MWINYI aliwekwa atawale Zanzibar kwa mwaka mmoja tu, alipoonekana anafaa ndio akaletwa huku Bara kumrithi Nyerere.
Ila hapo Wazanzibar hawatoisahau awamu ya Rais Salmin Amour " Komandoo " huku Mohamed Gharib Billali akiwa Waziri Kiongozi, ulikuwa ni utawala wa mkono wa chuma, damu ilimwagika, watu walipotea na baadhi ya wapemba walikimbia Nchi wakakimbilia Mombasa.
Kweli nyakati huja na kutoweka. Apumzike kwa amani Idris Abdul Wakil Rais mpole na muungwana kuwahi kutokea Zanzibar na ndio maana haishangazi alikuwa Rais wa awamu moja tu.
Zanzibar ina historia kubwa sana ambayo watawala wanajitahidi kuificha sana!