Orders za nje

TZINVESTOR

Senior Member
Joined
May 29, 2014
Posts
106
Reaction score
23
Jamani nina order ya vitlfuatavyo:

1. kupeleka sangara Ulaya....kwa mwezi jamaa wanataka tani 50

Je naweza kupata contacts za wauzaji?

Je kwa kilp moja dola ngapi?

2. Nahitajo kununua gold...toka kwa wachimbaji wakubwa au serikali.

Hii ni serious deal tukikubaliana kila kitu laIma kitapitiwa na assayers kisha malipo yatafanyika.

Kiaai...tunataka kuanzia kilo moja ans above...

3. Pia kwa watu mliopo nchi za Nje na husuaana arabuni. Client anahitaji LNG lakini sisi role yetu ni introduction tuu kisha we are out....

4. Nahitaji matunda ya aina mbali mbali kwa ajilinya kupeleka ulaya. Bei na mengineyo ni maelewano


Kama kuna mtu anaona anahitaji kuongea zaidi bas anaweza kunitumia PM..lakini nataka watu serious only.


Asanteni
 
mkuu matunda gan hasa unayohitaji
 
Mimi ninauwezo wa ku suply matunda aina ya machungwa , na mapapai, je utayafuata hapa shambani?
 
Sidhani kama Ulaya wananunua samaki Kama vile wanavyouzwa kigambani
 
Ndugu unaejiita jina kubwa la TZinvestor bado hujajipanga,na sijui kama sio dalali ambae amevamia asichokijua,maana ni sawa na dadali wa nyumba kupangisha nyumba hata kama ina majini na haikaliki.

Kwanza tuambie kampuni yako inaitwaje,maana mbwembwe kibao.
Nidokoe tu pale kwenye Gold,unasema unataka Gold kutoka kwa wachimbaji wakubwa au Serikali,Mhhhhhh
Yaani wewe TIC hupajui au?au wauzaji wakubwa na wadogo wa dhahabu Tanzania wanahitaji Tochi kuwajua walipo.
Maana mie sio biashara yangu ila kesho tu nikitaka nawajua wote.Sasa inakuwaje wewe mwenye mtandao huu usiwajue.
Na pili Gold upande wa Serikali inamaana hapa unataka kufanya bisahara na Serikali,sasa Wizara ya Madini huijui pale.

Acha usanii,

Umenifurahisha kitu kimoja tu,kwamba unataka watu walio Serious tu,duhhh,
Tanzania eeeeeeeeeee,nakupendaaaaaaaaaaa,nchi yangu eeeeeeeeeeeeeee
Haya karibu kaka
 
Habari za toka jana wadau

Naomba niweke wazi mambo yafuatayo.

Hizi orders mara ny8ingi hufanywa na watu wenye asili ya Asia kupitia netweks zao na sasa sisi waswahili tumeizipata na sioni ubaya kufanya au kutumia nafasi hizi

Hivi mnajua kama Yusuf Manji ameajiri watu 100 ambao kazi yao ni kupitia na kuchanganua tenda zote za serikali ya Tanzania na wao kuwa madalali wa hizi procurements.

Sasa kusema kuwa mimi nina resources na capacity kama YA yusuf manji nitakuwa mwongo na mimi napigana ninavyoweza na kwakuonyesha sina hiyana wala matatizo nimeona bora ni share nanyinyi wenzangu ili tuangalie...mwenye connection na aliyekuwa na uwezo tufanye kazi pamoja.

Binafsi sipendi kujishulisha na kufanya kila kitu hivyo naangalia kama muunganishaji (wazungu wanaita FINDERS FEE) nitalipwa changu kisha naaanza.

Pia sijapendezwa na kauli za kejeli za kuwadharau madalali zilizotolewa na baadhi posters. Tusisahau kuwa hao mnaowaida madalali ndio hao hao wanaitwa BROKERS na sidhani kama kuna ubaya mtu kuwa DALALI ...as long as kila mmoja analipwa kwa jasho lake

sasa mimi nimebahatika kupata hizi orders lakini kwa kazi kama hiyo ya Dhahabu siijui inakwenda vipi ndio maana nimeuliza. Ni kweli ningeweza kuwauliza TIC lakini nikishakwenda TIC inamaana wengine humu watakuwa hawatopata kitu.

sasa order imetoka kwa watu wa uhakika lakini sharti lao ni kuwa hawataki ku deal na ma middle men wengi. ila wao watatoa finders fee kisha wao watadeal na hao wauzaji direct....je kuna ubaya gani mimi kuulizia hilo?

Pia nimeulizia kuhusu Sangara na naweza kusema kuwa hii haina matatizo ila pesa yetu tutatengeneza kwenye bei per kilo....sidhani kama hilo nalo ni tatizo na lipo ndani ya uwezo wetu kwani mimi ni muumini wa kidogokidogo hujaza kibaba...mtu ukipata dola 10,000 za uhakika ni bora zaidi kuliko dola laki moja ambazo haziji mpata upite muda mrefu.

Na pia sioni ubaya kutaka ku deal na watu serious.
 

Kuhusu dhaabu piga hii no 0768832945
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…