Operesheni ya uzai ya kupangwa(Elective Caesarean section) ni upasuaji ambao huwa umepangwa kabla ya uchungu kuanza,hivyo huwa hakuna dharura.Ziposababu nyingi za kufanya Elective C/S ambazo ni za kidaktari na nyingine ni binafsi(mgonjwa anaomba mwenyewe),This is a common occurence in developed world.Siku hizi pia wapo wanaoomba Elective C/S kama njia ya kupunguza uwezekano wa mama mwenye VVU kumwambukiza mwanae wakati wa kuzaliwa (C/S reduces chances of transmission of HIV by 50%)
Tukija kwenye swali lako;jibu langu halitakuwa la moja kwa moja,kuna mambo kadhaa ya kutizama:-
Uwezo wa akili wa mtu huchangiwa pia na vinasaba(genes )za wazazi wake.
Pia Uwezo huo huchangiwa na mazingira anayokulia mtoto n:k
Inaweza kutokea wakati wa kujifungua mtoto akapata kitu kinaitwa BIRTH ASPHYXIA hii kwa lugha rahisi ni kuwa mtoto anachelewa kulia baada ya kuzaliwa(meaning alishindwa kupumua vizuri na hivyo ubongo kukosa hewa).Brain damage katika umri mdogo wa mtoto huwa ni permanent hivyo huweza kusababisha utaahira (degree of severity hutofautiana kutoka kkuwa na uwezo mdogo darasani mpaka wale wanaoshindwa kujimudu kabisa)
Zababu za mtoto kushindwa kupumua imeadiately baada ya kuzaliwa ni nyingi ikiwemo prolonged Obstructed labour (kama ulivyosema nyonga ndogo nk),Mtoto kulala vibaya (breech presentation) na nyinginezo
Conclusion:Hakuna ukweli kuwa watoto waliozaliwa kwa elective C/S wana akili zaidi ya wale waliozaliwa kawaida