Operation za kusajili line kupitia NIN na changamoto zake

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Habari za maandalizi ya sikukuu ya X-mass wakuu na kuukaribisha mwaka mpya 2020, tumwombe mungu atuvushe katika hili..

Kama mnavyojua kuwa serikali kupitia mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kushirikiana na mitandao ya simu wametangaza kuwa tar 31 Disember hii kuwa line zote zisizosajiriwa kwa alama za vidole zitafungiwa.
Hivyo kutokana na kubaki kwa Siku chache kuelekea Siku ya kuzimwa line kumekuwa na adha kubwa sana katika mchakato wa hili zoezi.
Mfano, huku niliko mim
1. Ni mji mdogo na naweza kusema kuwa una mawakala wachache wa kusajili hzi line. Kama haitoshi, vitongoji/vijiji mbalimbali hutegemea mji huu kuja kusajiri line zao.
Hali hii husabanisha foleni kubwa sana (Mfano Jana nililitumia mda mwingi hadi kuja kusajiri line yangu kutokana na foleni ya watu.

2. Tozo/Gharama za usajili.
Hii imekuwa kero nyingine kwa mda huu wa lala salama (kama Mimi Jana nimetozwa tozo kwa ajili ya usajili wa line hali ya kuwa toka hii operation imeanza ilikuwa na free kabisa)

3. kutokuwepo na vituo/mawakala kwa baadhi ya mitandao ya simu, (mfano TTCL).
Jana nilishanga, ety mji nzima hakuna wakala yeyote anayesajiri line za TTCL.. Sasa inanilazoma nisafiri hadi mkoani nikafanye hii kitu hali ya kuwa zimebaki Siku chache.

Hivyo, hizo ni challenge kuu zinazoziona ktk kuelekea mwshoni mwa hii operation.
So niwaombe TCRA & Mitandao ya sim kwa ujumla waliangalie hili na wajaribu kuongeza mda kidogo wa hii operation. Pia TTCL waongeze vitu vya uasiji kwa hii miji midgo .. Maana nilichokia observe jana ni kuwa watu wengi/kibao hawajafanikiwa kusajiri line zao kwa alama za vidole.

Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…