Mzigdash
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 440
- 377
Operesheni Wembley ni jina ambalo ilipewa operesheni ya usalama nchini Uganda mwanzoni mwa miaka 2001 ilikupambana na makundi mbalimbali ya uharifu kwa kuwakamata, kuwaweka kizuizini, kuwatesa na kuwaua majambazi wenye silaha.
Raisi wa Uganda Y. Miseveni alianzisha operesheni hiyo Maalumu baada ya kuwepo kwa vikundi mbali mbali vya ujambazi, wizi na mauaji katika jiji la Kampala.
Alimteuwa IGP Katumba Wamala Mwanajeshi aliyekuwa kwenye operatisheni Maalumu Nchini Congo.
Alimteuwa mkuu wa shirika la Ujasusi( ISO) Kanali ELLY KAYANJA. Kamanda wa Operesheni Wembley akisaidiwa na ASP Magara, Godfrey Musana, Bageya, Kanali Tusiime.

- Kanali Elly Kayanja alianzisha kikosi kazi maalumu chenye Wanajeshi, polisi na majasusi (ISO).
- Alianzisha vituo maalum vya mahojiano kukiwa na vyumba vya mateso vya siri katika barabara ya Clement Hill nyuma ya ofisi kuu ya MTN katikati mwa Kampala ambayo baadaye ilihamia kambi ya jeshi ya Kireka, matawi ya kikanda katika maeneo yote ya nchi.
- Mahakama maalum ya kijeshi iliundwa haraka huku Jenerali Tumwine akiwa Mwenyekiti wake. Mahakama maalum kwa ajili ya kuwahukumu washukiwa na kuwaweka kizuizini.
- karibu 95% ya washukiwa walikuwa walio fukuzwa jeshini, wanamgambo waliotokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Uganda 1986- 1994 na wale ambao jeshi liliwaacha kupitia mafunzo ya kijeshi.
- Operesheni Wembley ilifanikiwa kukamata siraha
- Operesheni Wembley ilifanikiwa kupambana na uharifu katika Jiji la Kampala na viunga vyake
- Operesheni Wembley ilifanikiwa kukamata takribani washukiwa 450 mpaka kufikia Novemba 2003 karibu 200 waliripotiwa kukabiliwa na kesi mbele ya mahakama za kijeshi zinazoundwa na maafisa wakuu wa jeshi.