Operation OKOA YANGA Sehemu ya kwanza 1

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
Tumevunja benchi la Ufundi Sawa. Kongole kwa uongozi na Wadhamini na wafadhili wetu GSM kwa uamuzi huu maana tuliona timu ilikosa kabisa ari ya uchezaji haikuwa na mbinu wala maarifa ya ziada na hata utimamu (Fitness) ya wachezaji ni haba.

Kuwafukuza makocha ni sehemu ya kutibu tatizo la wazi ambalo linaonekana Uwanjani mbele ya macho ya watu wengi, lakini kuna shida nyingine ya kutatua ili Kuiokoa Yanga yetu, katika mfululizo wa Makala hizi nitaainisha matatizo ambayo tunayafuga na yanatuyumbisha ndani ya Yanga yetu.

Tatizo 1
KARIGO GODSON

Huyu ndio shida kubwa kwa sasa ndani ya Yanga, ameingia kwa kupitia mgongo wa mdhamini wetu GSM na kupewa madaraka ambayo yanampa nguvu kubwa na kwa kuwa ametoka upande wa Tajiri basi anadharau kila kitu cha Makao Makuu.

KARIGO kwa sasa anatumia nafasi yake kuuangusha uongozi wa Mwenyekiti Dkt. Msolla ambao yeye hakuwa anautaka, kwani yeye alikuwa ni Kambi ya IGANGULA. Hivyo basi anatumia nafasi aliyopewa na GSM kuuvuruga uongozi wa Msolla bila kujua kwamba anaiyumbisha Yanga na kwa kiasi kikubwa matokeo haya anayafurahia kwa sababu watu watauchukia Uongozi zaidi kuliko GSM na yeye KARIGO atafanikisha mpango wake lakini hadi hilo lifanikiwe je Yanga na WanaYanga watakuwa imeumia kiasi gani?

ITAENDELEA..

#SisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm[emoji1241]

PIA SOMA: Operation OKOA YANGA SEHEMU YA PILI - 2
 
Uto bana,
Si Ungeendelea tu hapa hapa?
 
Duh tatizo n huo mwiko nyuma usimsingizie karigo siku tukiutoa huo mwiko yanga itasonga mbele

Nb msinifikirie vibaya sio mwiko wa ugali naouzungumzia hapa
 
nimewaona yanga na basi lao wakipita bagamoyo road sijui wanaenda wapi?
 
Bro itakua cku iz ule mchongo wa jezi aupigi!
Yaan wanaangaika sana

Sidhani kama anaelewa kuwa Mgazija ni mwajiliwa wa serikali, daktari wa Temeke.

Ila Mchakato wa mfumo ukamilike mapema mwekezaji akabidhiwe timu, haya hatutayasikia tena
 
Back
Top Bottom