Operesheni Ondoa CCM 2025 inanze sasa

Operesheni Ondoa CCM 2025 inanze sasa

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ndugu zangu wapinzani nawaomba tuweke itikadi zetu mfukoni na tuendeshe Operesheni Ondoa CCM 2025.

Katika operesheni hii siyo mbumbumbu kuzunguka wakiwatangazia watu ondoa ccm 2025 bali ni kwetu sisi kutazama ili tuwaondoe hawa tunahitaji kufanya nini?

mkakati uko hivi

1. Tutazame makundi ya kijamii yaliyoachwa na tuandae sera bora za kuwakomboa ifikapo kampeni za 2025.

2. Ni mwiko kuikamata serikali na dola ndevu kwa sasa, tunahitaji kufanya siasa za kistaarabu tukiwapa watu wengi zaidi popularity. tusiganganie kutumia watu wetu wachache kuitunishia serikali iliyopo madarakani misuli

3. Tuachane na uanaharakati na tuchukue sera zinazogusa watu wengi.

4. 2025 tunahitaji watu strong ambao wakati upande wa pili watakapokuwa wakigombania nyama kwenye mchuzi sisi tutakuwa tukiwaahidi waliokosa ajira kupata ajira, waliokosa fursa za biashara maisha bora, waliokosa kuuza mazao ya kilimo tutakuwa tunawaahidi soko.

Nikichungulia kwenye kambi ya upande wa pili naona kabisa mgawanyiko wa kambi ni nje nje na ni fursa nzuri sana iwapo tutajipanga vizuri.

Tofauti zetu zisiwatishe na kila chama kijitolee kwa mwaka huo kufunika mambo mengi ilimradi siasa zibalansi.

Hakuna Mtanzania anayeweza kushangilia kila mwaka watu walewale wanaingia madarakani kama hakuna direct link ya ubora au unafuu anaoupata yeye katika maisha.
 
Sawa,CCM wameshawasikia na watalifanyia kazi.
Wakati ni huu.
 
Haiwezi kuanza sasa kwani ligaidi bado linasota mahabusu. Makamanda uchwara wamesambaratika kwa fedheha.
 
Bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi hakuna la maana.
Acha fikra za kujikwamisha.

2025 ni mwaka wa fursa kwa maana ile kambi lazima wavutane na vita ya pazi ndiyo fursa kwa kunguru
 
Mkuu labda jeshi litake vinginevyo kwa Tz regime change bado sana. Watz walio wengi hawataki kubeba gharama ya mabadiliko kwa hiyo sahau mabadiliko ya kiuongozi kutokea.
 
Shetani hafukuzwi kwa mapambio....
Kweli tusijidanganye, ili kumtoa shetani ni lazima akemewe. “Makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.”—MATHAYO 7:28, 29.
 
Mkuu labda jeshi litake vinginevyo kwa Tz regime change bado sana. Watz walio wengi hawataki kubeba gharama ya mabadiliko kwa hiyo sahau mabadiliko ya kiuongozi kutokea.
Achana na fikra za jeshi.

watanzania hawabebi ajenda za mabadiriko bali ajenga zinabebwa na hoja mnazoibuka nazo.

ni wakati sasa kukaa chini na kujiuliza hawa vijana wanaomaliza shule hawana ajira tutafanya nini kuwapatia ajira na siyo kusema tu nitawapa ajira lakini wakikutazama usoni huna mpango hata mmoja wa ajira.

hivyo tufanye kazi ya ziada kujua changamoto za watanzania na kutolala tukibuni majibu.

tukifanya hayo ndiyo tume huru, hayo ndiyo chachu ya watanzania kupenda mabadiriko
 
Vijana wengi wa kitanzania akili zetu zimeganda
Ili ccm itoke madarakani tunatakiwa sisi vijana tujitambue kwanza
Tuache kuwa wabeba mabegi ya vigogo wachache wa upinzani
Ushauri
Vijana wote wa upinzani kutoka vyama vyote vya siasa tukutane
Tupindue meza angani tuunganishe nguvu kama vijana tumtafute na sisi malema wetu au bobi wine wetu tumssuport
Tuweke slogan yetu 2025 ni ya kibabe zaid vijana tupindue meza kibabe
Tuachane na hivi vyama vya mifukoni
Twende na chama letu vijana tutalipa jina huko mbele kwa mbele
Tukifanikiwa kuunganisha vijana nchi nzima na kuweka wagombea wetu vijana nchi nzima matembele awatoboi nakwambia kinyume na hapo ccm watakuwepo sana tu..
 
ukitazama vyuo vikuu watu wanahitimu kila mwaka wengi tu

kuna fani hata hazina ajira maalumu lakini zinafundishwa na hawa wakimaliza wanahangaika kweli mtaani kutafuta ajira.

ukombozi wa vijana unakuja
 
Back
Top Bottom